Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

romelu-lukaku-manchester-united_10zlr3j449ewu17a6p6whyj3g7.jpg
 
WHAT'S NEXT FOR UNITED?

The Reds travel to Alan Pardew's West Bromwich Albion on Sunday 17 December, with kick off at 14:15 GMT, with the Baggies buoyed by a goalless draw at Liverpool.
 
Shida ni Moja naona kama watu wanamchukia Jose kwa sababu zao binafs especialy kwa ile hulka yake ya Ujeur ila most of the time anaangalia matokeo na mafanikio yake,
Huwez kusema wewe ni kocha bora huku umeshida Kombe la FA wakat mwenzio msimu wake wa kwanza amechukua Europa Cup na League Cup.
LVG alijua kutuchezesha mpira wa mapasi meng bila kuwa na magoli ila kwa jose tuna direct footbal huku tukiwa na magoli meng ya Kufunga
Mfumo wa Pep ni huo attacking n possesing hawez kubadilika kamwe na hakuna wa kumbadilisha na Jose nae ana mfumo wake ambao hauwez kubadilika
Kama mnakumbuka Inter Milan anamtoa Barca kwenye Champion League kwa style ya kupak bus kila mtu alimsifu Jose kwa maana alijua nn anataka na mwisho wa siku alienda kuchukua Champions League Trophy
So Jose abakie na mfumo wake ambao umekuwa ukimpa mafanikio siku zote na Pep atabakia na mfumo wake ambao umekuwa unampa mafanikio hzi kelele za kutaka Man utd wacheze kama Man city zitabakia siku zote ila ni kitu ambacho hakitakuja kutokea kama hii team itabakia china ya Jose
Aisee sidhani kama ni kweli watu wanataka Man U icheze kama City, watu wanataka Man U iende na ishambulie kwa sababu wachezaji wa kufanya hivyo pale wapo, na siyo Man U inayofunguka inapocheza na Bournamouth halafu ikicheza na top 6 teams inajifungia nyuma halafu tukitoka hapo tunalaumu Lukaku
 
Man utd hatutaki kucheza kama Man city, tunataka tucheze kama Man utd, ile ye Babu Fergie, Babu Fergie nae possession footbal sio style yake, yeye ni mashambulizi tu, ukipata mpira unatakiwa ufanye ufike mbele, Babu Fergie hataki kutia udi kabisa...... Na sio kwamba hawezi au hajui kuchezesha Possession anaweza vizuri sana tu, Ila shida yake ni mashambulizi. Na hata ukiikuta Man utd imecheza na Man city na kufungwa, lakini Under Fergie unajua kuwa ama timu ilizidiwa maarifa, au ilikuwa siku ya kufa nyani tu. Lakini under Jose, unapokutana na timu kubwa yoyote, basi tayari ameshaset mentality yake kuwa tuondoke na point 1 ishatosha, THIS IS NOT MAN UTD!!!
Daaa ndugu umeongea kwa uchungu na ukweli mtupu, mimi sijui wanaomtetea Mou kwa hii staili ya uchezaji wanapata wapi uhalali huo. Nadhani hata utamaduni wa klabu yao ule ambao mashabiki pale OT wamekuwa wakifanyia chanting Attack! Attack! Attack! Hawaujui.
 
Kwaio Mourinho wa chelsea kipindi ndo anajoin hio team alikuwa ana paki basi na hakuna mashambulizi kabisa? Mourinho yule ilikuwa akikutana na timu kubwa alikuwa anatafuta droo tu hakua na attacking mind? Alikuwa akizi approach timu kubwa kwa woga? Ndivo alivokuwa vile?
Chelsea iliyochukua ubingwa kabla Mou hajafukuzwa ilikuwa ina shambulia sana. Hata Real Madri ya Mou iliyoanza kuifunga barca ilikuwa inashambulia na kumiliki mpira kwa kiasi fulani.
 
Hili ndio kosa ambalo masahabik weng wa manchester utd tunalifanya zama zimebadilika sio kila siku tutahtaj kile alichokifanya SAF bas makocha wengne nao wafanye hvyo hvyo hatutakuwa tunawatendea haki kabisa

Hata SAF alipkuja Man utd alikuta kuna kocha amabae alikuwa na falsafa yake what if nao wangetaka wacheze kama ilivyokuwa kwa kocha wa nyuma

Tuna bahat mbaya weng kizaz chetu kimeona zaid mafanikio ya SAF kuliko kocha mwengne ila ilfika kipind aliona kabisa utawala wake umefika kikomo amuachie mtu mwengne

SAF alwah kuhojiwa kama angekuwa kocha kipind hik man utd wangemvumila kwa misimu mitatu ya mwanzo bila kuwa na kombe kwa mdomo wake alisema hapana angeshafukuzwa kwa aina ya mfumo wa soka la sasa ulvyo

