BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 422
- 1,049
Kuna tabia ambayo imekuwepo kwa muda, awali ilianza kama kitu kidogo kwa kufanywa na watu wachache lakini sasa hivi inazidi kuwa kama ndivyo uhalisia.
Daladala za kutoka Kawe kwenda Buza (Dar es Salaam) hasa nyakati za jioni zimekuwa na kawaida ya kutokamilisha ‘ruti’, zinaishia Buguruni kisha baada ya hapo zinageuza kurejea Kawe au zinasogea hadi cha Chama kilichopo maeneo hayo na kuanza kubeba abiria upya kuelekea Buza au maeneo mengine.
Hiki wanachokifanya si sawa kwa kuwa kinatuumiza sisi Wananchi hasa wa hali ya chini ambao maisha yetu yanategemea usafiri wa Daladala.
Maumivu zaidi ni kuwa hivi karibuni Serikali ilitangaza kuongeza bei ya nauli, so nauli zimeongezwa kisha daladala zinaamua kutoza mara mbili nauli, hapo maumivu yake ni makali zaidi ya noma.
Mamlaka za usafiri wa ardhini ziangalie hili suala, tunaumia kwa sana.
Hili ni moja ya Daladala ambayo ilikatisha ruti nami nikiwa ndani ya basi hilo nikalazimika kuanza kutafuta usafiri mwingine.