Mambo ya 50/50 binafsi mnitoe siyatakiiii

Mambo ya 50/50 binafsi mnitoe siyatakiiii

Kuombana pesa kwa wanandoa sio lugha sahihi, labda useme mwanamke anakuwa anamkumbusha mume kuna mahitaji gani kwenye familia.

Kama mwanaume ana biashara zake za maana au ajira inayompa kipato kikubwa kuliko mke automatically tu atakuwa analipa kodi au ajenge nyumba, atanunua usafiri wake ambao utakuwa ndio wa familia, atakuwa analipa ada, gharama za matibabu/bima hapo utakuta huyo mke mwenye kipato kidogo au cha kawaida labda ananunua chakula na vikorokoro vyake vidogo vidogo huko vya kujiremba, hapo huwezi kusema kuna kuombana pesa au 50/50.

Ishu ukute mwanamke ana kipato kikubwa zaidi kuliko mwanaume au sawa na hashindi nyumbani halafu hachangii pia chochote cha maana katika kuendesha familia. Au tatizo lengine ni pale mke anapoanza kutaka pesa za mume wake kujengea wazazi wake au kuhudumia ndugu zake, hapo sasa ndio itabidi aanze kuomba na wanaume wengi ndio huwa vichwa vinapata moto.
Mwanamke hata kama hashindi nyumbani akirudi anakupikia, anatunza watoto, anakufulia na mengine mengi. Unless uniambie majukumu ya nyumbani mnashea nitakubaliana na hiyo 50/50, hilo ni jukumu lako wewe
 
Seran wewe unasemaje kuhusu mada? Mbona hutoi msimamo wako?
Acha tu😓
DD9B319A-5938-453A-A6BB-8B2D898CB03F.jpeg
 
Nikiwa popote na mwanamke then akajifanya anataka alipe bill ambayo tumekula au kunywa pahala, huwa namzuia nailipa mm mwenyewe

Then after hapo hata sms hapati kutoka kwangu na sim zake sipokei.. dharau sana nitoke na wewe then ujifanye kulipia bill

Nachukia sana
Kama ni wakumtumia tu mpe mnunulie anachotaka , mhonge . Ila kama unataka awe mke wa kuoa umakini mkubwa unahitajika usije fuga jambazi ndani

Note: Haya madini nimeyatoa kwa bi mkubwa kabisa😅
 
Hizo shughuli za kulea watoto Siku hizi zinafanywa na house girl na daycare.
Sijui ni kipi hujaelewa,
Kama mwanamke anashinda nyumbani na halei watoto anamuachia house girl au anawapeleka daycare hilo ni tatizo na ndicho nilichokisema hapo anakuwa hana mchango wowote katika familia. Hata hivyo ni vizuri kufahamu pia kama mwanamke ana watoto wengi ni vigumu kuhudumia mwenyewe bila usaidizi wa ndugu au house girl, au vinginevyo atawageuza watoto wakubwa wawe ndio house girls .
 
Ndoa inamnufaisha mwanamke kuliko mwanaume.

Mwamaume kwenye ndoa anachohitaji ni Sex ambayo hata nje anaweza kuipata.
Nje ya hapo mwanaume hategemei chochote kutoka kwenye ndoa.

Wanawake wanapata vingi kwenye ndoa
Kuanzia sex, huduma, ulinzi, n.k

Ndio, ndoa ni dili kwa mwanamke, mwanamke ndio mshindi kwenye ndoa, sherehe ya "Send off" watu wengi wanafikiri ni kumuuga bi harusi, ni sherehe ya kumpongeza kwa ushindi huo, kumpa zawadi kemkem na kumpongeza. 😊
 
Kwenye ndoa , hakuna pesa yangu na pesa yako linapokuja suala la ustawi wa familia..
Wote wana haki ya kutunzwa, inabidi kutunzana..
Mtasaidiazana kwenye dharura..
Hio sio charity organization kwamba mmoja ni mfadhili na mwingine ni mnufaika..

