Kituo cha daladala Kawe. Fupa lililomshinda Askofu Gwajima

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566
Ndugu zangu,

Hali ya vituo vingi vya daladala nchini hasa wakati wa mvua bado ni mbaya sana. Lakini kama mjuavyo Mwamba ngoma huvutia kwake wacha leo niwaoneshe hali ya kituo cha mtaa wetu hapa Kawe.

Miongoni mwa sehemu zilizolalamikiwa sana ni hali mbaya ya kituo cha Kawe. Mvua ikinyesha kituo kinakuwa kama shamba la mpunga au jalala. Wahusika wamekuwa wakifanya ujanja kwa kumwaga vifusi visivyotatua tatizo hata chembe.

Mbaya zaidi kituo cha Kawe kina Wajasiriamali wengi wanaouza chakula jambo linalohatarisha afya la watu wanaokula vyakula vya eneo hilo.

Kwa idadi ya malalamiko yaliyowasilishwa na wadau katika mitandao mbalimbali ni wazi kituo hiki kimekuwa fupa gumu sana kwa Askofu Gwajima. Ninapata confidence kusema cheo hiki kimakuwa kikubwa sana kwa Mbunge wetu huyu.

Tazama Video hizi hapa chini ujionee mwenyewe:

1706194049062.jpeg


Kawe 3.jpg



 
Back
Top Bottom