Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Kama mtu amesha undergo medical checkup hivi bado kunauwezekano kweli wa kubadili maamuzi?
 
Screenshot_2017-07-08-09-17-48.png
 
Rekodi ya ufungaji ya Lukaku kwa umri wa 24 kwa musimu wa 2016/17 inatisha. Hebu tuangalie wachezaji wengine walifunga magoli mangapi kwenye umri huo:-

( Mechi -Magoli)
Lukaku - 374 - 165

Messi - 446 - 253

Ronaldo- 290. - 233

Drogba. 83. - 18

Zlatan. 291. - 110

Rooney. 427. - 174

Suarez 282. - 164

Lewandowski. 343. - 170

Thiery. 351. - 125

CR7. 393. - 145

Aguero. 379. - 170

Higuan. 291. - 134

Owen. 363. - 186

Shearer. 302. - 141


Screenshot_2017-07-08-09-07-53.png
 
Kiukweli sijawahi muona lukaku aki perform kiuanaume katika mechi kubwa. Namuona ni mchezaji was mechi ndogo. Hyo inantia wasiwasi kwenye UCL

Kuperform vizuri mechi kubwa inategema na uwezo wa kikosi cha timu hasa eneo la kiungo. Sasa Everton wana viungo wazuri kuliko Arsenal,Chelsea,Man United,Man City? Unategemea Lukaku ata perform vipi vizuri?
Ubora wa kikosi unamuongezea mchezaji uwezo wa kucheza vizuri.
Kama kwenye kiungo una mtu kama Pogba,Herrera,(Matic),Micki na Mata hivi utashindwa kuperform vizuri?
 
Japo sijawahi changia humu jukwaani ila kwa hili naomba nichangie kidogo kwa ufahamu wangu.

Navyo jua jinsi timu zinavyo sajili wachezaji kwa bei kubwa na mishahara mikubwa hii inapelekea gharama za uendeshaji wa timu kuongezeka. Kwa kuongezeka huko gharama mauzo ya TV rights zitapanda sababu timu ni brand na gharama ya kuendesha hiyo brand imepanda. Kwa hiyo mfano DSTV itabidi alipie gharama kubwa hali itayo pelekea na wao kupandisha bei za huduma. Mwisho wa siku sisi wa kibnda umiza tutakuja kulipia bandani pale. Sasa katika hiyo scenario usiombe na thamani ya pesa yetu ishuke dhid ya dollar.

Kwa hiyo kwa namna moja au nyingine na sisi inatuathiri.
Real Madrid Wamewahi Kuvunja records za usajili miaka nenda rudi kuanzia kipindi cha zizou, kaka, Cristiano Rinaldo mpaka Gareth Bale ila hatukuwahi kushuhudia hicho unachokizungumzia wewe.

Arsenal licha ya kutokuwa team inayomwaga hela kubwa kwenye transfer market ndio team inayoongoza uingereza kwa Ticket ghali / Bei kubwa ya kuangalia mechi zao pale Emirates stadium. Kama ingekuwa Transfer fee kubwa zina athari kubwa pale Manchester united tungeanza kushuhudia bei za ticket kushuhudia mechi pale Old Trafford zikiwa Juu, kwa sababu tangu amestaafu Sir Ferguson Manchester ndio team inayoongoza kwa kuspend kiasi kikubwa kwenye transfer market na mishahara.


Pia Manchester haijaanza Leo kuvunja record za transfer ... Mwaka 2002 Manchester walitoa paundi million 30 kumsajil Beki Rio Ferdinand. Akawa beki ghali duniani


Mwaka 2004 Manchester wakatoa paundi million 30 kumsajili Wayne Rooney akiwa chini ya miaka 18, akawa mchezaji ghali duniani chini ya miaka 18.... Hivi kuna team duniani inaweza kuthubutu kumwaga paundi hizo kwa mchezaji Mwenye miaka 16 ???? Manchester ilifanya ... Hizo zilikuwa big transfer spendings mkuu na hakuna matokeo ya hicho unachokizungumza... Sana sana sasa hivi dstv ndio kwaaaaaaAaaaanza mpaka kifurushi cha elfu 30 unacheki games


GGMU
 
Back
Top Bottom