Wamiliki wa team mashabik wanaangalia mafanikio ya team kwa ujumla wake leo hii ucheze soka la kushambulia na bado huna kombe hata moja hakuna ambae ataoenda kuwa na kocha wa namna hyo

Mourinho ana mfumo wake na sio kwamba ulianzia man utd hapana alikuwa nao toka alipoanza kufundsha soka bas na yeye anataka kutengenza legacy yake kupitia huo mfumo kwa maana ndio ambao umekua ukimpa mafanikio siku zote
Na wewe unapouhusudu huo mfumo wako na Mou ukumbuke kwamba ni kweli zama zimebadilika na huo mfumo unafeli pia. Kumbuka wakati Mou ameanzisha huo mfumo wenu alikuwa ana concede goals kirahisi? Alikuwa anapoteza game kirahisi? Alikuwa anakoswa koswa magoli mengi ya wazi ktk kila game alyocheza huo mfumo? Utagundua ni BIG NO! sasa mbona sasa anafungwa ktk huo huo mfumo wenu kirahisi na timu ya inakuwa exposed sana kwa maadui hasa hasa kwenye defence? Yani unaita cjui kupaki basi, sijui meli halafu wapinzani wanatengeneza nafasi nyingi za magoli ya wazi Mungu anaingilia kati tunakoswa? Refer back game ya liverpool tulitoka droo ila jamaa walikosa magoli ya wazi kabisa, Totten tukawafunga dk ya 85 na tuliruhusu pia walitengeneza nafasi za wazi, chelsea tukacheza nao hivyo tukafungwa, Arsenal tukacheza nao mfumo huo na De gea akafanya saving nyingi kwa game moja hadi kuwazidi makipa wengine wengi ktk game zote walizocheza msimu huu, na wengine bado hawajamfikia, hapo ni Mungu aliokoa jahazi. Tumecheza na City kwa mfumo huo huo tumefungwa tunasema wamebahatisha. Tusipoangalia hata kwa Sevilla tutapaki basi na tutatolewa Champions league.
 
Leo Mou kanisikiliza, badala ya kuwaweka Rashford na Martial kamuweka mmoja na Mata ambae atasaidia creativity all round.
Asee Mou hasikilizagi mtu ngoja siku ampange Mata tukiwa tunacheza na Chelsea halafu amwambie huyo Mata acheze namba sita na marufuku kwenda mbele ndo utaposhangaa. Ile siku tumecheza na City nlivoiona lineup yetu nikasema leo ni mwendo wa viberenge tu na cty watahema leo duuu!!!
 
Sifa za mashabiki wa man u;
1.Hawajui mpira,wengi wao hufuata mkumbo
2.Wanaongea sana kuliko uwezo halisi wa timu yao utawasikia leo tunashinda 4g halafu wanashinda 1g au wanapata kipigo kabisa
3.Ni mabingwa wa kuvamia thread za watu hata kama wao hawana mechi halafu mambo yakiwaendea kombo huingia mitini tafikir hawapo
4.Wakifungwa mechi husingizia mchezaji fulani hayupo eg PP
5.Timu yao haijui kucheza mpira ila wanalazimisha ionekane inajua utasikia man city tuliwabana walitubahatisha magoli tuliwapa pasi sisi,mara hatutaki kuposses mpira tunacheza mpira wa mashambulizi wa fergie halafu wanaambulia shots on target 4 mechi nzima
Ushauri:Hamuwezi kupambana na city na sasa mnatakiwa kupambana ili mshiriki uefa next season
Sifa na 6. Hawa mashabiki wanaishangilia timu yenye mashabiki wengi zaidi duniani
7. Wanashabikia timu yenye kuuza jezi nyingi zaidi duniani
8. Timu yao ina vikombe vingi zaidi vya ligi yauingereza kuliko timu zingine za ligi hyo.
9. Kuna uwezekano mkubwa wa hawa mashabiki kuendelea kufurahi kwa timu yao kuingia robo fainali ya UCL. Nyinginewengine wanajua na watazisema
 
Daaa ndugu umeongea kwa uchungu na ukweli mtupu, mimi sijui wanaomtetea Mou kwa hii staili ya uchezaji wanapata wapi uhalali huo. Nadhani hata utamaduni wa klabu yao ule ambao mashabiki pale OT wamekuwa wakifanyia chanting Attack! Attack! Attack! Hawaujui.
Hakuna wanaomtetea Mourinho tunaongea reality then dont try to compare SAF na makocha wengine kwenye EPL hakuna wa kumfananisha nae alishai-master EPL kuna mechi alipanga karibia timu nzima mabeki lakini alimfunga Arsenal goli 4

1.Mourinho is still Mourinho sijaona alichobadilika since akiwa Chelsea -Inter-Madrid-Chelsea anacheza mpira kwa approach ile ile tofauti ni quality ya wachezaji aliokuwa nao kwenye hizo timu alizopita.

