SoC01 Mambo ya kuzingatia kabla ya kuhamia Dar es Salaam

Stories of Change - 2021 Competition

Mancobra

Member
May 31, 2021
54
95
Jiji la Dar es Salaam lipo kati ya latitudo nyuzi 6 hadi 7 na longitudo kati 39.45 kwa upande wa Mashariki na nyuzi 39 kwa upande wa magharibi, Kusini mwa ikweta na upande wa magharibi, Kusini na Kaskazini. Jiji linapakana na Mkoa wa Pwani, upande wa Mashariki linapaka na Bahari ya Hindi. Jiji la Dar es Salaam lina eneo la ukubwa wa kilomita za Mraba zipatazo 1,800; kati ya hizo, kilomita za mraba 1,350 ni eneo la nchi kavu ikijumuisha visiwa vinane vilivyopo katika eneo la bahari ya Hindi. Jiji hupata joto la wastani wa kati ya nyuzi 25 hadi 33 na mvua katika misimu miwili ya vuli ambayo ni miezi ya Oktoba Desemba na Masika ambayo huanza miezi ya Machi Mei. Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 Jiji lina idadi ya watu 4,364,541, ambapo kati yao wanaume ni 2,125,786 na wanawake ni 2,238,755.

Jiji la Dar es salaam ni jiji lenye shughuli nyingi za kijamii, kiuchumi, kisiasa na kijamii. ndani ya jiji la Dar es salaam ndipo inapatikana miundombinu ya kisasa zaidi kuliko sehemu yoyote Tanzania, kuna barabara za mwendokasi, flyover na majengo mengi marefu(ghorofa). Kwenye huduma za kijamii mfano huduma za afya kuna hospitali za viwango vya juu kama Muhimbili, Aga Khan, Ocean road na Temeke hospital. Lakini pia Dar kuna vyuo vingi vizuri kama MUHAS, DIT, IFM na UD. Kwenye upande wa biashara kuna soko kuu la Kariakoo, Karume na masoko mengine mengi ambayo yana mzunguko mzuri wa pesa. Kwenye upande wa starehe ndani ya jiji la Dar kuna kumbi nyingi za starehe za kuanzia hadhi ya chini mpaka juu; kuna Samaki Samaki, Nextdoor - Masaki na Dar Live.

