Prof. Lipumba, Joseph Selasini, Mzee Cheyo na Mnyika washiriki Majadiliano Rika miongoni mwa Wadau wa Siasa, Machi 11, 2024

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Mazungumzo ya Wanasiasa wakongwe na Chipukizi yanafanyika UDSM, leo Jumatatu Machi 11, 2024.


Majadiliano Rika (Intergenerational Dialogues) ndani ya vyama vya kisiasa ni muhimu kwa ajili ya kujenga uzoefu na kuongeza maarifa kwaniyanaongeza mwingiliano kati ya vijana, watu wa umri wa kati, na wazee. Majadiliano haya pia yanasaidia kukuza ushiriki wenye ufanisi na uwakilishi wenye maana katika medani ya kisiasa.

Vilevile, Majadiliano haya husaidia katika kujenga uelewa wa pamoja kwa kila kundi na hatimaye kusaidia katika kukabiliana na changamoto ambazo vijana wanakabiliana nazo kuhusiana na ushiriki wao katika michakato ya kisiasa na uchaguzi.

Kuelewa jukumu muhimu la mazungumzo ya kizazi kwa kizazi, TCD inalenga kuwaleta pamoja viongozi wa vyama vya kisiasa wa makundi mbalimbali ya umri katika mchakato wa kisiasa kama njia ya kubadilishana mbinu za uongozi na uzoefu ili kuboresha ushirikiano ndani ya mchakato wa utawala wa kidemokrasia. Inatarajiwa kwamba kupitia majadiliano, vijana watapata habari muhimu kwa ajili ya ushiriki na uwakilishi wao katika michakato ya kisiasa na uchaguzi.

Baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaoshiriki katika mazungumzo haya ni pamoja na Prof. Ibrahim Lipumba, Joseph Selasini na John Cheyo, John Mnyika n.k. Lakini pia, Balozi wa Marekani, Michael Battle, pamoja na balozi wa Uholanzi, Wiebe de Boer, ni miongoni mwa wageni wengine wanaohudhuria mazungumzo haya.

Endelea kufuatilia kupata updates zaidi...

MICHAEL BATTLE, Balozi wa Marekani
Tanzania imefanikiwa kuwa na bahati ya kuwa na viongozi wanaojali maslahi ya Nchi na ndio maana wakaruhusu uwepo wa vyama vingi na kuruhusu ukuaji wa Demokrasia.

Hivi karibuni tulimpoteza Rais Ali Mwinyi, moja kati ya sifa yake kubwa ni kuruhusu soko huria, kubadilisha sera za kiuchumi na mabadiliko ya kiuchumi, japokuwa naye aliendeleza msingi ambao ulishatengenezwa na mtangulizi wake, Mwalimu Julius Nyerere.

Kuna uhusiano mkubwa kati ya Uchumi Hai na Mfumo wa Demokrasia wa Nchi, Tanzania ina bahati ya kuwa na Rais mstaafu ambaye yuko hai, JakaYa Kikwete, ambaye anajulikana kwa kuruhusu mabadiliko yenye fikra ya chanya ambaye pia amewapa fursa vijana, amezungumza nayo na amewapa ushauri wa masuala mbalimbali.

TCD 2.jpg

Balozi wa Marekani, Michael Battle akizungumza katika ufunguzi wa mazungumzo hayo.

Kwa sasa tuna Rais Samia, ametoa fursa ya uhuru wa Demokrasia, sio tu kuruhusu uhai wa Vyama vingi, lakini ameruhusu uhuru wa kujieleza kwa kiwango kikubwa.

Kwa mara ya kwanza (Rais Samia) amefanya Watu wawe huru kuandamana hadi ndani ya Dar es Salaam, watu wengi wamekuwa huru kuelezea hisia zao, sifa hizo siyo tu zinaenda kwa Serikali yake bali hata kwa chama kinachotawala.

Uongozi umeelewa umuhimu wa uhuru wa mabadiliko, itambulike kuwa kila Mtanzania ana haki ya kushiriki katika maendeleo ya Nchi yake.

Tanzania haijalishi unatokea wapi, hii Nchi ni yako na una haki ya kushiriki na kuchangia maendeleo.

TCD 3.jpg

Baadhi ya washiriki wakifuatilia

Kuna siku nilizungumza na kijana mmoja akasema hawa Wanasiasa Wazee au watu wazima wamekuwa wakiingia katika mgogoro na vijana, nikamwambia kila Mwanasiasa mzee unatakiwa kutambua kuwa siku moja naye alikuwa kijana.

Kuna wakati watu wanazeeka na wanasahau kuwa wanazeeka, wanasahau kuwa kuna kizazi kitakuja kinahitaji mabadiliko na mawazo mapya.