Mwanaume ana haki pia ya kupunguziwa mizigo ya kiuchumi na mkewe, hasa kama mke ana uwezo mkubwa...
Asaidiwe pale alipokwama sio kugawana nusu kwa nusu
 
Kama ni wakumtumia tu mpe mnunulie anachotaka , mhonge . Ila kama unataka awe mke wa kuoa umakini mkubwa unahitajika usije fuga jambazi ndani

Note: Haya madini nimeyatoa kwa bi mkubwa kabisa😅
Angelikiwa anataka kumuoa kuna process angezilifata

Mpaka kamuita gizani anataka nyara kwa njia za haramu

Inabidi binti ashtukie mchezo asiwe mzembe

Aweke urithi wa wanae kabla hawajazaliwa

Jacklin mengi
 
Sijasoma comments zote lakini naona broke guys wamepanic sanaaaaa, shida inaweza kua nini jamaniiii me nachokaaaa, anyway nitarudi tena lunch time
Raha ya mahusiano ni mwanaume kwa hiyali yake anakuhudumia sio mwanamke kugeuka kuwa omba omba ukinaona hivyo ujue wewe kama mwanamke unamapungufu mengi ya kike.
 
Safi sana mtibeli,

Kwenye kikao chetu kijacho,utakaa mstari wa mbele kabisa.

Wanawake wengi wanataka wawe kama Malkia, wakae tuum KAZI hawataki kufanya, wakiwa nyumbani house girl kazi zote, watoto analea house girl. Mke kazi yake kujizungusha zungusha na kujipigisha kelele za kijinga.
Ambazo kelele hizohizo ukimuelekeza yeye halitaki. Linaona linanyanyaswa.

Ni wanawake wachache anaweza kumsaidia House girl.

Haya kuna yale yanayofanya KAZI yameajiriwa. Haya ndio kabisa yaani ukisikia koroma ndio haya
Kazi unafanya pesa zako hutaki ziguswe. Aiseeh! Labda sio Watibeli.

Unafanya kazi pesa lazima zitumike.
Uchague kukaa nyumbani ulee watoto na kusaidiana na house girl (suria) majukumu au uchague kazi ndoa ivunjwe mapema tuu bila kikao. Maelezo utaenda kuwapa wewe.
Sisi wengine hatutakuwa na muda wa kujibu maswali
 
Asaidiwe pale alipokwama sio kugawana nusu kwa nusu
Hausaidii mwanaume anapokwama bali unahusika kuendesha familia kwa kipato chako, nguvu kazi, usimamizi n.k. Yani ukiwa kwenye ndoa lazima uwe na mchango wa kuendesha familia, huwezi kusema upo tu kama boga au Jiwe kwa sababu ni mwanamke huna mchango wowote au eti ni kama fire hadi moto uwake ndio ujitokeze kuzima. Lazima uwe active kuendesha familia.
 
Sijui ni kipi hujaelewa,
Kama mwanamke anashinda nyumbani na halei watoto anamuachia house girl au anawapeleka daycare hilo ni tatizo na ndicho nilichokisema hapo anakuwa hana mchango wowote katika familia. Hata hivyo ni vizuri kufahamu pia kama mwanamke ana watoto wengi ni vigumu kuhudumia mwenyewe bila usaidizi wa ndugu au house girl, au vinginevyo atawageuza watoto wakubwa wawe ndio house girls .

Upo sahihi kabisa.

Ninachokuambia ni kile kinachoendelea kwa kizazi hiki.
Wanawake wengi kazi hawataki, mtoto Hana, na bado anahitaji maid WA kumsaidia kazi ambazo angeweza kufanya mwenyewe.

Wewe unafikiri kwa nini kuna ongezeko kubwa la kataa ndoa?

Ni kwamba Wanawake wengi hawana tija. Nje ya kuzaa hawana mchango wa maana wowote ule.

Nani atakubali kukaa na mzigo?
 
ephen_ kwenye ndoa au ile ya kuishi pamoja , huyo ni life partner wako, mnafanya mambo kwa pamoja , mnajenga familia kwa pamoja na pesa zenu ni mali ya familia , hakuna mwenye pesa zake binafsi , yeyote atakae dokoa pesa kaibia familia, hakuna kuhongana humo, kwa sababu vyote ni vyenu, ukiona kwenye ndoa mnahongana wewe jua tu nyie ni wahalifu na majambazi mlio amua kuishi pamoja , mnaviziana tu .
 
I took a break baada ya kipigo cha city, huku niona nili rejea game 6 kabla ya ubingwa.
Namimi baada ya City kutoa sare na Bournemouth nikaamua kuchukua likizo fupi hapa jukwaani maana huku mtaani nako nilikuwa napitia magumu kwa hiyo sikujua ni wapi nitakuwa safe dhidi ya harassments zenu.

Mpaka pale nilipoona ku stream series ndio njia pekee ya ku avoid hayo yote.
 
Back
Top Bottom