Mambo mazito CCM Dodoma: Wajivua gamba?

Mambo mazito CCM Dodoma: Wajivua gamba?

Kama haya ni ya kweli, basi CCM haina shukrani. Makamba kawapigania siku zote! Alikubali kupakwa matope ya chama akabaki nayo ili chama kinusurike! Eti kaondoka kirahisi hivyo? Makamba usijali Mungu atakulipia!

hahahahahahahahah,,,mkuu, post yako imeniacha hoi sana,,, yani hata kucoment nimeshindwa, nimebaki kucheka tu
 
Fumua fumua CCM, Makamba na Sekretarieti wajiuzulu

Sunday, 10 April 2011

ccmmakamba.jpg

Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba akizungumza kwenye mkutano kwa Kamati Kuu ya chama hicho mjini Dodoma jana kabla ya kujiuzulua.Kushoto ni Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu. Picha na Edwin Mjwahuzi

Waandishi wetu, Dodoma

MABADILIKO makubwa ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) yamefanyika baada ya wajumbe wa sekretarieti ya chama hicho kujiuzulu.

Kutokana na hali hiyo, huenda Kamati Kuu nayo ikajiuzulu na kubakiwa na Mwenyekiti, Rais Jakaya Kikwete, Spika wa Bunge, Anna Makinda ambao wanaingia kwa nafasi zao na John Malecela ambaye ni Mjumbe wa Kudumu.

Habari zilizopatikana kutoka ndani ya kikao cha Kamati Kuu ya CCM iliyokutana mjini Dodoma jana, zinaeleza kuwa hatua hiyo inatokana na mgawanyiko uliokikumba chama hicho.

Hatua hiyo ya kujiuzulu kwa wajumbe wa nafasi nyeti ya chama hicho, inakuja miezi mwili baada ya Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Rais Jakaya Kikwete kueleza wazi kuwa chama kinahitaji kujivua gamba ili kiweze kurejesha heshima yake.

Akihutubia kilele cha maadhimisho ya siku ya kuzaliwa CCM, mjini Dodoma Februari 5 mwaka huu, Rais Kikwete alisema chama hicho kinahitaji mabadiliko makubwa kiweze kurejesha hadhi yake.

Wajumbe waliojiuzulu ni Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba ambaye ni mwenyekiti, manaibu makatibu wakuu wa CCM Bara na Visiwani, George Mkuchika na Saleh Ramadhan Feruzi na Katibu wa Itikadi na Uenezi, John Chiligati.

Wengine ni Katibu wa Uchumi na Fedha, Amos Makala, Katibu wa Mipango, Kidawa Saleh na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mambo ya Nje, Bernard Membe.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo gazeti hili imezipata jana usiku zilieleza kwamba Makamba aliwasilisha barua yake kwa kuiweka kwenye meza ya mwenyekiti kwenye ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.

Taarifa hizo zinasema kuwa baada ya kuwasilisha barua hiyo, Makamba aliomba ruhusa ya kuondoka kwa maelezo kuwa amepata msiba nyumbani kwao Tanga.

Hata hivyo, wajumbe wa kamati hiyo walikataa kutokana na umuhimu wake kwenye kikao hicho, hivyo wakamweleza kuwa atume mwakilishi kwenye msiba.

Habari zaidi zinasema, Makamba amemtuma mwanaye, Januari Makamba ambaye ni mbunge wa Bumbuli mkoani Tanga kwenda kumwakilisha kwenye msiba huo.

Awali wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CC-CCM), waliendelea kuvutana na kusababisha kuahirishwa kwa Mkutano wa Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho kilichokuwa kianze jana.

Kikao cha CC ambacho kilianza juzi jioni kilitarajiwa kumalizika usiku wa siku hiyo na jana kilikuwa kifanyike kikao cha NEC, ajenda kuu ikiwa ni kujadili tathmini ya uchaguzi mkuu uliopita.

Hata hivyo, Kamati Kuu iliyoanza kikao saa 10 jioni juzi, iliahirisha kikao chake saa 1:00 usiku na kurejea tena saa 3:00 hadi saa 5:00 usiku, bila kumaliza kupanga ajenda za NEC.

Wajumbe wa NEC walianza kukusanyika asubuhi jana katika Makao Makuu ya CCM, baadaye walitakiwa kurudi tena saa 7:00 mchana, lakini waliporejea walitakiwa kurudi tena saa 10:00 jioni, pia walitakiwa kurejea leo saa 3:00 asubuhi.

