Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Unaweza kuwa ni mapema mno kusema! Lakini Mou have to go, ameharibu timu kabisa, mbinu zake za kizee za kulinda goli na sub ya Fellaini mcheza foul mkubwa zimetukosesha ushindi. Sitaki Mou, aende zake.
Nani aje
 
anyway....... #_tutafika tu... yaani sometime I don't know what's wrong.....very bad performance in second time..... thanks De gea....... anyway thanks team Hata kwa Hili dogo nashukuru .....GGMU
Mr akiwa hana uwezo wa kukupa mimba na hana tiba chepuka ukipata mtoto bambikiza tu utafanyaje? Njoo huku hutaki on a sasa
 
Arsenal walipotoa draw vs Man Utd, Mourinho alisema alitamani angekuwa na a tall player on the bench hasa Fellaini angesaidia kulinda ushindi. Leo Fellaini aliletwa kulinda ushindi badala yake ameua ushindi.
Mpaka Leo umeshindwa kumuelewa huyu jamaa ni MTU wa chai
 
Huwezi kumchezesha pogba namba 10, kwa kweli huu ni ujinga na ilisha shindikana, kwa nini asi muingize mata!!? Kwa mfumo wa 4-2-3-1, Pogba angeweza kucheza 10 at least kama tuna tumia 4-3-3 ambapo awe ana cheza na mtu kama Pirlo au Carrick, hivi kweli kocha kama Mourinho hakufikilia jambo kama hili ambalo hata mimi naweza kufikilia!!?
This guy is finished hamna kitu hapo.

Inakera
Kaka sio kabila hiyo
 
1480926736451.jpg
 
Nashindwa hata namna ya kuelezea game ya jana zaidi ya hasira juu ya hasira.Mipango ya Jose kipindi cha pili ilikuwa mibovu labda tungesema kosa lake kubwa lilikuwa ukosefu wa uzoefu lakini hapana Jose ana uzoefu mkubwa katika soka kafundisha clubs nyingi kubwa.

Tatizo la Man ni kumtegemea sana Zlatan kupita kiasi,unaweza kusifu bao lake la jana lakini ukitazama dakika 90 alikuwa akifanya nini uwanjani unabaki kushangaa,hana uwezo wa kukaa na mpira,hana uwezo wa kupunguza mabeki,hana uwezo wa kukimbizana labda angeenda Seria A angefanya maajabu lakini si EPL.Man inajengwa around Zlatan nadhani ni kosa kubwa sana tena kubwa sana kwasababu huyu ni mchezaji mwenye umri mkubwa sana 36 anakwenda 37 muda si mrefu.Nashangaa Jose anamhitaji msimu ujao huu ni upimbi wa kupitiliza.

Sijui kwanini Mata hakuwemo katika kikosi cha jana,nasema sijui kama yupo mnazi wa Man tafadhali anisaidie maelezo mazuri yaliyo nyooka na si vinginevyo.Mechi ya jana Rooney alikuwa anatumikia adhabu yake Mata alitakiwa sana hii tabia ya Jose kupenda michezaji mirefu imepitwa na wakati kabisa na sioni akibadilika hata kiduchu sana sana namwona akizidi kuishiwa mipang kadri siku zinavyosonga mbele.

Gap baina yetu na top 4 inazidi kupanuka siku hadi siku.Mipango ya kucheza mipira ya kuzuia hata kwa timu kama Evaton inazidi kunichosha kabisa.Sub za jana zilituangusha sana kati ya michezo sita au saba mechi ya jana ilikubwa mbovu sana hasa kipindi cha pili.

Ifike wakati Jose atengeneze timu ya miaka 3 hadi 5 ijayo lazima umri wa wachezaji anaotaka kusajili wafit katika mipango ya MAN na si mipango yake ya muda mfupi.
 
Kwa hiyo unachotaka ni goli la ufundi ama? Goli la ufundi na lisilo na ufundi lina effect vipi matokeo? BTW, Ibra alitumia akili, baada ya kuona kipa yupo mbali na goli. Siyo wachezaji wengi wanaweza kufanya hivyo.

Maan, don't be so bitter and negative to the point of making a fool of yourself...maana kwa kung'ang'ania kusema goli la Ibra ni kosa la kipa, unasahau nilichokisema kwamba soka ni mchezo wa makosa: make ma mistake, opponents wana-capitalise kwa kufunga. Sasa kama unachokifanya siyo ku-discreti goli, basi nakuwa na mashaka na uelewa wako wa mpira.

Ebu nitajie goli 1 tu katika historia ya soka ambalo halikutokana na kosa la mchezaji au wachezaji wa timu iliyofungwa.



Okay, nifanye kukubaliana na hili. Akifukuzwa, what next? Who should take over?



1. José amfanyaje ili Pogba a-fit? Kwa United ya sasa, ni mido gani huyo aliye na kasi ili u-slowness wake usiathiri timu? Ni combination ipi ya midfielders ambayo itamfanya Pogba a-fit?

