Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Niliwahi kuandika humu na ninaandika tena; kiwango cha Jose mourinho hapo ndio mwisho , hana ufundi. Tactics zake zipo outdated na hakuna la ziada tunapaswa kutarajia.



Ni muda wa kocha kujitafakari Mara 2
Akijitafakari ndyo mtaacha ku draw?
 
76191eb42e4cb0245407d4ca0ab81a24.jpg
 
Mimi sioni tatizo la wachezaji hapa lazima kuna kitu mbona ligi ilivyoanza timu ilikua inacheza vizuri sana?? Matokeo safi kabisa sasa hivi tatizo nini??
Timu haibadiliki kiuchezaji inamaana soton wana wachezaji bora kuliko man u? Hapana!!! Tatizo nini KOCHA..............


Nadhani Hapa Waweza Jifunza Kitu:
↓↓
 
Kumbe uliliona hilo tegemezi wake alikua big fella sasa hayupo. Timu inashindwa kucheza hata pasi 5 murua mbele pale yani dah.
Tukubali tu Mou kufundisha mpira wa ufundi hawezi na ndo sababu ya wachezaji wengi viwango kushuka kila siku.
Ukisema mou hawezi kufundisha mpira wa kisasa,wanakupinga,wanasema hatuna wachezaji...
 
Ni muda wa mou kusepa...hivi mmeona post press conference yake alivokuwa anaongea upumbavu?....analialia kuhusu penalt,na kuwalaumu tu marefa,wakati mpira tuliocheza jana tulikuwa tunastahili kufungwa..
 
Mkufunzi wa manchester United Jose Mourinho amekiri kwamba mshambuliaji Romelu Lukaku amechoka lakini ng'o hawezi kumpumzisha.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 amecheza kila dakika za mechi za Man United kufikia sasa kutokana na matatizo ya majeraha yanayomkumba mshambuliaji mwenza Zlatan Ibrahimovic.
Lukaku alianza msimu na mabao 11 katika mechi 10 lakini kufikia sasa amefunga magoli manne katika mechi 19.

''Kijana amechoka, ana nguvu nyingi sana lakini sasa zimekwisha na anahisi amechoka'', alisema Mourinho. ''Mchezaji huyu ni mzuri sana .Lakini siwezi kumpumzisha''.

Lukaku amehusishwa na makosa katika lango la timu yake katika wiki za hivi karibuni ambayo yamesababisha mabao kwa upande wa Manchester City na Burnley.

Lakini mkufunzi huyo wa United alikataa kumkosoa mchezaji huyo wa Ubelgiji akisema kuwa makosa hayo huenda yamesababishwa na uchovu.
 
Mkuu im very sorry for You...

Pole sana Mkuu
Tumwombe Mungu tusitoke hata hapo ndani ya 4.

Ila ukweli usemwe,, Timu imemzid Mkufunzi...

Hatuna wachezaji wa kuendana ma falsafa yake
Inter alikua na kna Zennet,, Lucio,, Chivu,, Maicon,, nw
Chelsea part One walkuepo kna Makelele,, Essien,, Cole,, JT, nw

Madrid alianza huo upuuzi akachemka akaishia kuwafanya wawaone Barcelona maadui wao katika sayari hii ya tatu... Ili hali mpira unapigwa peupe

Martial unataka awe mkabaji?? Mkhi kweli utauona ubora wake ili hali mda !mwingi kaambia akumbuke kukaba??
Tutawalaumu sana wachezaji but mbinu za Mwalim nazo mhhhhh!!!

Kama sio Matic,, Kama sio David Mwakamwa 2018 mwanzoni Kabisa Josee asngekua Mkufunzi wa Manchester United..


Nilichokibaini ni kuwa Josee kajitaidi sana kuijenga timu na ni moja ya ndoto zake viatabu vya kumbukumbu vya soka kumwandika kama moja ya makocha waliowahi kufanya vizuri akiwa Manchester United..

Ila,,,

Manchester United ni kubwa kulko Josee tuwe wakweli!!

Let say akapewa Hyo Bale,, au Perisic,, Griez au Dyabala ni kweli atatoka hapo??? Mkhi kashindwa kumtu!ia,, Mata as well ije kuwa Ozil tunaemjua???