Kuahirishwa kwa kikao cha NEC, kulidaiwa kuwa kumetokana na CC kutomaliza kuandaa ajenda za kikao hicho.

Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho, zilidai kuwa hatua ya kuahirishwa kwa kikao hicho ilitokana na kuwepo kwa mvutano mkali kati ya wajumbe wa CC, wakitaka baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wajiuzulu ili kukinusuru chama kutokana na tuhuma mbalimbali kinazobebeshwa na kuharibu taswira yake.

Kundi hilo linadai pia kuwa kama wajumbe hao watatoswa watakuwa wamewanyima Chadema ajenda mbele ya wananchi, lakini kundi jingine linalowaunga mkono likipinga mapendekezo hayo.

Baadhi ya wenyeviti wa mikoa wa CCM, wanaunga mkono kundi hilo la watuhumiwa lilikuwa likikutana kwenye hoteli moja, wakihaha kuhakikisha ajenda hiyo inazimwa.

Katika mkutano huo, inadaiwa ajenda nyingine iliyokuwa na mvutano zaidi ni ya Muswada wa Sheria ya Kubadilisha Katiba wa 2011 ambapo katika kikao hicho Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Fredrick Werema pia alihudhuria.

Wanaotajwa kurithi nafasi ya Makamba ni, Balozi wa Tanzania nchini Russia, Jaka Mwambi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi na Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk Emmanuel Nchimbi.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Kanali Abdulrahman Kinana, ambaye anadaiwa anaweza kukinusuru chama hicho na mgawanyiko uliopo, anadaiwa kukataa nafasi hiyo baada ya kuombwa na mwenyekiti. Hata hivyo, taarifa zinaeleza kuwa amekubali kuwa Naibu Katibu Mkuu.

Mwingine anayetajwa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Steven Wassira, lakini anahukumiwa na historia yake ya kuhama chama hicho kwenda NCCR-Mageuzi mwaka 1995.

Kikao hicho kinadaiwa pia kujadili matamshi ya kejeli na matusi yaliyotolewa na Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) dhidi ya Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, kuwa yanakigharimu chama.

"Kama kuna kitu kimetugharimu kichama ni kauli za UVCCM, huwezi ukabeza mchango wa Frederick Sumaye. Huyu amelitumikia taifa na chama kwa muda wa mrefu," kilisema chanzo chetu.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati, alisema ngoma bado ni nzito na kuwataka wajumbe wa Nec kuwapo kwa ajili ya kikao leo saa 5:00 asubuhi.

Hata hivyo, Chiligati alikataa kutaja ajenda zilizokuwa zikijadiliwa kupelekwa NEC na kuahidi kuzitaja kwa waandishi wa habari leo saa 3:00 asubuhi.
 
Teh teh kumbe kweli na jk ulikuwa kimkakati tumekutafuta sana kwenye kongamano udom
Watu wakasema unashauriana na jk kuokoa jahazi nikajua wanakuonea wivu kama kawaida yao .teh teh uko kiccm zaidi .
Umeona eee watu wamechangia sana kwenye thread ya Kongamano la CDM Udom jamaa hata hakuona umhimu wa kuchangia wakati ni kongamano la viongozi wake wakuu sasa hili la ukatibu wa CCM ndio kaona lina muhimu zaidi.
 
The more things change the more they remain the same..........................CCM haiwezi kubadilika hadi hapo itakaposhindwa uchaguzi........................hapo massive defections za wale wote ambao matumbo yao ndiyo miungu yao watakapoishia na CCM kurudi kwa walalahoi....................................these are cosmetic reforms aiming to hoodwink the ineptitude..........................I am glad that I am not in that ensemble.......................................................................
 
Jamani hapa Jk usanii mtupu, huyu Zakia Mehgi aliekua maliasili na utalii? Khaaa kweli Jk kachemka.
 
Kwa nini Wilson Mukama Asiwe Katibu Mkuu CCM?
Wazee,
Miongoni mwa hazina kubwa ya ccm ni Bw. Wilson Mukama. Huyu jamaa ni kifaa na hivi karibuni ametumika sana kujaribu kufunikafunika uchafu wa ccm na serikali yake. Inawezekana jk akamteua kuwa Katibu Mkuu wake.
Hizi kweli ni sifa za bora kiongozi au kiongozi bora......................................judge for yourself.....................
 