Siku zote Mourinho mfumo wake timu haitengenezi nafasi nyingi lakini conversation ni kubwa sana mfumo unahitaji striker/midfield akipata chance moja ni kufunga tofauti na sasa ambapo Lukaku anakosa sana magoli ya wazi

Since SAF ameondoka at least now United imeanza kurudi kuwa big team in Europe although still bado kazi inahitajika
 
City wameweka rekodi mpya Ligi ya Uingereza baada ya kushinda mechi ya 15 mfululizo lakini Jose Mourinho amesisitiza kuwa mbio bado hazijaisha
Jose Mourinho amedai kuwa mbio za taji Ligi Kuu Uingereza bado hazijafika mwisho na amesisitiza kuwa angekuwa kwenye likizo sasa kama Manchester United ingekuwa imekata tamaa.
Mashetani Wekundu walirudi kwenye njia za ushindi baada ya kichapo cha Manchester City kwa kuifunga 1-0 Bournemouth Jumatano usiku, shukrani kwa goli la kipindi cha kwanza la Romelu Lukaku.

Hata hivyo, Citizens wameweka rekodi mpya Ligi Kuu Uingereza kwa kushinda mara 15 mfululizo baada ya kuichapa 4-0 Swansea City usiku ambao waliendeleza pengo la alama 11 dhidi ya United kileleni mwa msimamo.
"Nimefurahishwa na pointi tatu, ilikuwa mechi ngumu," Mourinho aliiambia BBC Sport. "Walikuwa na siku moja zaidi ya kupumzika kuliko sisi, walikwa wamepumzika vya kutosha kuliko sisi, na utulivu wa akili kwa sababu mechi kubwa huwachosha zaidi wachezaji wetu.

Tulikuwa na nafasi, [Anthony] Martial alikosa nafasi nzuri, [Marcus] Rashford angefurahia matunda ya jitihada zake, na dakika 15 za mwisho walitushinikiza.
"Nilisema tunacheza mechi baada ya mechi na kila mechi tutajitahidi kushinda, tunajaribu mechi baada ya mechi. Mbio zinaisha tu baada ya mwezi Mei, kama mbio zimekwisha basi naenda Brazili au Los Angeles."

Mechi inayofuata Man United Ligi Kuu Uingereza watasafiri kwenda West Bromwich Albion Jumapili.
 
Romelu Lukaku ndiye mfungaji wa goli pekee la Manchester United dhidi ya Bournemouth kwenye ushindi wa goli moja kwa bila nyumbani Old Trafford
Luke Shaw na Scott McTominay walipewa nafasi ya kuanza kwa mara ya kwanza kwenye Ligi Kuu msimu huu, huku Ashley Young na Ander Herrea wakitokea benchi.

Katika mechi hiyo nafasi ya kwanza ilipatikana dakika 21 kama Charlie Daniels alimlazimisha David De Gea kufanya kazi ya ziada kuokoa shuti la umbali wa mita 2. Dakika 4 baadae, Mashetani wekundu walifanya shambulizi kali ambalo lilizaa goli kipitia kwa mshambuliaji wao Lukaku akimalizia krosi ya Juan Mata.
Baada ya goli hilo Bournemouth hawakubaki nyuma badala yake walishambulia na kushinikiza kusawazisha ingawa walijitahidi kutengeneza nafasi za wazi lakini hazikuweza kutumiwa vizuri.

Hata hivyo, ubao ulibakia 1-0 kwa vijana wa Jose Mourinho kwenda mapumziko wakiwa kifua mbele. United wangeweza kupata goli la pili katika dakika ya 59 lakini Anthony Martial alishindwa kutumbukiza mpira wavuni akiwa mita 6 baada ya mlinda mlango Asmir Begovic kutema kombora la Lukaku.
Kwa dakika 20 za mwisho, Bournemouth iliwaingiza washambuliaji wake Jermaine Defoe na Benike Afobe kwa lengo la kwenda kusawazisha kwa dakika hizo za mwisho.

Mchezaji Marcus Rashford ambayr aliaanzia nje kwenye mchezo huo kidogo aipatie goli timu yake kuguatia shuti lake kali kumshinda mlinda mlango wa Bournemouth na kugonga mwamba katika dakika ya 72.
Mashetani hao waliendelea kutawala kwa kipindi cha pili kabla wageni hawajabadilika dakika za mwishoni na kuanza kuwapa presha wenyeji.
Hadi 90 zinamalizika, United walifanikiwa kuondoka na ushindi wa goli moja kwa bila na kurudisha ile hali ya ushindi
 
Back
Top Bottom