Kutokana na sifa za jiji la Dar kuwa kitovu cha biashara nchini Tanzania, vijana wengi kutoka mikoa mbalimbali hutamani kuja Dar es salaam wakiamini watakua na uhakika wa kupata maisha bora. VIjana huamini kuwa kwa kufika Dar wataweza kupata vitu vifuatavyo;​
  1. kupata ajira nzuri(hata wasiokua na elimu huamini hivyo pia).​
  2. kupata pesa nyingi kwa wakati mfupi.​
  3. kupata huduma za kijamii kwa uhakika(maji, umeme na huduma za afya).​
  4. Wataweza kufanikisha ndoto zao kama kuwa msanii, muigizaji na mchezaji mpira.​
Mitazamo hii ya vijana huwafanya kuwekeza nguvu nyingi kwenye kutafuta pesa ya nauli na pesa ya kujikimu wafikapo jijini. Lakini pia, kutokana na akili zao kufocus zaidi kuja Dar, vijana wengi wanafanikiwa kuona fursa za kiuchumi zinazopatikana kwenye maeneo yao. Hivo basi, vijana hupambana kwa nguvu zote kupata nauli na pesa ya kujikimu na wengi hufanikiwa kufika jiji la Dar es salaam. Baada ya kufika Dar na kukaa kwa muda mfupi tu, vijana(kike na kiume) hugundua mambo yafuatayo;​
  1. Ajira ni ngumu sana: vijana wenzao waliowatangulia kutoka mikoani wanafanya kazi za kawaida sana na nyingine za kujidhalilisha(mfano ukahaba) tofauti na walivyokua wanawaza kabla ya kuja. Hawa vijana wa mikoani wengine hufanikiwa kukutana na rafiki, ndugu na jamaa zao wa mikoani na kuona wanavyotaabika na maisha ya Dar es salaam.​
  2. Pesa haipatikani kirahisi rahisi kama walivyofikiri: Baada ya kutoka mkoani, vijana wa mkoa hushangaa kuona fursa walizoziona na kuzisikia kwenye media hazipo tena. Hii hupelekea kutumia hovyo pesa walizokua wamepanga kama mtaji wakiwa Dar. Mwisho wa siku mipango ya kuzalisha pesa waliyokua nayo inakufa.​
  3. Upatikanaji wa huduma za kijamii kama huna pesa ni bora uishi mkoani: Vijana wa mkoani watagundua kuwa usipokua na pesa huduma za kijamii(maji,umeme na afya) utaishia kuziona bila kupata huduma. Hapo ndipo watakapokumbuka bora mkoani unaweza kuomba kwa jirani maji ya kunywa ila sio huku Dar.​
  4. Kuna kazi ya ziada inabidi ufanye kufikia ndoto yako: Baada ya kufika Dar, vijana wa mikoani watagundua ili uwe msanii, mfanyabiashara mkubwa, muigizaji na tajiri ni lazima upambane sana na kufika Dar pekee haitoshi kufanikisha ndoto zako. Na wengine watagundua kuwa ili ndoto itimie ni lazima arudi mkoani kwanza ndo baadae arudi Dar.​
  5. Maisha ya watu wengi ni fake sio real: Mitandao ilichangia kuwaaminisha kuwa role mode wao(mfano, wasanii), rafiki na ndugu zao wana pesa nyingi na maisha mazuri. Baada ya kufika mjini wanakuta vitu ni tofauti kabisa.​
Hayo ni matokeo baada ya kukaa muda mfupi tu. Kadri muda utakavyosonga mbele kuna vijana huamua kurudisha mpira kwa kipa( kurudi mkoani) na wengine hukomaa jijini. Kwa wanaokomaa jijini(wale wanaokaa muda mrefu), kuna baadhi hujihusisha na mambo yafuatayo;​
  1. Utapeli, wizi na ukabaji: Baada ya maisha kuwa magumu na kukosa hela ya nauli, vijana hawa huamua kujipatia kipato kwa njia zisizo halali. Hii hutokea sana unakutana na mtu mmetoka sehemu moja anakutapeli mchana kweupe kwa kufifanya mjanja, hii inatokana na ugumu wa maisha.​
  2. Omba omba: Unakuta kijana kila siku anaomba pesa japokua hana ulemavu wowote. Hii inasababishwa na kukosa kazi ya kufanya ya kujiingizia kipato. Hawa ndo wale ukijuana nae muda huo huo anakuomba pesa.​
  3. Ukahaba na ushoga: Dada zetu wanaojiuza sinza, samaki samaki na mitaa mingi ya Dar asilimia kubwa inatokana na ugumu wa maisha. Wa kiume nao huamua kulawitiwa ili wapate chochote kitu. Be careful.​
  4. Matumizi ya madawa ya kulevya: Hii inatokana na msongo wa mawazo baada ya kukosa pesa, wengi hujikuta wanavuta bangi hovyo hovyo, cocaine na heroin.​
  5. Kulelewa: kwa vijana wa kiume wengne wanajikuta wanalelewa na masuggar mummy na sometime hupelekea kupata magonjwa lakini pia kukosa uhuru wao kama watoto wa kiume.​
Kutokana na hali halisi ya jijini Dar es salaam ilivyo, wenye pesa ndo hufaidi mambo unayoyaona kwenye luninga wakazi anasema "Dar es salam vitamu wanafaidi magwiji" na ndo ukweli kabsa. Sio tatzo kwa kijana wa mkoani kuja Dar, kabla ya kuja Dar jiulize maswali yafuatayo​
  1. umejipanga vipi kuishi na kukabiliana na changamoto za Dar?​
  2. Je, ndoto zako zinaendana na mazingira ya Dar?​
  3. Mambo yakiwa tofauti na ulivyotegemea utafanya nini?​
  4. Je, kazi unayotegemea kufanya ukiwa Dar kwenye mazingira yako hiyo fursa haipo?​
  5. Je, kuna watu wa kukusupport ukifika Dar?​
Ukishajiuliza hayo maswali na kupata majibu unaweza kuja au kutokuja kulingana na majibu yako. Hivyo basi, kabla ya kufanya maamuzi ya kutoka mkoani na kuja Dar, kijana ni lazima uwe na vitu vifuatavyo;
  1. ujuzi wowote; hapa inategemeana na malengo yako, unaweza kuwa fundi, mjasiriamali na dereva.
  2. Mtaji: Hii ni muhimu zaidi kwa wale wanaokuja kutafuta maisha bila kutegemea mtu.
  3. Mentor: Huyu ni mtu anayeishi Dar na kuyajua mazingira na kitu unachotaka kufanya. Mentor ni muhimu sana kwenye kufanikisha malengo.​
  4. Lifeskills: Ujue jinsi ya kuishi na watu vizuri. maisha ni watu.​
  5. Nidhamu ya pesa.​
Hitimisho, maisha popote ila kabla ya kwenda sehemu lazima ujipange kiakili na kiuchumi la sivyo utaishia kushindwa, kuabika na kufanya maamuzi yasiyo na maana. Kumbuka kua hata sehemu uliyotoka kuna fursa pia, jiulize, hiyo kazi uliyofanya kupata hela ya nauli ni kwa nini usiendelee nayo ikupe kipato?. Usije mjini kama huna pa kuanzia.​
 
Makala nzuri Sana lkn nigependa utoe mapendekezo kwa jamii kiujumla nn kifanyanyike kuwasaidia awa vijana wa aina hii
 
Makala nzuri Sana lkn nigependa utoe mapendekezo kwa jamii kiujumla nn kifanyanyike kuwasaidia awa vijana wa aina hii

Makala nzuri Sana lkn nigependa utoe mapendekezo kwa jamii kiujumla nn kifanyanyike kuwasaidia awa vijana wa aina hii
Kwanza, ni lazima kijana ajitambue yeye mwenyewe lengo la kutoka nyumban kwenda Dar kutafuta maisha. Ni lazma awe anajua fursa zinazopatikana kwenye mazngra yake na kuona kama zinamfaa au la.
Hili suala la vijana kutamani kuhamia Dar ni suala la uelewa tu na jamii kuanzia level ya familia mpka taifa yani wazazi na serikali inabidi watoe malezi na elimu bora ya kuwawezesha watoto watambue fursa zinazopatikan kwenye mazingira yao.
Lakin pia uwepo wa shughuli za kibiashara kama viwanda, kilimo na miundombinu bora mikoani itasaidia vijana kupata ajira na kumudu gharama za maisha mikoani bila kutaman kuhama.
Hivyobasi, sera nzuri ya serikali kujenga miundombinu mikoani itasaidia kupunguza tatzo na vijana inabidi wapende kazi bila kubagua aina ya kazi mfano, kilimo.
 
Back
Top Bottom