Comments

1234

0 #56 issa moshi 2011-04-10 17:56 huu ni mwanzo kunasiku hawa watu tunaamini watafika mahakamani kujibu mashitaka kama siyo kunyongwa kabisa kwa mambo waliowafanyia watanzania
Quote

0 #55 JONES 2011-04-10 17:39 KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU,CCM INAPASWA KUACHIA DOLA ILI KUUA MTANDAO WA UFISADI UNAOMALIZA PESA ZETU WATANZANIA.KAMA KWELI WATANZANIA TUNATAKA MABADILIKO 2015 TUIANGUSHE CCM TUKIPE NAFASI CHAMA KINGINE TUEPUKANE NA UFISADI NA UTEGEMEZI KWA WAFADHILI.NCHI YETU SIO MASIKINI ILA VIONGOZI WETU WAKIONGOZWA NA CCM NDIO MASIKINI WA AKILI.
Quote

0 #54 Ralp J. Kimbisa 2011-04-10 17:34 Hata Mubarak alianza hivyo hivyo kufuta Cabinet yote ya mawaziri, lakini bado wananchi hawakuridhika, hadi alipong'olewa.

Iwapo hakuna ufumbuzi wa mikataba mibovu ya madini, umaskini wa watanzania na katiba mpya, kufuta Cabinet sio hoja. Hiyo ni danganya toto tu ili CCM iendelee kubaki madarakani.
Quote

0 #53 Kuzunya 2011-04-10 17:12 I will never forgive Kikwete and Makamba his Mhentor. They have brought us to far! We loved you CCM but Satan loved you more! Sad I will never see you!! Go to Hell CCM, thus where you belong...
Quote

0 #52 Katebo 2011-04-10 17:07 Rais, Mungu akuongezee hekima kuumba chama chako upya, hivyo maombi yatakiwa, vinginevyo 2015 nchi itaandika historia mpya mbele yako. Kujiuzulu ni hekima, hasa kwa wakati huu wa nuru kwa watanzania.MAKAMBA ULIMPENDA SANA LAKINI WANACHAMA HAWAKUMPENDA ZAIDI.
Quote

0 #51 maishaduniangumu JR 2011-04-10 17:05 MAKAMBA AMECHELEWA KUACHIA NGAZI, TUNASUBIRI CHAMA KIPYA CCM-USWAHILI, NA CCM-UFISADI, NA CMM-ITIKADI
Quote

+2 #50 LENGAI 2011-04-10 16:34 CHAMA CHA MAPINDUZI CCM MNATAKIWA MUJIUZULU WOTE CHAMA KIZIKWE. CHAMA HAKINA FAIDA KWA WATANZANIA ZAIDI YA KUTEGEMEA WAFADHILI KWA KILA KITU.JK NAMSIFU KWA KUFUMBIA MACHO MAMBO MUHIMU.EWE MWENYEZI MUNGU MUUMBA MBINGU NA NCHI NA VYOTE VILIVYOMO. TUNAKUOMBA UKIMALIZE HIKI CHAMA CHA MAFISADI TUISHI SALAMA.
Quote

0 #49 MABIHIVANU 2011-04-10 16:20 CCM reforms as a political party needs to go through different phases which all will try to address the crisis of its retrogressing performance in terms of legitimacy to the people. The failure of the out going team led by Makamba to achieve the objectives of the party to the acceptable and desired levels to people led to the emergence of new vigor and was an opportunity to the opposition to use such a weakness as an opportunity for their advancement. To this regard therefore, It is worth saying that there is no suggested sequence of reforms all the components whether structure, process, or people are important and they need to be taken as system for reforms to be successful. The reforms should not end with the people, the party needs to examine, scan and overhaul the processes and structures of the party. The structures if left the newly appointed personnel may be hijacked by the archaic processes and structures, hence yield very little to our expectations. I strongly believe that CCM is still a strong party and has a strong social base compared to other parties. In terms of resources is well endowed both with Human and financial resources.
I am a realist in thinking, and I know well there is no sweet without pain. Some party cadres should have a reasonable degree of tolerance when the change is effected within the party. Politics of witch hunt should come to an end for the interest of the party.
Quote

+1 #48 wise man 2011-04-10 16:18 NASIKITIKA SANA CCM IMEGUNDUA WACHAWI WAKATI KUMEKUCHA. KUWAWEKA WAZEE WENYE UBINAFSI, THULUMA NA WASIOJUA KUWAJIBU WAPIGA KURA VIZURI. HIVI NCHI HII NI YA KIKUNDI CHA WATU?

