PostGE2025 TCRA yatoa onyo kwa vyombo vya habari kusambaza maudhui yanayoweza kuhatarisha amani kutoka kwa watu wenye kesi za uhaini

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,176
Reaction score
4,918
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inapenda kuutaarifu umma na kuvikumbusha vyombo vyote vya habari nchini, ikiwemo televisheni, redio, machapisho, mitandao ya kijamii, tovuti na majukwaa ya kidijitali, juu ya wajibu wao wa kufuata sheria na kanuni za mawasiliano katika kutoa habari kwa umma.

Soma TCRA yakanusha kutoa onyo kwa vyombo vya habari kusambaza maudhui kutoka kwa watu wenye kesi za uhaini

TCRA imebaini mwenendo wa baadhi ya watoa huduma za habari kurusha au kusambaza maudhui kutoka kwa watu wenye kesi zinazoendelea mahakamani, ikijumuisha kesi za tuhuma za uhaini, maudhui ambayo kwa namna tofauti yanaweza:
  • Kuhamasisha au kuchochea uvunjifu wa amani,
  • Kuathiri mchakato wa haki mahakamani,
  • Kusababisha upotoshaji na taharuki kwa jamii,
  • Kuhatarisha usalama na utulivu wa taifa.
Kwa mujibu wa Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) na kanuni zake, hairuhusiwi kusambaza au kutangaza maudhui yanayoweza kusababisha uvunjifu wa amani, uchochezi wa tafrani, au yanayoweza kudhoofisha masuala ya usalama wa taifa.

Maelekezo kwa vyombo vya habari:
  1. Msitoe, msirushe, wala kusambaza maudhui kutoka kwa watu wenye kesi zinazoendelea mahakamani bila kufuata taratibu zinazokubalika kisheria.
  2. Hakikisheni uhariri wa kina kabla ya kuchapisha au kutangaza taarifa zinazoweza kuathiri amani na usalama wa nchi.
  3. Epukeni kurusha maudhui yenye lugha ya uchochezi, upotoshaji au yanayoweza kujenga hofu na mgawanyiko katika jamii.
TCRA inatoa wito kwa wananchi wote kutumia majukwaa ya mtandaoni kwa njia ya kujenga, yenye busara, na inayolinda maslahi ya taifa. Aidha, tunahimiza watumiaji wote kuripoti akaunti au maudhui. hatarishi kupitia mifumo ya taarifa ya TCRA au mamlaka za usalama.

Mamlaka itaendelea kufuatilia kwa karibu mawasiliano yote ya kielektroniki ili kuhakikisha kuwa mtandao unatumika kwa manufaa ya jamii na nchi kwa ujumla.
1763555023671.png
 
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa onyo kali kwa vyombo vya habari, majukwaa ya mitandaoni na watumiaji wa huduma za mawasiliano nchini kuhusu kusambaza maudhui yanayohusiana na watu wenye kesi za uhaini zinazondelea mahakamani.

Katika taarifa hiyo, TCRA imesema imebaini baadhi ya vyombo na watoa huduma wamekuwa wakirusha maudhui yanayoweza:

  • Kuhamasisha au kuchochea uvunjifu wa amani,
  • Kuathiri mchakato wa haki mahakamani,
  • Kusababisha taharuki na upotoshaji kwa jamii,
  • Kuhatarisha usalama wa taifa.

TCRA imekumbusha vyombo vya habari kutosambaza maudhui ya kesi zinazoendelea bila kufuata taratibu za kisheria. Pia imewataka kuhakikisha uhalisia wa taarifa kabla ya kuziandika na kuepuka lugha ya uchochezi au inayoweza kuathiri amani na utulivu.

Aidha, mamlaka hiyo imewataka wananchi kuwa makini na taarifa wanazosoma na kutoa wito wa kuripoti akaunti au maudhui hatarishi kwa TCRA au mamlaka za usalama.

Taarifa hiyo imetolewa tarehe 19 Novemba 2025 na kusainiwa na Dkt. Jabiri K. Bakari, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA.
1763555052607.png
 
View attachment 3504329
Unapoamua kutumia tumbo kufikiri badala ya kichwa
 
Dah, so taarifa ikitoka kwa watu wasio na kesi za uhaini, unaruhusiwa kushare?

Nguvu kubwa inatumika kufunika taarifa muhimu zinazohusu maisha ya watu, hii ni aibu kwa taifa.
 
Hawa jamaa ni Bora tu wafungie radio station na TV zote nationwide na wabakize TV Moja ambayo wata operates wao ili Ku comply na Izo directives zao

Yani zama za habari ni kama tupo zama z Mawe vile
 
Na nyie muache kututumia ma msg yenu kwenye simu mnatumalizia chaji Pia ni usumbufu ki katiba yenu uchwara!
 
