Mambo ya 50/50 binafsi mnitoe siyatakiiii

Mambo ya 50/50 binafsi mnitoe siyatakiiii

Hausaidii mwanaume anapokwama bali unahusika kuendesha familia kwa kipato chako, nguvu kazi, usimamizi n.k. Yani ukiwa kwenye ndoa lazima uwe na mchango wa kuendesha familia, huwezi kusema upo tu kama boga au Jiwe kwa sababu ni mwanamke huna mchango wowote au eti ni kama fire hadi moto uwake ndio ujitokeze kuzima. Lazima uwe active kuendesha familia.

Unapoteza kufafanua hayo.

Ukitaka ujue kwa nini familia nyingi za kiafrika ni maskini na zitadumu kwenye umaskini angalia comments humu JF.

Hasa mambo ya Kifamilia.
Wanawake wa kiafrika wamejengewa fikra za kimaskini. Kutokuwa na tija.

Fikiria mwanamke anafikiria yeye ni pambo tuu. Uliona wapi mwanamke wa maana akawaza hivyo?

Mwanamke ni zaidi ya pambo.

Fikiria mwanamke kumnunulia mumewe zawadi anaona kafanya Jambo kubwa Sana maishani😂 au kulipia bills. Alafu useme umeoa au unamke?
 
ephen_ kwenye ndoa au ile ya kuishi pamoja , huyo ni life partner wako, mnafanya mambo kwa pamoja , mnajenga familia kwa pamoja na pesa zenu ni mali ya familia , hakuna mwenye pesa zake binafsi , yeyote atakae dokoa pesa kaibia familia, hakuna kuhongana humo, kwa sababu vyote ni vyenu, ukiona kwenye ndoa mnahongana wewe jua tu nyie ni wahalifu na majambazi mlio amua kuishi pamoja , mnaviziana tu .
Nilifikiri hii ni common sense tu kumbe common sense is not so common!
 
Kwenye ndoa , hakuna pesa yangu na pesa yako linapokuja suala la ustawi wa familia..
Wote wana haki ya kutunzwa, inabidi kutunzana..
Mtasaidiazana kwenye dharura..
Hio sio charity organization kwamba mmoja ni mfadhili na mwingine ni mnufaika..

Mwanaume ana haki pia ya kupunguziwa mizigo ya kiuchumi na mkewe, hasa kama mke ana uwezo mkubwa...

Ukipata mwanamke mwenye mtazamo kama huu hesabu umekutana na muujiza
 
Vip? Kuhusu mmeo wa ndoa akipiga chini kiuchumi na wewe unajiweza kwa kipindi icho

utamsaidia majukumu au utatafuta wanaume wengine wakusaidie majukumu ya ndani kwako, kwa kigezo cha hauwezi kutoa pesa yako wakati wanaume wapo!!
 
Namimi baada ya City kutoa sare na Bournemouth nikaamua kuchukua likizo fupi hapa jukwaani maana huku mtaani nako nilikuwa napitia magumu kwa hiyo sikujua ni wapi nitakuwa safe dhidi ya harassments zenu.

Mpaka pale nilipoona ku stream series ndio njia pekee ya ku avoid hayo yote.
Tuache utani ume preach somo zuri kwa huu uzi, ila harass iko pale pale viva arsenal 🔥
 
ephen_ kwenye ndoa au ile ya kuishi pamoja , huyo ni life partner wako, mnafanya mambo kwa pamoja , mnajenga familia kwa pamoja na pesa zenu ni mali ya familia , hakuna mwenye pesa zake binafsi , yeyote atakae dokoa pesa kaibia familia, hakuna kuhongana humo, kwa sababu vyote ni vyenu, ukiona kwenye ndoa mnahongana wewe jua tu nyie ni wahalifu na majambazi mlio amua kuishi pamoja , mnaviziana tu .

Ndio hiki anachokielezea mtoa mada.. utapeli.
Zakwake ziwe zakwake. Zako ziwe za wote.

Katika vitu mwanaume anatakiwa kuomba ni kukutana na mwanamke mwenye fikra hizi au aliyelelewa na Mama mwenye fikra hizi
 
ephen_ kwenye ndoa au ile ya kuishi pamoja , huyo ni life partner wako, mnafanya mambo kwa pamoja , mnajenga familia kwa pamoja na pesa zenu ni mali ya familia , hakuna mwenye pesa zake binafsi , yeyote atakae dokoa pesa kaibia familia, hakuna kuhongana humo, kwa sababu vyote ni vyenu, ukiona kwenye ndoa mnahongana wewe jua tu nyie ni wahalifu na majambazi mlio amua kuishi pamoja , mnaviziana tu .
Comments za mtibeli zimenifanya nisimulie kisa cha kaka yangu.

Yeye na mkewe walifunga ndoa 2015, hawana mtoto, mkewe hajawahi kufanya kazi yoyote.
Ashamfungulia mkewe saloon, min market, duka lakini vyote vilikufa chanzo mkewe hataki kwenda kuvisimamia! Yeye anataka kukaa tu wafanyakazi wamletee hesabu nyumbani.

Anajuta kumuoa ila hawezi kumuacha kisa nyumba yao aliandika jina la mkewe.
Sasa hivi nyumbani kwao wana housegirls wawili kumbuka hawana mtoto na mke yupo tu nyumbani.