RAI KWA RAIS
TUNAOMBA UWATOSE BILA HURUMA HAWA MADHALIMU. CHAGUA WAZEE VIJANA WENYE MTAZAMO CHANYA.
Quote

+1 #47 kilangilo 2011-04-10 16:08 OK HUO NI MWANZO 2.TUNATAKA NAS MWENYEKITI AJIUUZULU THEN CHAMA KIFE KWANI MADUDU MLIOYAFANYA YANATOSHA. MLIMNG'ANG'ANIA MAKAMBA UTFIKIRI NI YEYE 2 TANZANIA HII. MAKAMBA ONDOKA NA MWANAO PIA AONDOKE KA2MTAKI.
Quote

+1 #46 stone 2011-04-10 16:05 Kifo cha CCM kimeanza bado muda kitambo kitakuwa chama cha upinzani kuanzia urais hadi wenyeviti wa mitaa
Quote

-2 #45 Mtanzania mwema 2011-04-10 16:02 Nafikiri wewe na mwenzio mnamtafuta Mungu maneno!!Kwa nini mnamchezea Mwenyezi Mungu namna hiyo??Hebu jichunguzeni matendo yenu kwanza kabla hamjaanza kumuomba Mungu kuwaadhibu wengine kwani adhabu yaweza kuwarudia ninyi tena mkashangaa!Quoting Shahid:
Quoting mim:
Eehhe!!!! Mwanyezi Mungu, Muumba mbingu na Nchi, tunaomba utusaidie hiki chama kife ili wanao tupate salimika, tunapiga magoti mbele yako Baba, nyosha mkono wako kukimaliza hichi chama ili nasi tupate kupona, Amen!!​

Yarabi Tunusuru na shetani huyo hapo juu na anaowaombea,nch i hii imejaa mashetani ambao wanagombea uongozi wa nchi hii, Yaarabi tunusuru na viongozi wasio waadilifu,wazin ifu na wauza unga. Yaarabi tunusuru na viongozi wenye ukabila,Yaarabi tunusuru na hao majambazi wanaoitaka ikulu kwa udi na uvumba,tuondele e jinamizi la ccm lakini usituwekee wachaga katika uongozi wa juu tutaangamia,Yaa rabi muangamize Dr Slaa kwa kuchukua mke wa mnyonge kwa nguvu ya pesa wanazodhulumu walalahoi wa nchi,Yaarabi tunusuru na huyu aliyeshindwa kutii hata amri ya dini yake. Yaarabi iokoe nchii na viongozi wenye tamaa na utuwekee waadilifu.....Aaamin Raaabilaalamin​
Quote

+1 #44 walimu 2011-04-10 15:58 CCM IMEFARIKI DUNIA
Quote

0 #43 talentbrain 2011-04-10 15:52 Quoting Shahid:
Quoting mim:
Eehhe!!!! Mwanyezi Mungu, Muumba mbingu na Nchi, tunaomba utusaidie hiki chama kife ili wanao tupate salimika, tunapiga magoti mbele yako Baba, nyosha mkono wako kukimaliza hichi chama ili nasi tupate kupona, Amen!!​

Yarabi Tunusuru na shetani huyo hapo juu na anaowaombea,nch i hii imejaa mashetani ambao wanagombea uongozi wa nchi hii, Yaarabi tunusuru na viongozi wasio waadilifu,wazin ifu na wauza unga. Yaarabi tunusuru na viongozi wenye ukabila,Yaarabi tunusuru na hao majambazi wanaoitaka ikulu kwa udi na uvumba,tuondele e jinamizi la ccm lakini usituwekee wachaga katika uongozi wa juu tutaangamia,Yaa rabi muangamize Dr Slaa kwa kuchukua mke wa mnyonge kwa nguvu ya pesa wanazodhulumu walalahoi wa nchi,Yaarabi tunusuru na huyu aliyeshindwa kutii hata amri ya dini yake. Yaarabi iokoe nchii na viongozi wenye tamaa na utuwekee waadilifu.....Aaamin Raaabilaalamin​
Udini mtupu Rashidi, hayo yote unayoyasema tumeyazoea. Acha upopooooo wewe kama huna la kusema kaa kimya. Tunakushauri urudi kwenu bush ukakomae na kilimo wakati huna sokola kuuza, maisha magumu ila wewe unachekelea. Ama hakika Rashidi una mgando wa mawazo.
Quote

