SoC03 Mambo ya kuzingatia ili kupandisha uchumi wa nchi na wananchi pamoja na kupandisha thamani ya pesa ya Tanzania

Stories of Change - 2023 Competition

sideuka

Member
May 18, 2023
5
5
Nawasalimu Kwa jina la Muungano wa Tanzania.Ni matumaini yangu kuwa mmejibu Kazi iendelee.

Katika makala hii leo napenda kuzungumzia vitu ambavyo vinafanya uchumi wa nchi kuimarika bila kusahau jinsi ambavyo thamani ya pesa yetu itakavyoweza kupanda na kuwa moja kati ya pesa zenye thamani kubwa Duniani kama ilivyo kwa mataifa mengine Duniani au hata baadhi ya nchi nyingine zinazotuzunguka mfano mzuri mpa kasasa shilingi moja ya Tanzania ni sawa na kwacha sifuri nukta sifuri sifuri nane mbili ya Zambia pia shilingi moja ya Tanzania ni sawa na shilingi sifuri nukta sifuri tano tisa kwa shilingi ya Kenya lakini shilingi moja ya Tanzania ni sawa na shilingi moja nukta sita sifuri kwa shilingi ya Uganda.

Katika mifano hii utaona kuwa shilingi ya Tanzania ipo chini kithamani ukilinganisha na shilingi ya Kenya na kwacha ya Zambia lakini shilingi ya Uganda imekuwa chini katika shilingi ya Tanzania. Swali nini kifanyike ili kuweza kuifanya shilingi ya Tanzania iweze kuwa moja ya pesa yenye thamani kubwa Africa na nje ya Africa ? zifuatazo ni baadhi ya njia ambazo serikali na menejimenti zake zikizizingatia zinaweza zikaifanya pesa ya Tanzania kuwa na thamani kubwa zaidi.

Moja, Uwekezaji, serikali inabidi ijikite katika uwekezaji wa miradi mbalimbali ndani na nje ya nchi hii itafanya serikali kukusanya pesa nyingi kila mwaka kuliko kutegemea wawekezaji wa nje waje kuwekeza ndani nakujikusanyia mapato kwa nchi yao na kulipo kodi kidogo kwa serikali ningeshauri kuwa serikali iwekeze kwenye miradi mikubwa kama vile kwenye umeme kwenye bandari na sekta nyingine mbalimbali zenye kuingiza kipato cha nchi mfano katika sekta ya madini.

mbili, kupunguza matumizi ya pesa yasiyo ya lazima , ili nchi iweze kuwa na pesa yakutosha nayenye thamani inapasa kupunguza matumizi ambayo sio ya lazima baadhi ya matumizi ni kuachana na baadhi ya sherehe, sherehe zinagharimu pesa nyingi na badala yake pesa hizo zitumike katika uwekezaji wa vitu vingine ambavyo vitaizalisha faida maradufu kuliko kuitumia pesa hiyo katika tukio la siku moja kwa kufanya hivyo itafanya thamani ya pesa ya nchi kupanda vile vile kutawezesha uchumi wa wanachi kupanda kwakuwa uwekezaji mkubwa upo kwa wananchi mfano serikali inaweza ikawakopesha wananchi pesa kwa riba ndogo na kukusanya faida baada ya muda badala ya kuitumia pesa hiyo kwa sherehe au jambo ambalo halina faida ila linahitaji matumizi makubwa ya pesa.

Tatu, Wazawa wapewe kipaumbele kwenye tenda mbalimbali za serikali, kama serikali itakuwa inawapa wazawa tenda zake basi itakuwa inagusa moja kwa moja maisha ya wananchi pili itakuwa inafanya mzunguko wa pesa zake ndani ya nchi nakufanya nchi kuwa napesa nyingi kuliko kuwapa tenda watu wanje ambao mwisho wa siku wataondoka na pesa za nchi na kuacha nchi haina kitu.

Nne, kupunguza madeni, Tunaona kila siku jinsi watu wanavyofilisiwa na makampuni mbalimbali ya mikopo hii sio kwa wananchi tu hadi katika serkali ipo endapo kama nchi itkuwa na madeni na ikashindwa kuyalipa lazima itafilisiwa baadhi ya miradi na kuifanya nchi kuwa msikini hivyo ili nchi iwe na uchumi imara na pesa yenye thamani inapaswa kupunguza mikopo, mikopo isiwe mingi kupita bajeti ya nchi kwa kufanya hivyo nchi itakuwa na pesa yenye thamani na nguvu.

Tano, utafutaji wa masoko, niwazi kuwa nchi ya Tanzania inautajiri mkubwa wa mazao ya chakula na mazao ya biashara hivyo itakuwa vyema kama serikali itasimama vyema kuwatafutia wananchi masoko yenye bei nzuri za mazao yao kuliko kuwaacha wananchi kujiamuria tu kuuza mazao yao na mwisho wa siku kujikuta kuwa wanapata hasara au kama inawezekana serikali ndio iwe mnunuzi mkuu wa mazao ya wananchi hii itamgusa mwananchi wa chini kabisa nakumfanya apate tija ya kile alichokifanya kwa mikono yake. Tena katika hili serikali inaweza ikatengeneza viwanda vya uchakataji mazao na kuuza bidhaa hizo za mazao nje ya nchi hii itafanya nchi iongeze pato na thamani ya pesa.

Sita, utoaji wa elimu mbalimbali kwa wananchi nakuwawezesha wananchi, kila serikali Duniani inategemea mapato kutoka kwa wananchi kupitia ulipaji wa kodi hivyo mwananchi ambae hana chanzo cha kipato inakuwa ngumu kulipa kodi kwa serikali badala yake anakuwa anaitegemea serikali hivyo ili kuliepusha hili serikali inapaswa kutoa elimu kwa wanachi na kuwagawia mitaji ambayo mwisho wa siku mitaji hiyo itatoa faida na kuweza kuongeza pato la Taifa vile utoaji wa elimu kwa wananchi itasaidia ongezeko laupatikanji wa ajira kwa wananchi na hivyo kufanya pato la taifa kuongezeka.

Mwisho mwishoni napenda kutoa shukrani zangu Kwa serikali kwakuweza kugusa maisha ya wananchi hasa katika Nyanja ya nishati, elimu pamoja na miundo mbinu lakini naomba niishauri serikali yangu Tukufu kuwa inahitaji kuchukua hatuathabiti katika uwekezaji kwani ikifanikiwa katika hili naiona Tanzania ni moja kati ya nchi imara sana huko mbeleni.
 
Back
Top Bottom