Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Tetesi
ALEX SANDRO ANATAKA KUTUA CHELSEA


Beki wa Juventus Alex Sandro anapendelea kwenda Chelsea kuliko Manchester United, kwa mujibu wa The Sun .
Blues walishindwa kumpata beki huyo wa Kibrazili majira ya joto, na kuipa United fursa ya kumfukuzia mchezaji huyo lakini anatamani kutua Stamford Bridge Januari.
 
Wakuu Mou ni kocha mzuri kulingana na historia yake ila anamapungufu mengi..Nakumbuka siku tumetangaza kumpata huyu Mou sikuwa na furaha kihivo maana nilijua kuna ladha tutaikosa sidhani kama kulikuwa na ulazima wa kupaki basi kwa city ambao walionesha kuwa na tahadhari mda mwingi....mpaka tufungwe ndo tuanze kushambulia,mimi binafsi nilipendelea zaidi aje Diego simeone wa Athletic wengi wakapinga kuwa anafika fainal ila hajawahi chukua kitu,jamaa anatengeneza sana wachezaji mentally na anacheza mchezo wa kuvutia sana tena sana...mou yeye anapandikiza wazimu wachezaji wanaenda kujitoa muhanga tukifungwa lawama tu...sikumbuki ni member gani alisema hadhani kama mou anastahili saaaana kuongezewa mkataba Man u maana inaumiza sana wakuu tumepoteza aina ya mchezo wetu na confidence yetu kabisa,,,man u sio ya kupaki bus man u ya kushambulia,man u sio wa kutegemea bahati...Mou anazingua sana man u kwa fujo za city tunaonekana sisi ni genge la wahuni fergie asingeweza kuja kufanya haya daima..
 
G Neville: "I've only read reports about LvG's quotes on United's style but my personal view is that the football under Jose is going in a better direction. Also, in terms of results, JM has won a European trophy & has the team second in the league, so he's also more successful."
 
Anaesema kuw City kafungia bahati simuelewi kabisa. Ulitaka ufungwej ndo ukubali kuw ujafungiw bahati?

Ukawa mpo wengi ila kwa woga wenu mnakuja hadi myapate matokeo mnabadili na avetor kipind mnapokea vipogo vya wakina everton wala hamkuwepo


MASHABIK MATOKEO NYIE wengine mnafungua account mpya kuja kivingine baada ya matimu yenu kupoteza uelekeo city tz na africa kawapata wapi mashabiki?
 
Ukawa mpo wengi ila kwa woga wenu mnakuja hadi myapate matokeo mnabadili na avetor kipind mnapokea vipogo vya wakina everton wala hamkuwepo


MASHABIK MATOKEO NYIE wengine mnafungua account mpya kuja kivingine baada ya matimu yenu kupoteza uelekeo city tz na africa kawapata wapi mashabiki?
Mtazamo wako. Maoni yako. Mawazo yako. Vyote haki yako. Mim shabiki wa City na sijawahi hama team yoyote EPL.
 
Manchester United break silence on Romelu Lukaku accusations

Jose Mourinho has defended Manchester United striker Romelu Lukaku after his disastrous derby debut on Sunday.

Lukaku contributed to both of City's goals in the 2-1 defeat and spurned a presentable chance to equalise in the 86th minute.
 
G Neville: "I've only read reports about LvG's quotes on United's style but my personal view is that the football under Jose is going in a better direction. Also, in terms of results, JM has won a European trophy & has the team second in the league, so he's also more successful."
Shida ni Moja naona kama watu wanamchukia Jose kwa sababu zao binafs especialy kwa ile hulka yake ya Ujeur ila most of the time anaangalia matokeo na mafanikio yake,
Huwez kusema wewe ni kocha bora huku umeshida Kombe la FA wakat mwenzio msimu wake wa kwanza amechukua Europa Cup na League Cup.
LVG alijua kutuchezesha mpira wa mapasi meng bila kuwa na magoli ila kwa jose tuna direct footbal huku tukiwa na magoli meng ya Kufunga
Mfumo wa Pep ni huo attacking n possesing hawez kubadilika kamwe na hakuna wa kumbadilisha na Jose nae ana mfumo wake ambao hauwez kubadilika
Kama mnakumbuka Inter Milan anamtoa Barca kwenye Champion League kwa style ya kupak bus kila mtu alimsifu Jose kwa maana alijua nn anataka na mwisho wa siku alienda kuchukua Champions League Trophy
So Jose abakie na mfumo wake ambao umekuwa ukimpa mafanikio siku zote na Pep atabakia na mfumo wake ambao umekuwa unampa mafanikio hzi kelele za kutaka Man utd wacheze kama Man city zitabakia siku zote ila ni kitu ambacho hakitakuja kutokea kama hii team itabakia china ya Jose
 
Inawezekana kweli simjui Mourinho. Kwani si ndio yule alooneshwa kwenye CNN anamfunga kitanzi Saddam?
Jose hajabadilika bado anacheza mfumo uleule tangu aanze kufundisha soka nashangaa unasema Mourinho wa Chelsea ni tofauti na huyu wa sasa
 
hzi kelele za kutaka Man utd wacheze kama Man city zitabakia siku zote ila ni kitu ambacho hakitakuja kutokea kama hii team itabakia china ya Jose

Man utd hatutaki kucheza kama Man city, tunataka tucheze kama Man utd, ile ye Babu Fergie, Babu Fergie nae possession footbal sio style yake, yeye ni mashambulizi tu, ukipata mpira unatakiwa ufanye ufike mbele, Babu Fergie hataki kutia udi kabisa...... Na sio kwamba hawezi au hajui kuchezesha Possession anaweza vizuri sana tu, Ila shida yake ni mashambulizi. Na hata ukiikuta Man utd imecheza na Man city na kufungwa, lakini Under Fergie unajua kuwa ama timu ilizidiwa maarifa, au ilikuwa siku ya kufa nyani tu. Lakini under Jose, unapokutana na timu kubwa yoyote, basi tayari ameshaset mentality yake kuwa tuondoke na point 1 ishatosha, THIS IS NOT MAN UTD!!!
 
Back
Top Bottom