+3 #42 joseph stanslaus 2011-04-10 15:49 jk hata baba wa taifa alihofia hatma ya chama mikononi mwako,si kwa kukuona wewe mchanga tu bali pia aliona nyoyo za ubinafsi na tamaa na kukosa utaifa ndani yenu,mnashangaz a kujinunulia magari mkiacha barabara mbovu,hospitali bila ambulanse,shule bila maabara,kwa kipaumbele cha matumbo yenu na wanawenu,kubali kwamba kisichostahili kuishi sharti kife kwa manufaa ya viishivyo,ni wakati wa watanzania wakweli kwa tanzania yenye mwelekeo,wote wana haki ya kuwaongoza vema si nyinyi tena
Quote

1234
 
na kwa makundi yaliyopo sasa katiba haipitishwi kabisa! Ha ha ha ha hasira hasara
 
mpaka sasa hivi habari nilizonazo ni kwamba hakuna uchaguzi wowote uliofanyika kwa hiyo hayo ya wakina mkama bado rumours tu
Nimesikia BBC kuwa eti katibu wa ccm bado hajajulikana.
 
Nina bahati ya kumfahamu Mukama binafsi wakati wakiwa Mkuregenzi wa jiji. Ni mtu mzuri sana na tena ana akili sana, ila linapokuja swala la kutafuta pesa kwa njia yoyote hata ya kifisadi, ndugu huyu huwa habaki nyuma hata siku moja. Inawezekana kwa vile ni mtu mwenye akili sana akatambua kuwa vita dhidi ya ufisadi ndiyo iliyomueweka pale, na hivyo akashidana na vishawishi vya ufisadi. Vinginevyo inawezekana CCM imeondoa a Rock na kuweka a Hard Place.
 
Huyo Mukama ni mropokaji Makamba sifuri.Mukama siyo msomaji, hajengi hoja bali huongea kwa jazba kulazimisha anachotaka, hashauriki. Hata celina ana akili kuliko. Nyie subirini aanze kuparamia katiba mpya muone
 
Fumua fumua CCM, Makamba na Sekretarieti wajiuzulu Send to a friend Sunday, 10 April 2011 06:39 0diggsdigg

ccmmakamba.jpg
Waandishi wetu, Dodoma
MABADILIKO makubwa ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) yamefanyika baada ya wajumbe wa sekretarieti ya chama hicho kujiuzulu.
Kutokana na hali hiyo, huenda Kamati Kuu nayo ikajiuzulu na kubakiwa na Mwenyekiti, Rais Jakaya Kikwete, Spika wa Bunge, Anna Makinda ambao wanaingia kwa nafasi zao na John Malecela ambaye ni Mjumbe wa Kudumu.

Habari zilizopatikana kutoka ndani ya kikao cha Kamati Kuu ya CCM iliyokutana mjini Dodoma jana, zinaeleza kuwa hatua hiyo inatokana na mgawanyiko uliokikumba chama hicho.

Hatua hiyo ya kujiuzulu kwa wajumbe wa nafasi nyeti ya chama hicho, inakuja miezi mwili baada ya Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Rais Jakaya Kikwete kueleza wazi kuwa chama kinahitaji kujivua gamba ili kiweze kurejesha heshima yake.

Akihutubia kilele cha maadhimisho ya siku ya kuzaliwa CCM, mjini Dodoma Februari 5 mwaka huu, Rais Kikwete alisema chama hicho kinahitaji mabadiliko makubwa kiweze kurejesha hadhi yake.

Wajumbe waliojiuzulu ni Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba ambaye ni mwenyekiti, manaibu makatibu wakuu wa CCM Bara na Visiwani, George Mkuchika na Saleh Ramadhan Feruzi na Katibu wa Itikadi na Uenezi, John Chiligati.

Wengine ni Katibu wa Uchumi na Fedha, Amos Makala, Katibu wa Mipango, Kidawa Saleh na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mambo ya Nje, Bernard Membe.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo gazeti hili imezipata jana usiku zilieleza kwamba Makamba aliwasilisha barua yake kwa kuiweka kwenye meza ya mwenyekiti kwenye ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.

Taarifa hizo zinasema kuwa baada ya kuwasilisha barua hiyo, Makamba aliomba ruhusa ya kuondoka kwa maelezo kuwa amepata msiba nyumbani kwao Tanga.