Hivyo, ni jukumu letu kupitia mazungumzo kama haya yanaweza kutufanya tukumbushane wajibu wetu na kutambua Tanzania inamilikiwa na Watanzania wenyewe.

PROF. IBRAHIM LIPUMBA, Mwenyekiti - Kituo cha Demokrasia Taznzania (TCD)
Mjadala huu nikuona ni namna gani tunaweza kubadilishana mawazo vijana na watu wazima wa rika mbalimbali ili tuweze kujifunza ili tuweze kuimarisha demokrasia yetu kwenye nchi yetu.

Ukiutazama uchaguzi wa serikali za mitaa ulivyokuwa mwaka 2019 hadi sasa, kama Mkurugenzi alivyozungumza, hatujui kanuni. Je uchaguzi wa mwaka huu utakuwa kama wa 2019? Na tunapowaambia vijana washiriki, je wanakwenda kushiriki katika mazingira gani? Uchguzi wa 2020 ulivyokuwa na mazingira yake, kwamba vyama vya upinzani Tanzania vimefanikiwa kupata vitiviwili tu, kati ya viti 214.

Lipumba.jpg

Prof. Ibrahim Lipumba akiwasilisha hoja

Kuna mabadiliko ya sheria lakini hatujui utekelezaji wake utakuwaje na kwamba mazingira ganitutakuwa nayo katika uchaguzi wa mwaka 2025.

Sasa, sisi tuna uzoefu wa nyuma na tutauzungumza hapa.Mazungumo haya yananipa moyo kuwa tunaweza kuleta mabadiliko kwenye siasa za kidemokrasia

Tanzania inakabiliwa na mambo mawili. Moja ni kushindwa kukuza uchumi ambao ni shairikishi na utakaotokomeza umasikini ambao umekithiri katika nchi yetu. Lakini pili ni kujenga misingi mizuri ya kidemokrasia; demokrasia ya kweli ambapo watu wanashiriki ambao wanachagua viongozi wao ambao watatatua changamoto zao. Haya ni mambo mazito.

Sasa, suala la ushiriki si kushiriki tu kwenye uongozi, balo kushiriki kwa malengo ya kutatua matatizo yanayowakabili wananchi wetu.

JOHN CHEYO, Mwenyekiti chama cha UDP
Kijana unayetaka kuingia kwenye Siasa uwe na nia ya kusaidia Watu, ushiriki katika kutengeneza mtindo wa uchaguzi ambao ni mzuri, kwani bila kufanya hivyo, uchaguzi ni kama mnada, usipokuwa na hela huwezi kupata.

Cheyo Lipumba.jpg

Mzee Cheyo akisalimiana na Prof. Lipumba.

Wakati nawania urais niliona changamoto kubwa hasa ya Wakulima ni kukosa uhuru wa mazao na mashamba yao, CCM iliyokuwepo wakati huo ilikuwa ni mbaya, kulikuwa na uonevu mwingi wa viongozi, ndio maana nikaona utatuzi pekee ni kuwakomboa Wakulima na wapate pesa.

Kama unataka kufilisika katika Maisha yako basi nenda kwenye Siasa ukiamini kwamba utapata pesa. Hakuna pesa, na hao wenye pesa ni wezi.

JOHN MNYIKA, Katibu Mkuu CHADEMA
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika ametoa wito kwa vijana kwa kuwaambia inawezekana kuingia kwenye siasa hata kama hauna fedha bali muhimu ni kuwa na nia na kuwasilisha sera vizuri

Baada ya kufanya harakati za muda mrefu kuanzia ngazi ya shule, vijana wengi waliamini kuingia kwenye siasa ni vigumu kwa kuwa unalazimika kupambana na watu wenye uwezo wa kifedha, nikaona kuna sababu ya kuingia kwenye siasa moja kwa moja kuonesha kwa mifano kuwa inawezekana kugombea na kushinda.

Mnyika.jpeg

John Mnyika akiwasilisha hoja

Nikaingia CHADEMA na kugombea Mwaka 2005 nikiwa bado Mwanafunzi wa UDSM, mpinzani wangu akiwa ni marehemu Charles Keenja ambaye alikuwa ana umri wa miaka 65 na ni Waziri, walioshuhudia waliona ushindani ulivyokuwa mkali.

DOROTH SEMU, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo
Tuliosoma zamani kidogo tulisoma somo la Siasa, hiyo ilitujenga kuamini Vijana wote ni sehemu ya Siasa na kutambua ukifikisha umri wa Miaka 18 ni jukumu lako kwenda kupiga kura, sio kubembelezwa au kushawishiwa.

