Mamlaka haziwaoni mateja kituo cha daladala Kawe? ni aibu kubwa sana

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Inatisha sana ukipita asubuhi eneo la Kawe Stand na kukuta makundi ya vijana wakivuta bangi na kujidunga sindano za dawa za kulevya huku wakisindikiza na pombe na energy.

Inashangaza sana kwasababu kituo cha Polisi Kawe hakipo mbali na eneo lile, ni kama mita 250 hivi lakini vijana wale wanatumia dawa za kulevya bila kujificha.

Usiku hujibanza kwenye mabanda ya mama lishe na mabanda mengine yaliyo eneo hilo, kukikucha wakati hayo mabanda yakitumika kwa kazi za uzalishaji basi vijana wale husambaa mpaka kwenye uzio wa mabati ambako kuna mradi wa ujenzi wa nyumba za NHC na kutumia hizo dawa, japokuwa hawana shida na mtu lakini si salama maana vijana wetu hupita pale na kuwakuta hivyo inaweza kupelekea nao kutamani kugeza tabia hizo.

Nashauri tu mamlaka ziweze kuingilia kati suala hili ili kuokoa hicho kizazi kinachopotea.

1k.jpg
2k.jpg
 
Ni kweli kabisa, nipo Kawe, nayaona. Nilishangaa kumuona binti aliyemaliza form 4 anavuta bangi na madawa, tena mwendo wa kupepesuka.
 
Inatisha sana ukipita asubuhi eneo la Kawe Stand na kukuta makundi ya vijana wakivuta bangi na kujidunga sindano za dawa za kulevya huku wakisindikiza na pombe na energy.

Inashangaza sana kwasababu kituo cha Polisi Kawe hakipo mbali na eneo lile, ni kama mita 250 hivi lakini vijana wale wanatumia dawa za kulevya bila kujificha.

Usiku hujibanza kwenye mabanda ya mama lishe na mabanda mengine yaliyo eneo hilo, kukikucha wakati hayo mabanda yakitumika kwa kazi za uzalishaji basi vijana wale husambaa mpaka kwenye uzio wa mabati ambako kuna mradi wa ujenzi wa nyumba za NHC na kutumia hizo dawa, japokuwa hawana shida na mtu lakini si salama maana vijana wetu hupita pale na kuwakuta hivyo inaweza kupelekea nao kutamani kugeza tabia hizo.

Nashauri tu mamlaka ziweze kuingilia kati suala hili ili kuokoa hicho kizazi kinachopotea.
Unataka GENTAMYCINE akamatwe
 
tuanze utafiti wa brains za polisi au tuwekeze nguvu ktk kujenga jamii iliyo na maadili???
Vyote vinatakiwa kwenda sambamba.
Polisi ndo msaada mkubwa kwa wahuni walioshindikana kwenye jamii.

Hata huku kwetu vibaka wamezidi hadi wanaua, na wanaonekana wazi kijiwe chao...ukipita usiku unawaona wanatumia mirungi na bangi hadharani halafu kituo cha polisi kipo hapa hapa mtaani.

Hawa polisi kazi yao haswa ni nini kama wanashindwa kudhibidi uhalifu unaoonekana wazi wazi?
 
Mamlaka zinawaona wanaowapiga spana tu kuhusu DP world mengine yanajisumbukia yenyewe huko.
 
Back
Top Bottom