Kama ni suala la picha za mama Abdul na lile jambazi Kwa Nini hazikuthibitiwa na mamlaka za Rais zisitoke? Umma ulizipataje? Kama ambavyo watu/platform zingine zilivyozipata hizo picha na hili jukwaa limezipata Kwa style hiyo hiyo, Kwa Nini watu wafungiwe kutoa maoni ndani ya nchi yao, kuburudika na kupata elimu kwa pamoja? Mamlaka ya TCRA inapaswa kujitafakari au la ni mashinikizo kutoka kwa watu ambao hawalitakii mema taifa hili Bali wanajali interest zao binafsi. I have confidence serikali na vyombo vyake vimekuwa vikipata taarifa mhimu kupitia jukwaa hili ktk kuleta ustawi wa Jamie ya kitanzania, hivyo ni rai yetu TCRA wafikirie upya uamuzi batili huu wa kusitisha jukwaa hili mhimu kwa watanzania hasa ktk kipindi hiki cha uchaguzi.