Hawa jamaa ni Bora tu wafungie radio station na TV zote nationwide na wabakize TV Moja ambayo wata operates wao ili Ku comply na Izo directives zao

Yani zama za habari ni kama tupo zama z Mawe vile
Nashangaa media zinafanyaje kazi kwenye mazingira haya, wangekuwa na umoja wote wanazima mitambo ibakie TBC tu, huku wakidai mabadiliko ya sheria za habari.
 
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa onyo kali kwa vyombo vya habari, majukwaa ya mitandaoni na watumiaji wa huduma za mawasiliano nchini kuhusu kusambaza maudhui yanayohusiana na watu wenye kesi za uhaini zinazondelea mahakamani.

Katika taarifa hiyo, TCRA imesema imebaini baadhi ya vyombo na watoa huduma wamekuwa wakirusha maudhui yanayoweza:

  • Kuhamasisha au kuchochea uvunjifu wa amani,
  • Kuathiri mchakato wa haki mahakamani,
  • Kusababisha taharuki na upotoshaji kwa jamii,
  • Kuhatarisha usalama wa taifa.

TCRA imekumbusha vyombo vya habari kutosambaza maudhui ya kesi zinazoendelea bila kufuata taratibu za kisheria. Pia imewataka kuhakikisha uhalisia wa taarifa kabla ya kuziandika na kuepuka lugha ya uchochezi au inayoweza kuathiri amani na utulivu.

Aidha, mamlaka hiyo imewataka wananchi kuwa makini na taarifa wanazosoma na kutoa wito wa kuripoti akaunti au maudhui hatarishi kwa TCRA au mamlaka za usalama.

Taarifa hiyo imetolewa tarehe 19 Novemba 2025 na kusainiwa na Dkt. Jabiri K. Bakari, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA.
hakuna kazi za kufanya huko tcra?
 
wanazidi kupigwa pini, baada ya habari kusambaa

Hizi taasisi nazo zinahitaji reforms
Ile sheria ya vyombo vya habari ni mbaya sana. Wapinzani waliilalamikia sana lkn hakuna aliyewasikia. Ndio maana hakuna hata TV moja wala gazeti linalothubutu kuandika chochote dhidi ya hujuma za uchaguzi zilizofanyika. Hili onyo linalenga kuwafumba midomo wahariri wasiandike habari kwa u dani dhidi ya yanayoendelea nchini
 
Naam, vyombo vya habari kwa umoja wao wasipogoma na kuoinga hili. Soo media zitakuwa zimekufa
Na ajira zao matatani
 
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inapenda kuutaarifu umma na kuvikumbusha vyombo vyote vya habari nchini, ikiwemo televisheni, redio, machapisho, mitandao ya kijamii, tovuti na majukwaa ya kidijitali, juu ya wajibu wao wa kufuata sheria na kanuni za mawasiliano katika kutoa habari kwa umma.

TCRA imebaini mwenendo wa baadhi ya watoa huduma za habari kurusha au kusambaza maudhui kutoka kwa watu wenye kesi zinazoendelea mahakamani, ikijumuisha kesi za tuhuma za uhaini, maudhui ambayo kwa namna tofauti yanaweza:
  • Kuhamasisha au kuchochea uvunjifu wa amani,
  • Kuathiri mchakato wa haki mahakamani,
  • Kusababisha upotoshaji na taharuki kwa jamii,
  • Kuhatarisha usalama na utulivu wa taifa.
Kwa mujibu wa Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) na kanuni zake, hairuhusiwi kusambaza au kutangaza maudhui yanayoweza kusababisha uvunjifu wa amani, uchochezi wa tafrani, au yanayoweza kudhoofisha masuala ya usalama wa taifa.

Maelekezo kwa vyombo vya habari:
  1. Msitoe, msirushe, wala kusambaza maudhui kutoka kwa watu wenye kesi zinazoendelea mahakamani bila kufuata taratibu zinazokubalika kisheria.
  2. Hakikisheni uhariri wa kina kabla ya kuchapisha au kutangaza taarifa zinazoweza kuathiri amani na usalama wa nchi.
  3. Epukeni kurusha maudhui yenye lugha ya uchochezi, upotoshaji au yanayoweza kujenga hofu na mgawanyiko katika jamii.
TCRA inatoa wito kwa wananchi wote kutumia majukwaa ya mtandaoni kwa njia ya kujenga, yenye busara, na inayolinda maslahi ya taifa. Aidha, tunahimiza watumiaji wote kuripoti akaunti au maudhui. hatarishi kupitia mifumo ya taarifa ya TCRA au mamlaka za usalama.

Mamlaka itaendelea kufuatilia kwa karibu mawasiliano yote ya kielektroniki ili kuhakikisha kuwa mtandao unatumika kwa manufaa ya jamii na nchi kwa ujumla.
View attachment 3504329
Ila yale ya mashehe ubwabwa aaah, hadi TBC wanayarusha
 
Back
Top Bottom