Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Screenshot_2017-05-14-20-31-23.png
 
Carrick kama ndiyo dili basi ujue ubingwa next year ni majogoo. Midfielder lazima afunge au hata kutoa assist Carrick takwimu zake ni kimeo.
Unajuwa position ya Carrick msimu huu kweli?unamfannanisha na kiungo gani? Pamoja na umri kumtupa lakini Caric ni mmoja wa wachezaji waliocheza mpira katika kiwango cha juu akitimiza majukumu yako vema uwanjani,sema kutokana na kiwango kibovu cha timu msimu huu ndio kinachotufanya tuwaone wachezaji wote kuwa na kiwango kibovu,ila kwa mchezaji mmoja mmoja aliye perform ndani ya timu Caric tunampa nafasi nzuri na katika 10 kwangu anachukua 7 (7/10).

So jaribu kuangalia nafasi yake uwanjani na majukumu yake,je anatimiza malengo?

Mara nyingi huwa na jukumu la kutukiza kiungo chetu pale tunapopoteana hata tunapofungwa.

Labda nisaidie fact!!!!
 
Timu inacheza kama ya simuyu bana,hamna mipango kabisa,ovyo ovyo..Rooney,carrick,jones,smalling,lingard waondoke tu..martial,mikhitaryan,darmian blind pia wafwatie..hamna haja ya kukaa na wachezaji wanaobahatisha
 
Mpira umeisha

Spurs 2-1 Manutd
Sikutaka kuingalia hii match ya leo kutokana na kujua matokeo na lengo la timu katika match zilizobaki,Ki ukweli kama wengi walicomment Man U ndoto za kuwa ndani ya top 4 zilikoma mara baada ya match na Sunderland.

Baada ya hapo hatukuwa na cha kupoteza,ona akili,mipango na game plan za Mou katika EPL, ameshakubali na kuridhika nafasi tuliyopo,amenyoosha Mikono na amechagua kushindwa.

Sasa akili,nguvu na resources zote tunaelekeza katika fainal na Ajax,ndio tegemeo letu kubwa hapo May 24.

Kwa mara ya kwanza namuona Mou akirisk na kukubali kuachia kitu kimoja kati ya viwili hii nadhani ni kutokana na kuwa na kikosi finyu, uwezo wa wastani wa wachezaji wetu na majeruhi.

Nadhani ni muda wa kuwapa nafasi ya kupumzika wachezaji muhimu lakini kuwacheza akina Smalling na Jones kuona makosa yao na kuwapa game fitness kwa ajili ya match ya fainal .
 
Msimu wetu wa EPL uliisha siku tuliyotoka sare na Swansea. Kuanzia siku ile mechi zilibaki mbili vs Celta na vs Ajax.
Mechi nyingine zote ni warm ups kwa ajili ya mechi hio. Tukishinda hio mechi tunapata kombe ambalo hatukuwahi kupata na nafasi ya kucheza ECL.....its a NO BRAINER!
Endeleeni kujidanganya,sijui mkifungwa itakuwaje!
Maana hiyo ndiyo imekuwa sababu kuu sasa.
 
Hata huko UCL tukienda na wachezaji hawa hawa wasiokuwa na roho ya upambanaji sijui..
Wachezaji sio tatizo,roho ya upambanaji huumbwa au kutengenezwa,Babu kwa wachezaji hawa hawa ange chukua makombe na kucheza fainal UEFA,tatizo mbinu za kocha,Mifumo ya Mou mara nyingi ndio huwafanya wachezaji kuwa hivi,Ushindi wa magoli machache lakini kutokufungwa.

Hachezi soka la kushambulia ndio mana haihitaji wawinga katika vikosi vyake,huhutaji viungo wengi Zaidi tena Wenye kariba ya kukaba kama Fellain.

Nadhani kuna haja ya Mou kubadilika msimu ujao,na kuwa na mawinga na Viungo washambuliaji.

Nimesikia tete si za kuja kwa Gareth Bale Nadhani atashauriwa na msimu ujao anaweza kuja kivingine na kumpa nafasi Zaidi Pogba kucheza dimba la juu kuliko sasa kuwa nyuma ya Viungo washambuliaji.
 
Back
Top Bottom