Mambo ya Nyakati: Mbatia, Prof Lipumba, Maalim Seif na Mrema watarejea CCM kabla ya Uchaguzi Mkuu. CHADEMA itabaki kwa mzee Mtei

Huko kujioambanua kwa cdm ni kwa jasho na akili nyingi
Ila wataonja kifungo kwanza ndipo wakubalike wapinzani wa kweli au kukosa ruzuku kabisa kwa miaka 10 wakifaulu hayo watabakia milele na kuongoza serikali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vyama ni mali ya wanachama,hata viongozi wa vyama wakinunuliwa viongozi wengine kutoka miongoni mwawanachama wataibuka, na mwendelezo wa kuisotesha CCM utaendelea vilevile.

Makaburu wa africa ya kusini waliamini kuwa kuwaua viongozi waliokuwa wanawapigania watu weusi kutawaletea unafuu,lakini ndio kwanza wakimuua mmoja wanazaliwa watetezi 100 na msoto kwa makaburu unakuwa mkubwa zaidi nafuu uliopita.mwisho wake makaburu wamewekwa benchi kama mbwa wanaosubiri huruma ya kurushiwa mfupa wakati walikuwa wanakula minofu.
 
Ukizisoma vizuri hizi nyakati utagundua hakuna fursa tena ya Upinzani mamboleo ule unaotegemea " hisani" ya ruzuku ili chama na viongozi wake waweze kuishi.

Unaweza kujiuliza kwanini maalimu Seif alialikwa Ikulu na yeye siyo kiongozi wa ACT wazalendo?

Halafu iangalie vizuri historia ya Prof Lipumba na James Mbatia katika siasa za Tanzania. Kisha jikumbushe namna Nccr mageuzi na Cuf zilivyoasisiwa na namna mzee Mapalala rip alivyokimbizwa chamani na maalimu Seif.

Yuko wapi mzee Marando wa Nccr mageuzi aliyehamia Chadema? Je baada ya bunge kuvunjwa Joseph Selasini atabakia Chadema?...... Prof Baregu je? na Prof Safari?

Kwa kifupi ni kwamba robo karne ya Upinzani mamboleo imefikia tamati, Chadema itabaki na mzee Mtei lakini Lyatonga Mrema, mzee Cheyo, mzee Shibuda wote hawa watarejea CCM where they belong.

Kisha vipimo vitamwelekea Zitto Kabwe wa ACT wazalendo kama ni mpinzani wa kizazi kipya au ndio walewale. Ikumbukwe wakati upinzani unaasisiwa Zitto alikuwa bado ni mtoto kwa mujibu wa sheria za nchi.

Nawatakia Kwaresma yenye baraka

Maendeleo hayana vyama!

Hivi mzee Mtei alibariki ujio wa Lowassa??
 
Back
Top Bottom