Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) yatangaza kuifungia JamiiForums

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) yatangaza kuifungia JamiiForums

JamiiForums

JF Official Account
Joined
Nov 9, 2006
Posts
6,240
Reaction score
5,658
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesitisha Leseni ya Maudhui Mtandaoni ya JamiiForums kwa muda wa siku 90 na kuzuia upatikanaji wa jukwaa hilo, kwa maelezo ya kukiuka Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta kuhusu maudhui mtandaoni

TCRA imesema uamuzi huu umetokana na JamiiForums kuchapisha taarifa ya Mwanasiasa Humphrey Polepole kuhusu Rostam kumiliki mgodi wa makaa ya mawe kwa asilimia 70 na taarifa za uhusiano kati ya Rais wa Tanzania na "Mfanyabiashara" Wicknell Chivayo bila kuzingatia mizania.

Kwa mujibu wa TCRA, JamiiForums ilishindwa kutafuta maoni ya Mamlaka husika/Msemaji wa Rais/Serikali, kuthibitisha uhalisia wa picha (za Rais na Chivayo) zilizotumika, na hivyo kuuaminisha Umma taarifa za upande mmoja.

Aidha, TCRA imeeleza kuwa jukwaa la JamiiForums halikudhibiti maudhui yenye lugha ya matusi, kashfa na kejeli dhidi ya Rais wa Tanzania, na kuendelea kuhifadhi maudhui hayo ambayo bado yanapatikana kwa umma.

TCRA imeongeza kuwa maudhui hayo yanakinzana na mila, desturi na utamaduni wa Kitanzania, hivyo kuhatarisha mshikamano wa kitaifa, amani na taswira ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Makaa ya Mawe.png

Chivayo.png

Screenshot 2025-09-06 at 13.50.05.png
 
Nadhani ni zile picha za mama Abdul akikumbatiana na yule raia fisadi wa Zimbabwe,nilijua hapa lazima kiumane,

Hatuna amani tena
Hii ni Moja ya picha alizopiga Mama Abdul na Wicknell Chivayo,fisadi mkuu huko Zimbabwe
 

Attachments

  • Screenshot_20250906-190540.jpg
    Screenshot_20250906-190540.jpg
    287.7 KB · Views: 28
Back
Top Bottom