Mamlaka ya usimamizi wa wanyama pori Tanzania (TAWA) yasema taratibu zote za kisheria zilifuatwa kwa mamba aliyewindwa na kuuawa ziwa Rukwa

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA) imesema imekamilisha uchunguzi uliokuwa unafanywa ili kuona kama kuna ukiukwaji wa sheria za uwindaji baada ya kuonekana kwa video ya Mwindaji wa Marekani Josh Bowmer akifurahia kuwinda mamba mkubwa chini Tanzania na kuleta taharuki, ambapo uchunguzi umeonesha mamba huyo aliwindwa kitalu cha Lake Rukwa GR kwa kibali halali, ada na tozo zote za uwindaji zililipwa na hakuna utaratibu uliokiukwa.

Taarifa iliyotolewa leo January 02,2024 na TAWA imesema "Kwa mujibu wa taratibu za mkataba wa kimataifa wa CITES, Tanzania imeruhusiwa kuwinda mamba wasiozidi 1,600 kwa mwaka, mpaka sasa mamba 39 tu kati ya 1,600 wamewindwa kutoka kwenye mgawo (quota) wa Taifa wa mwaka 2023, mamba anayeonekana kwenye picha jongefu (video clip) iliyosambaa aliwindwa katika kitalu cha Lake Rukwa GR kwa kibali halali namba MP-0001792 kilichoanza tarehe 12/08/2023 hadi 09/09/2023"

"Mamba huyo alikuwa na urefu wa futi 16.2 sawa na sentimita 493.8 ikiwa ni juu ya kiwango cha chini cha urefu wa sentimita 300 unaohitajika kwa mujibu wa sheria, aidha kwa mujibu wa takwimu za taasisi ya Marekani (Safari Club International- SCI), mamba mrefu zaidi duniani aliwindwa chini Ethiopia mwaka 2005 (futi 18.7 sawa na sentimita 561)"

"Vilevile, kumbukumbu zinaonesha, uwindaji huu ulisimamiwa na Askari kutoka TAWA na Mwindaji bingwa kutoka kwenye kampuni iliyopewa kibali kwa mujibu wa sheria, ada na tozo zote zinazohusiana na uwindaji wa mamba zililipwa kwa kuzingatia sheria na kanuni zinazosimamia uwindaji hapa nchini, hivyo taratibu zote hizi za kisheria zilizingatiwa na hakuna utaratibu uliokiukwa.

"TAWA inawahakikishia Wananchi kuwa uwindaji wa wanyamapori chini unazingatia Sheria na taratibu za ndani ya Nchi na zile za kimataifa na Mamlaka inawatoa hofu kuwa taratibu hizi zinasimamiwa ipasavyo na pale panapotokea ukiukwaii hatua stahiki huchukuliwa kwa mujibu wa sheria" -ameeleza Afisa Habari wa TAWA, Beatus Maganja.

Pia soma: TAWA: Bado tunachunguza tukio la Muwindaji kuua Mamba
 
Ndugu zangu Watanzania,

Mamlaka ya usimamizi wa wanyama pori Tanzania (TAWA) imesema mamba aliyewindwa na kuuwawa huko ziwa Rukwa aliwindwa kihalali na kampuni yenye vibali vyote halali pasipo ukiukwaji wa sheria ya aina yoyote ile.kwa hiyo TAWA wamesema Watanzania tuendelee kuwa watulivu na tusiwe na wasiwasi wowote ule maana TAWA wapo makini sana kuhakikisha kuwa sheria zinafuatwa na kuzingatiwa.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Nyie mnafikiria wale wawindaji wanawinda kiholela?
Kama hamtaki mambo haya iambieni
Serikali yenu wazuie trophy hunting

Ova
 
Sasa mlikua mnapiga kelele za nini mpaka sasa kuna mamba 1561 wanatakiwa kuwindwa. Wabongo bana
Idadi siyo hoja Bali ukubwa wa mamba na hao wawindaji walikuwa hata kwao Marekani wamepigwa marufuku .

Si umeona hiyo taarifa inaonesha eti wao siyo waliomwinda huyo Mamba bali aliwindwa na Askari wa TAWA na mwindaji bingwa toka kampuni iliyowaleta.

Umeelewa ni kwa nini TAWA inakwepa isionekane kina Josh na Sarah Bowmar ndiyo waliomwinda yule mamba??
 
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA) imesema imekamilisha uchunguzi uliokuwa unafanywa ili kuona kama kuna ukiukwaji wa sheria za uwindaji baada ya kuonekana kwa video ya Mwindaji wa Marekani Josh Bowmer akifurahia kuwinda mamba mkubwa chini Tanzania na kuleta taharuki, ambapo uchunguzi umeonesha mamba huyo aliwindwa kitalu cha Lake Rukwa GR kwa kibali halali, ada na tozo zote za uwindaji zililipwa na hakuna utaratibu uliokiukwa.

Taarifa iliyotolewa leo January 02,2024 na TAWA imesema "Kwa mujibu wa taratibu za mkataba wa kimataifa wa CITES, Tanzania imeruhusiwa kuwinda mamba wasiozidi 1,600 kwa mwaka, mpaka sasa mamba 39 tu kati ya 1,600 wamewindwa kutoka kwenye mgawo (quota) wa Taifa wa mwaka 2023, mamba anayeonekana kwenye picha jongefu (video clip) iliyosambaa aliwindwa katika kitalu cha Lake Rukwa GR kwa kibali halali namba MP-0001792 kilichoanza tarehe 12/08/2023 hadi 09/09/2023"

"Mamba huyo alikuwa na urefu wa futi 16.2 sawa na sentimita 493.8 ikiwa ni juu ya kiwango cha chini cha urefu wa sentimita 300 unaohitajika kwa mujibu wa sheria, aidha kwa mujibu wa takwimu za taasisi ya Marekani (Safari Club International- SCI), mamba mrefu zaidi duniani aliwindwa chini Ethiopia mwaka 2005 (futi 18.7 sawa na sentimita 561)"

"Vilevile, kumbukumbu zinaonesha, uwindaji huu ulisimamiwa na Askari kutoka TAWA na Mwindaji bingwa kutoka kwenye kampuni iliyopewa kibali kwa mujibu wa sheria, ada na tozo zote zinazohusiana na uwindaji wa mamba zililipwa kwa kuzingatia sheria na kanuni zinazosimamia uwindaji hapa nchini, hivyo taratibu zote hizi za kisheria zilizingatiwa na hakuna utaratibu uliokiukwa.

"TAWA inawahakikishia Wananchi kuwa uwindaji wa wanyamapori chini unazingatia Sheria na taratibu za ndani ya Nchi na zile za kimataifa na Mamlaka inawatoa hofu kuwa taratibu hizi zinasimamiwa ipasavyo na pale panapotokea ukiukwaii hatua stahiki huchukuliwa kwa mujibu wa sheria" -ameeleza Afisa Habari wa TAWA, Beatus Maganja.

Pia soma: TAWA: Bado tunachunguza tukio la Muwindaji kuua Mamba
Kitu kilichokuwa kinalalamikiwa ni kwanini Mamba mkubwa kuliko wote duniani auawe ??!!
Hawaoni hapo sisi ndio tuliofeli ??!
Suala sio Mamba bali Mamba mkubwa kuliko Mamba wote Duniani !!
 
Back
Top Bottom