NB: unapotoa mfano wa Vidal na Pirlo, nani hapo alikuwa na kasi?

2. Bastian na Morgan: kwa hiyo unataka kusema hawa ndiyo wawe starting midfielders? Really? And you criticise José's tactics by bringing this? Unasema mechi nyingi wameonyesha umuhimu wao: kwa kuwa unapenda numbers, ebu thibitisha kauli yako kwa kuonyesha statistics zinazoonyesha umuhimu wa hao wawili walipocheza pamoja (na wala sikumbuki kama ilishatokea, I might be wrong though).

NB: unavyotaja hao madogo, unamaanisha watumiwe kama midfield combo na Pogba ama watumiwe kama midfielders kwenye starting eleven?

3. Morali na nidhamu ya timu: José afanyaje ili morali na nidhamu iwepo? What more should he do? Awaandaaje wachezaji? What if, amewafanya hayo, lakini wachezaji hawabadiliki? Ni wakati gani lawama zinapaswa kwenda kwa wachezaji pia? Maana ni rahisi kumlaumu kocha, huku ukisahau wachezaji nao wana-play a bigger role on the results.

4. Matabaka: you seem to know about what happens in United's changing room. Ebu tusaidie hayo matabaka yanayojengwa? Licha ya kukubaliana na wewe juu ya kutoweka mzigo mkubwa kwa Ibra (sababu kubwa ni umri wake), hilo la matabaka ni baloney, unless you prove it. Unasahau kwamba unaongelea professional players, ambao kila mmoja anafahamu nafasi yake kwenye timu. Kila timu lazima kuwe na superstar(s) ambaye anakuwa treated tofauti na wenzake! Hili haliwezi kuwa tatizo kwa professional players, hata kama kweli José anawapendelea Ibra na Pogba.

5. Henrik: unataka José amtumiaje zaidi? Toka amefika, muda mrefu amekuwa majeruhi! Games 2 zilizopita, Henrik kapewa playing time ya kutosha, na he didn't disappoint! Sasa unataka utumiweje zaidi?


I have never seen a football club's fan this bitter, negative and pessimistic about his/her team. Honestly, you are just hurting yourself, especially knowing that no matter how bitter and pissed you are, you will have no IMPACT on what happens at United! The best thing you can do, is to enjoy the moment, feel sorrow for bad days in the office, and MOST IMPORTANTLY, be rational.

1.Goli la Ibra, narudia kuwa sija discredit goli lake ila nasema, goli lilitokana na Keepers error zaidi rather than ufundi binafsi wa mchezaji. Najua wewe ni muangaliaj mpira mzuri lakini unavo yachambua magoli ujue kuna vitu kama
Individual error au skills
Team error au skill
Communication error au skills

Kufunga goli kuta taka mfungaji awe na skills , kufungwa goli kuta taka mfungwaji afanye error. Sasa kuna time error % ina zidi skill % au vice versa, kazi kwako ni kuchambua kipi kili zidi kipi. ukitaka nitafute nikupe kitabu hiki usome.
'44 Secrets for Great Soccer Goal Scoring Skills' kimeandikwa na Mirsad Harsic. Huta pata tatizo la ku mpa credit mfungaji au mfungwaji wa goli.

2. Basti na Schneiderln, sija sema waanze au wacheze dakika zote tisini, kama uliona mchezo wa jana utajua wali hitajika wao kuliko Fellaini. So jana tu mechi ya stoke na Arsenal pia mtu kama Basti ali hitajika.

3. Yeye ndio kocha, yeye ndio kiongozi, hivo lawama ata pewa yeye kuliko wachezaji, ahakikishaje morali ni jambo ambalo hata kocha wa level 1 hufundishwa, kuna kitu kinaitwa sports psychology mkuu ni moja ya foundation course za ukocha. Kwa nini Mou aliondoka Madrid next year Anceloti akaja kubeba UEFA? Kwa nini Mou aliiacha pabaya Chelsea lakini Conte na Hiddink walijitahidi!? Tena wakicheza na vikosi almost hivo hivo alivo viacha Morinho!? Tatizo Siyo teknik tuu, hata suala la saikolojia ya wachezj lina husika.
Kama Mou hajui afanye nini ili morali iongezeke bas ndio ana stahili kufukuzwa.

5. Ukiweka hicho kitu kinacho itwa exceptional treatment bas ukifanye kwa exceptional player ambaye ni kweli some tyme single handedly ana ibeba timu, ila si Ibra na Pogba, they are just equal with other players kwa viwango wanavo onesha sasa, haina haja ya special treatment kwao. Part of being good coach is being fair kwa sasa pale man u ili kuwa fair lazima awa treat wote kama equals. Umesema kila timu lazima kuwa na superstar anaye treatiwa tofauti
Messi kwa Barca Yes
Ozil kwa Arsenl yes
Ronaldo kwa Madrid yes
Man u hatuna hata mmoja wa aina hiyo tunajidanganya hapo. Na Mou ana fanya kosa la kuwaza kama wewe unavo waza.