Kinqchomsikitisha amegundua kua mkewe kamjengea mama yake nyumba ya kisasa kijijini kwao.
Anajiuliza mkewe hela kapata wapi?
Nilimwambia bila kumficha kua nyumba imejengwa kwa pesa zake kaka yangu😂
 
Guys kuna raha kua Mwanamke na raha ya Mwanamke kuhudumiwa,
acheni sasa niwaambie mimi ni yule mwanamke hata nikipata mshahara sasa hivi, bado nitapiga simu kwa kaka zangu (wananipenda sana lastborn wao) wanitumie hela ya chips au icecream,
Siwezi kwenda lunch na kuna wanaume halafu mimi nilipe bill hata kama ni yangu, hapana nitatulia tuliii wanaume walipie,😐

Kuna siku ilikua lunch na co-workers sasa bill ilivyofika mdada mmoja naona anafungua wallet weeh acha nimpige kofi la bega, akashtuka nikamwambia "tulia ufurahie uanamke wako" akacheka akaweka wallet chini,🙃

Tukija nyumbani ndio kabisaaaa siwezi kubeba majukumu ya kununua chakula na kulipa bills, nope! labda kununua vitu vidogo vidogo kama chumvi na viberiti au snacks zangu, lol

Haya mambo ya 50/50 yaishie kwenye mabiashara hukooo ila kwenye mahusiano hapana jamani kila mtu asimamie majukumu yake yanayomuhusu, mimi jukumu langu ni kuleta utulivu, nuru na amani nyumbani,
Mtauliza sasa wewe mshahara wako unaufanyia nini sawa nitajibu, nanunua vitu vidogo vidogo kama mapambo ya ndani, kufix issues ndogo ndogo zitakazojitokeza na kuspend kwenye mambo yangu,🥰 wanawake tuna vitu vingi jamani na pesa kwetu haijawahi kutosha,😂

Ewe mwanamke unayejiita mwanamke wa shoka, unayevuja jasho na damu ili kuhudumia familia kwanza nakupongeza sana ila kama ukipata nafasi ya kufanyiwa jiachie ufanyiwe, Mwanamke ni pambo la dunia, kaumbiwa kutunzwa, kudekezwa, kupendwa, kubembelezwa, mwanamke anatakiwa awe laini laini sio wanaume wapo wewe mwanamke unabeba ngazi unaparamia ukuta kuweka umeme au unapanda kwenye stuli kufunga kamba za nguo jamani mtakuja kutenguka nyonga mshindwe kutoa raha kwa my zenu,🙄

Binafsi hizo 50/50 zenu pelekeni hukoooooooo mimi ni old school naelewa uanamke wangu unathamani kiasi gani.
Tchaooooo
Dr. Mariposa umeacha kusagana?
 
Comments za mtibeli zimenifanya nisimulie kisa cha kaka yangu.

Yeye na mkewe walifunga ndoa 2015, hawana mtoto, mkewe hajawahi kufanya kazi yoyote.
Ashamfungulia mkewe saloon, min market, duka lakini vyote vilikufa chanzo mkewe hataki kwenda kuvisimamia! Yeye anataka kukaa tu wafanyakazi wamletee hesabu nyumbani.

Anajuta kumuoa ila hawezi kumuacha kisa nyumba yao aliandika jina la mkewe.
Sasa hivi nyumbani kwao wana housegirls wawili kumbuka hawana mtoto na mke yupo tu nyumbani.

Kinqchomsikitisha amegundua kua mkewe kamjengea mama yake nyumba ya kisasa kijijini kwao.
Anajiuliza mkewe hela kapata wapi?
Nilimwambia bila kumficha kua nyumba imejengwa kwa pesa zake kaka yangu😂
Hahahaha hizi mambo zipo sana , ndoa za kuviziana , unaibia familia yako unaenda kuboresha familia ya baba yako kama sio ugoigoi ni nini?, mimi hata akichepuka naweza msamehe ila sio kufanya ujambazi ndani ya familia
 
Comments za mtibeli zimenifanya nisimulie kisa cha kaka yangu.

Yeye na mkewe walifunga ndoa 2015, hawana mtoto, mkewe hajawahi kufanya kazi yoyote.
Ashamfungulia mkewe saloon, min market, duka lakini vyote vilikufa chanzo mkewe hataki kwenda kuvisimamia! Yeye anataka kukaa tu wafanyakazi wamletee hesabu nyumbani.

Anajuta kumuoa ila hawezi kumuacha kisa nyumba yao aliandika jina la mkewe.
Sasa hivi nyumbani kwao wana housegirls wawili kumbuka hawana mtoto na mke yupo tu nyumbani.

Kinqchomsikitisha amegundua kua mkewe kamjengea mama yake nyumba ya kisasa kijijini kwao.
Anajiuliza mkewe hela kapata wapi?
Nilimwambia bila kumficha kua nyumba imejengwa kwa pesa zake kaka yangu😂
Huyo si mke bali mgidaji na ipo siku atamkimbia kaka yako
 
Suala la kuendesha familia kama mke na mume huwa nafikiri liko straight sana wala halihitaji mijadala mingi lakini huwa nashangaa linaibua mijadala mingi sana mikali na ya kushangaza kwenye roles na uwajibikaji.
Kabisa limenyooka mno , na kuna wanawake na wanaume wamenyooka pia , ila majambazi wamejazana ndani ya familia ndio wanaibua mizozo
 
Back
Top Bottom