TAWA: Bado tunachunguza tukio la Muwindaji kuua Mamba

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA) imesema inaendelea na uchunguzi kuona kama kuna ukiukwaji wa Sheria za uwindaji baada ya kuonekana kwa video ya Mwindaji wa Marekani Josh Bowmer akifurahia kuwinda mamba mkubwa nchini Tanzania mwenye rekodi ya dunia na kuleta taharuki.

Taarifa ya TAWA imesema mara baada ya uchunguzi kukamilika taarifa kamili itatolewa na hatua za kisheria zitachukuliwa iwapo ukiukwaji utabainika.

“TAWA inapenda kufahamisha Umma kuwa uwindaji wa kitali hufanyika kwa kuzingatia sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori sura ya 283 pamoja na kanuni za uwindaji wa kitalii za mwaka 2015 na marekebisho yake ya mwaka 2017, 2019 na 2020, uwindaji wa kitalii pia husimamiwa na Mkataba wa Kimataifa wa Biashara ya Wanyamapori na Mimea iliyohatarini kutoweka (Convention on International Trade In Endangered Species of Wild Fauna and Flora - CITES) ambao Nchi yetu imeridhia.

“Mamba ni miongoni mwa wanyamapori wanaolindwa na mkataba huu na wamewekwa katika kundi la pili (Appendix II) ambalo linaruhusu matumizi ya uvunaji ikiwemo windaji wa kitalii, masharti ya uwindaji wa mamba kwa muibu wa Kanuni na Mkataba wa CITES ni kuhakikisha mamba wote wanaowindwa chini hawazidi 1,600 kwa mwaka, mamba anavewindwa ana urefu usiopungua sentimita 300, vibandiko maalum (Skin tags) vinafungwa katika ngozi za mamba wanaowindwana (iv) Vibali vya CITES (CITES export permit) vinatumika kusafirisha nyara zitokanazo na mamba waliowindwa” imeeleza taarifa ya TAWA.

“Chini ya Sheria na Mkataba huo, Mtu yeyote anaruhusiwa kufanya uwindaji wa kitalii baada ya kupata kibali kutoka TAWA na kutimiza masharti kama ilivyobainishwa hapo juu, TAWA inawajibu wa kusimamia uwindaji huo katika hatua zake zote, kumbukumbu tulizonazo zinaonyesha kuwepo kwa vibali vya uwindaji wa wanyamapori ikiwemo mamba katika maeneo mbalimbali nchini”

IMG_20231228_183806_602.jpg


Pia soma: TAWA: Mamba aliwindwa kihalali kwa kufuata sheria, tozo zililipwa
 
Shida inaanzia hapo wanaposema.."mamba mkubwa mwenye rekodi Tanzania na Duniani....kama ana hizo record kwa nini auwawe...kwani asiengabaki akaendelea kuwa kivutio cha utalii n.k.

Kelele nyingi meaning kuna kitu hakiko sawa..wawindaji hawa wako miaka mingi..why watu wapige kelele kwa huyu?

Isijekuwa watu wamedhulumiana facilitation fees huko wakaona walipuane..
 
Shida inaanzia hapo wanaposema.."mamba mkubwa mwenye rekodi Tanzania na Duniani....kama ana hizo record kwa nini auwawe...kwani asiengabaki akaendelea kuwa kivutio cha utalii n.k
Kelele nyingi meaning kuna kitu hakiko sawa..wawindaji hawa wako miaka mingi..why watu wapige kelele kwa huyu??Isijekuwa watu wamedhulumiana facilitation fees huko wakaona walipuane..
Hakuna kesi hapo, uchaguzi oyee.
 
Sheria za Maliasili zinatoa kibali kuwinda mamba mwenye kimo cha zaidi ya mita 3, so kama amezidi hapo mzungu hana kosa na kama ana kibali cha uwindaji na usafirishaji wa nyara kimataifa CITES ambacho kinahusisha viumbe walio hatarini kupotea (Convention on International Trade in Endangered species of Wild Fauna and Floral
 
Wanaendelea kuchunguza wakati wamemfunga yule mama wa Iringa aliekua na nyama kilo saba za swala miaka 22 huku wageni mkiwagawia na kuwaambia wapige nazo picha inakera sana hii Nchi ina laana sio bure...
 
Shida inaanzia hapo wanaposema.."mamba mkubwa mwenye rekodi Tanzania na Duniani....kama ana hizo record kwa nini auwawe...kwani asiengabaki akaendelea kuwa kivutio cha utalii n.k
Kelele nyingi meaning kuna kitu hakiko sawa..wawindaji hawa wako miaka mingi..why watu wapige kelele kwa huyu??Isijekuwa watu wamedhulumiana facilitation fees huko wakaona walipuane..

Wewe umewahi kwenda kuangalia utalii wa mamba?

Kabla ya Hilo tukio ulikua unamjua huyo mamba?

Hunting is legal in TZ na jamaa wamefanya kila kitu within the legal scope hakuna sheria imevunjwa.
 
Ili kuficha aibu na kulindana hiyo ripoti haitokaa itoke na ikitoka lazima itafukia mashimo.

Upuuzi wa siku zote.

Ripoti inatoka inasema kila kitu kilifanyika legally. Hakuna kosa Hapo.

Kama hamtaki uwindaji badilisheni sheria going forward.
 
Wewe umewahi kwenda kuangalia utalii wa mamba?

Kabla ya Hilo tukio ulikua unamjua huyo mamba?

Hunting is legal in TZ na jamaa wamefanya kila kitu within the legal scope hakuna sheria imevunjwa.



Hiyo sheria inamapungufu inabidi ibadilishwe.

Kwanini wawinde na kuwaua au kuwachukua?

Kwanini wasiishie kutalii na kuangalia tu kila mtu ajae?

Wa kuisha je itakuwaje?
 
Hawa Tawa ndo wanatoa vibali, wanafuatilia Nini katika huu ulimwengu wa digitali ni mwendo wa ku click na details zote kushuka, hapo inamana wamefanya uwindaji haramu usio na kibali, waseme ukweli sio suala la kutafutana
 
Hiyo sheria inamapungufu inabidi ibadilishwe.

Kwanini wawinde na kuwaua au kuwachukua?

Kwanini wasiishie kutalii na kuangalia tu kila mtu ajae?

Wa kuisha je itakuwaje?

Uwindaji una faida zake na upo kisheria, hao mamba wakizidi pia ni hatari kwenye ecosystem. Serikali inaweza lazimika kuwaua na isipate kitu.

Kuna vijiji wanaomba Simba wauwawe maana wanahatarisha maisha yao.
 
KUNA SIKU TUTAKUJA KUWA
TUME YA KUFUATILIA CHUNGUZI ZOTE ZISIZOKUWA NA MAJIBU
 
Naenda moja kwa moja kwenye point.

Hata mimi nisiye na uelewa kwenye mambo haya ya uwindaji sijui na vibali vya uwindaji naamini kabisa katika hili tumepigwa kabisaaa either na huyu Mzungu au hawa TAWA"

Kama kweli huyu ndio mamba mkubwa kuliko wote Tanzania na anarekodi zake, basi kuna kitu hakiko sawa mahala huko TAWA.

Anywai ngoja tusubiri tu tuone.....! RIP Magufuli
 
Back
Top Bottom