5. Nakubali kuwa alikiwa majeruhi lakini alisha pona mechi 3 au 4 kabla ya jana, yet alikiwa hapangwi, nakubali kuwa at leat mechi mbili za mwisho kapangwa aendelee hivo hivo.

Wewe huwezi kunielewa kama unaingiza mitazamo yako ya ki personal, mfano mimi i have never seen a fan who think knows man utd in the sense of being arrogant as you! Uwa unajiskia kama wewe ndio shabiki bora hivi, unaijua timu vzuri unaujua utamaduni wa utd vizuri, wakat uko Tandale tu kama sisi wengine. Unajihisi ni shabiki mzuri mpaka unataka wengine tuwe kama wewe. Lakini sija wahi ingiza bias zangu kwenye comments zako, nyingine huwa nzuri tuu na huwa na kubali unapokuwa upo sahihi. Ukitaka kuwa ratianal pungiza kujiona wewe ndio kilanja wa mashabiki wa utd, sikiliza maoni ya kila mtu na usitake kila mtu awe kama wewe, halafu nakushauri soma majarida mbali.mbali ya soka, nenda hata you tube uangalie tekniks mbali mbali we mpira unajua ila kuna ki ji elim flan hivi unakikosa.

Am not bitter, natoa na data zangu, tungekuwa wa Pili kwenye ligi, data zingekiwa vizuri si ajabu ningekuwa namsifia hapa Kocha, lakini hali yetu si nzuri na haitii matumaini so lazima niseme. Na expect hatutaingiza mitazamo binafsi juu yetu ili mazungumzo yetu yawe na maelewano.
 
Tutaongea sana lakini United ina matatizo makubwa mawili. Kwanza Kocha. Pili wachezaji. Tatizo la kocha hajui ni wakati gani mchezaji gani anafaa acheze kwa nafasi ipi na kwa lengo lipi. Kila siku anabadili. Wanaokaa bench unashangaa kwanini hawapati minutes?? Tatizo la wachezaji ni uwezo mfano Zlatan ni mzigo hakuna lolote. Not skillful not fast not possessive. Wachezaji walio wengi uwezo binafsi uko low. With exception to Carrick, De Gea , Hererra na Mata. Wings hazipenetrate na overall ball possession is poor. Fellaini anatakiwa atoke kabisa United. Useless.
 
Less talent una maanisha nini ? Hivi enzi za SAF,Moyes,LVG ulikuwepo hapa JF

Unafahamu kuwa LVG aliwakuta RVP,Rafael,Chicharito na akawauza wote na aliwanunua Bastian,Schneiderlein,Darmian,Blind,Shaw,Herrera,Martial,Depay,Falcao,Di Maria,Romero,Rojo
Mourinho amenunua 4 players (kwa maoni yako talent player) ambao 2 kati yao (Pogba na Ibra) unawaponda
Unajua kwa nini SAF alikuwa kocha bora alikuwa na less talent na aliweza ku utilize.
Talent wise Ibra na pogba, Mikhi na Baily wame add depth kubwa kuliko aiyo kuwa nayo LvG, ambayo ingebidi mou ajue namna ya kuitumia ili ilete matokeo.
Kina RvP walikuwa ndio wako kwenye viwango vibovu kweli kwa wakat wao kipindi cha LvG. So bado LvG alikuwa na less talent heck hakufanya vibaya sana
Jf mi nimeingia mwaka huu huu lakin mpira nimeanza kuangalia kitambo
 
Mkubwa Fella alichokifanya jana amenikumbusha Phil Nevill alipokuwa anakipiga Everton game ngumu km zile matukio km ya yale yalikuwa ya kawaida ndani ya box ya everton na kutupatia Gift inshort Fella jana amewepa offer masela wake wa everton inaweza kuwa makusud au bahati mbaya
 
Unajua kwa nini SAF alikuwa kocha bora alikuwa na less talent na aliweza ku utilize.
Talent wise Ibra na pogba, Mikhi na Baily wame add depth kubwa kuliko aiyo kuwa nayo LvG, ambayo ingebidi mou ajue namna ya kuitumia ili ilete matokeo.
Kina RvP wakikuwa ndio wako kwenye viwango vibovu kweli kwa wakat wao kipindi cha LvG. So bado LvG alikuwa na less talent heck hakufanya vibaya sana
Jf mi nimeingia mwaka huu huu lakin mpira nimeanza kuangalia kitambo
nimependa maelezo yako.mimi huwa kila siku najiuliza kitatokea kitu gani kama kocha atamtumia mata pamoja na mkhityaran kwa pamoja.
 
Back
Top Bottom