Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,194
- 4,115
Kituo cha daladala Kawe ni kero kubwa sana kwa watumiaji wa kituo hicho, Kituo hakina ukarabati wowote, iwe masika na kiangazi, hakuna nafuu, ikiwa kiangazi kituo kinapambwa kwa mashimo na mabonde hali inayoathiri magari na abiria pale wanapofika kituoni.
Kwa masika kama kipindi hiki ndio balaa zoto kabisa, kituo kinapambwa na madimbwi ya maji na matope maziito yalijazana kwenye yale mashimo yaliotengenezeka wakati wa kiangazi, matope yameoza yanatoa harufu kali, hakuna sehemu ya abiria kushuka wala kupanda, wanalazimika kupita kwenye tope kama kambale.
Mnaohusika na ukarabati wa kituo cha daladala Kawe mmelala usingizi wa pono wala hamna habari, huwa naona mnakusanya ushuru sijui hizo pesa mnapeleka wapi kama hata ukarabati haufanyiki, basi kama mmeshindwa kukarabati mngepanda mpunga maana tope lile mngevuna magunia ya mpunga wa kutosha mkapata faida si mmeamua stendi iwe majaruba ya mpunga bwana.
Mbaya zaidi Kawe ilipata mbunge aliyejinasibu kwa kuwapeleka wana Kawe Marekani na kuleta Treni ya umeme cha ajabu Stendi tu ya Kawe imemshinda kuisemea ikafanyiwa ukarabati au kwa kuwa yeye haitumii ivyo sio kipaumbele kwake?