Semu.jpg

Dorothy Semu
Mfumo wa sasa ni uhuru wa kuchagua, Vijana wa siku hizi wanapenda kubembelezwa, uhuru umezidi na hawataki kutumia uwezo wao wa kuwa sehemu ya uongozi au mabadiliko, wanatakiwa watambue mabadiliko hayatokei tu bila ushiriki wao.

Vijana wengi wanapenda kupata vitu vingi kwa haraka bila kupitia mchakato stahiki, amedai wanakosa muda wa kujifunza mambo na wanataka matokeo ya harakaharaka.

JOSEPH SELASINI, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi
Nawaambia usiingie kwenye siasa kama Bendera inayofuata upepo, kwamba kuna mwingine yupo na wewe ukafuata, jitathmini kwanza, je, ni wito wako?

Siasa ina wito, moja ya kipimo cha Mwanasiasa kama una wito wa kufanya siasa ni wito wa kushughulika na shida za Watu hata kama huna cheo chochote, kama huna mapenzi hayo jitathimini. Siasa imekuwa kama fasheni sikuhizi, vijana wanaona ni kama sehemu ya fursa.

Selasini.jpeg

Joseph Selasini
Unakuta huku kwenye chama kuna Mtu anakuja, hajawahi kuwa Mwanachama lakini anataka kugombea Ubunge, hata Katiba ya chama chenyewe haijui, ukifanya hivyo utafeli.
 
Mazungumzo ya Wanasiasa wakongwe na Chipukizi yanafanyika UDSM, leo Jumatatu Machi 11, 2024.


Majadiliano Rika (Intergenerational Dialogues) ndani ya vyama vya kisiasa ni muhimu kwa ajili ya kujenga uzoefu na kuongeza maarifa kwaniyanaongeza mwingiliano kati ya vijana, watu wa umri wa kati, na wazee. Majadiliano haya pia yanasaidia kukuza ushiriki wenye ufanisi na uwakilishi wenye maana katika medani ya kisiasa.

Vilevile, Majadiliano haya husaidia katika kujenga uelewa wa pamoja kwa kila kundi na hatimaye kusaidia katika kukabiliana na changamoto ambazo vijana wanakabiliana nazo kuhusiana na ushiriki wao katika michakato ya kisiasa na uchaguzi.

Kuelewa jukumu muhimu la mazungumzo ya kizazi kwa kizazi, TCD inalenga kuwaleta pamoja viongozi wa vyama vya kisiasa wa makundi mbalimbali ya umri katika mchakato wa kisiasa kama njia ya kubadilishana mbinu za uongozi na uzoefu ili kuboresha ushirikiano ndani ya mchakato wa utawala wa kidemokrasia. Inatarajiwa kwamba kupitia majadiliano, vijana watapata habari muhimu kwa ajili ya ushiriki na uwakilishi wao katika michakato ya kisiasa na uchaguzi.

Baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaoshiriki katika mazungumzo haya ni pamoja na Zitto Kabwe, Abdulrahman Kinana au Emannuel Nchimbi, Freeman Mbowe, Prof. Ibrahim Lipumba, Joseph Selasini na John Cheyo, John Mnyika n.k. Lakini pia, Balozi wa Marekani, Michael Battle, pamoja na balozi wa Uholanzi, Wiebe de Boer, ni miongoni mwa wageni wengine wanaohudhuria mazungumzo haya.

Endelea kufuatilia kupata updates zaidi...

Selasini na Lipumba + Nyahoza
 
MICHAEL BATTLE, Balozi wa Marekani
"Tanzania imefanikiwa kuwa na bahati ya kuwa na viongozi wanaojali maslahi ya Nchi na ndio maana wakaruhusu uwepo wa vyama vingi na kuruhusu ukuaji wa Demokrasia."

Balozi amenunuliwa...?🙄

Maana maslahi ya nchi ni zaidi ya kuwa na vyama vya vingi. Mengi yanayoendelea sasa hivi sio kwa maslahi ya nchi wala ya wananchi, ni ya wenye nchi na vizazi vyao.
 
MICHAEL BATTLE, Balozi wa Marekani
"Tanzania imefanikiwa kuwa na bahati ya kuwa na viongozi wanaojali maslahi ya Nchi na ndio maana wakaruhusu uwepo wa vyama vingi na kuruhusu ukuaji wa Demokrasia."

Balozi amenunuliwa...?🙄

Maana maslahi ya nchi ni zaidi ya kuwa na vyama vya vingi. Mengi yanayoendelea sasa hivi sio kwa maslahi ya nchi wala ya wananchi, ni ya wenye nchi na vizazi vyao.
Siyo kununuliwa, hawa huwa wanafiki watupu!
 
Back
Top Bottom