Mbinu zake zmepitwa na wakati na wachezaji wa mbinu zile hawapo tena,,.. Walau unapaki Bas upo na tmu hatar,, sio Leicester Walio pungufu tena kiungo....

Utd Forever
Kweli chief watu wakushambulia wote anataka wakabe...
 
Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho amehoji madai ya mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp's ya mwaka 2016 kwamba yuko tayari kuwacha kazi yake badala ya kutumia fedha nyingi kununua wachezaji.

Liverpool inajianda kumsajili Virgil van Dijk kutoka Southampton kwa kitita cha £75m mnamo mwezi Januari, kitita ambacho kimevunja rekodi ya dunia kwa upande hamisho wa beki.

Klopp alisema siku ya Ijumaa kwamba kitu cha mwisho anachofikiria sio gharama kwa sababu wanampenda mchezaji huyo.
Aliongezea: Unapatiwa bei na ni lazima ukubali.

Hatahivyo Mourinho alitumia mkutano wake na wanahabri kuzungumzia kuhusu matamshi ya Klopp aliyotoa wakati United ilipomnunua Pogba kwa dau la £89m kutoka Juventus mnamo mwezi July 2016.

Klopp alinukuliwa akisema kwamba hawezi kununua mchezaji ni kiwango cha juu cha fedha na iwapo soka inaelekea katika mwelekeo huo basi huenda akawacha ukufunzi.
 
Tetesi
RONALDO KURUDI MAN UNITED?

Manchester United wanafuatilia kwa karibu ripoti za tofauti baina ya Cristiano Ronaldo na viongozi wa Real Madrid, kimedai Mirror .
Magazeti yanasema kuwa uhusiano baina ya Ronaldo na Florentino Perez umevunjika, jambo linaloleta shaka juu ya mustakabali wake Bernabeu.
Na United wanaweza kupata fursa ya kumrejesha mchezaji waliamjenga wenyewe ikiwa atakataa kubaki Hispania.

Imedaiwa kuwa Ronaldo amekuwa akifanya safari za siri kwenda Uingereza na kuangalia shule binafsi kwa ajili ya kijana wake wiki za hivi karibuni.
 
Tetesi
JOAO MARIO KURITHI NAFASI YA MKHITARYAN?


Nyota wa Inter Joao Mario ameingia kwenye arada za Manchester United wakitaka kumsajili kuziba pengo la Henrikh Mkhitaryan, kwa mujibu wa Sun .
Hali si shwari kwa kiungo huyo wa kimataifa wa Armenia katika Old Trafford, na klabu nyingi zinaitaka saini yake.
Ikiwa atatimkia Serie A, United watafanya jaribio la kumsajili Mreno wa Nerazzurri kwa kiasi cha paundi milioni 40.
 
Tetesi
RONALDO KURUDI MAN UNITED?

Manchester United wanafuatilia kwa karibu ripoti za tofauti baina ya Cristiano Ronaldo na viongozi wa Real Madrid, kimedai Mirror .
Magazeti yanasema kuwa uhusiano baina ya Ronaldo na Florentino Perez umevunjika, jambo linaloleta shaka juu ya mustakabali wake Bernabeu.
Na United wanaweza kupata fursa ya kumrejesha mchezaji waliamjenga wenyewe ikiwa atakataa kubaki Hispania.

Imedaiwa kuwa Ronaldo amekuwa akifanya safari za siri kwenda Uingereza na kuangalia shule binafsi kwa ajili ya kijana wake wiki za hivi karibuni.
Ataweza kuzuia mda wote ? Kama hawezi bc ajue hana namba
 
Tangu Web astaafu EPL man u ni maboya tu na mnazidi kurudi kwe nafasi yenu mlozoea

Web alicheza uefa na kikombe cha dunia ngaz ya vilabu? Hoja mufilisi unajipoza machungu timu haina wachezaj hiyo ndo hoja ya msingi
 
Nadhani kuna sintofahamu kati ya wachezaji na huyu molinyo. Haya matokeo si bure
 
Tetesi
Manchester United inamchunguza kiungo wa kati wa Napoli na Itali Jorginho, 26, ili kuchukua mahala pake Michael Carrick. (Manchester Evening News)
 
Tetesi
Mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge anapendelea uhamisho wa Southampton lakini anahofia United itazuia uhamisho wowote chini ya £25m. (Daily Mirror)
 
Back
Top Bottom