Hata hivyo, wajumbe wa kamati hiyo walikataa kutokana na umuhimu wake kwenye kikao hicho, hivyo wakamweleza kuwa atume mwakilishi kwenye msiba.

Habari zaidi zinasema, Makamba amemtuma mwanaye, Januari Makamba ambaye ni mbunge wa Bumbuli mkoani Tanga kwenda kumwakilisha kwenye msiba huo.

Awali wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CC-CCM), waliendelea kuvutana na kusababisha kuahirishwa kwa Mkutano wa Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho kilichokuwa kianze jana.

Kikao cha CC ambacho kilianza juzi jioni kilitarajiwa kumalizika usiku wa siku hiyo na jana kilikuwa kifanyike kikao cha NEC, ajenda kuu ikiwa ni kujadili tathmini ya uchaguzi mkuu uliopita.

Hata hivyo, Kamati Kuu iliyoanza kikao saa 10 jioni juzi, iliahirisha kikao chake saa 1:00 usiku na kurejea tena saa 3:00 hadi saa 5:00 usiku, bila kumaliza kupanga ajenda za NEC.

Wajumbe wa NEC walianza kukusanyika asubuhi jana katika Makao Makuu ya CCM, baadaye walitakiwa kurudi tena saa 7:00 mchana, lakini waliporejea walitakiwa kurudi tena saa 10:00 jioni, pia walitakiwa kurejea leo saa 3:00 asubuhi.

Kuahirishwa kwa kikao cha NEC, kulidaiwa kuwa kumetokana na CC kutomaliza kuandaa ajenda za kikao hicho.

Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho, zilidai kuwa hatua ya kuahirishwa kwa kikao hicho ilitokana na kuwepo kwa mvutano mkali kati ya wajumbe wa CC, wakitaka baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wajiuzulu ili kukinusuru chama kutokana na tuhuma mbalimbali kinazobebeshwa na kuharibu taswira yake.

Kundi hilo linadai pia kuwa kama wajumbe hao watatoswa watakuwa wamewanyima Chadema ajenda mbele ya wananchi, lakini kundi jingine linalowaunga mkono likipinga mapendekezo hayo.

Baadhi ya wenyeviti wa mikoa wa CCM, wanaunga mkono kundi hilo la watuhumiwa lilikuwa likikutana kwenye hoteli moja, wakihaha kuhakikisha ajenda hiyo inazimwa.

Katika mkutano huo, inadaiwa ajenda nyingine iliyokuwa na mvutano zaidi ni ya Muswada wa Sheria ya Kubadilisha Katiba wa 2011 ambapo katika kikao hicho Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Fredrick Werema pia alihudhuria.

Wanaotajwa kurithi nafasi ya Makamba ni, Balozi wa Tanzania nchini Russia, Jaka Mwambi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi na Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk Emmanuel Nchimbi.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Kanali Abdulrahman Kinana, ambaye anadaiwa anaweza kukinusuru chama hicho na mgawanyiko uliopo, anadaiwa kukataa nafasi hiyo baada ya kuombwa na mwenyekiti. Hata hivyo, taarifa zinaeleza kuwa amekubali kuwa Naibu Katibu Mkuu.

Mwingine anayetajwa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Steven Wassira, lakini anahukumiwa na historia yake ya kuhama chama hicho kwenda NCCR-Mageuzi mwaka 1995.

Kikao hicho kinadaiwa pia kujadili matamshi ya kejeli na matusi yaliyotolewa na Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) dhidi ya Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, kuwa yanakigharimu chama.

“Kama kuna kitu kimetugharimu kichama ni kauli za UVCCM, huwezi ukabeza mchango wa Frederick Sumaye. Huyu amelitumikia taifa na chama kwa muda wa mrefu,” kilisema chanzo chetu.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati, alisema ngoma bado ni nzito na kuwataka wajumbe wa Nec kuwapo kwa ajili ya kikao leo saa 5:00 asubuhi.

Hata hivyo, Chiligati alikataa kutaja ajenda zilizokuwa zikijadiliwa kupelekwa NEC na kuahidi kuzitaja kwa waandishi wa habari leo saa 3:00 asubuhi. source
Fumua fumua CCM, Makamba na Sekretarieti wajiuzulu
 
Kuchaguliwa kwa Nape liwe Fundisho kwa vijana wenzake wanaotumiwa na mafisadi kama yule msomari. Simamia ukweli na ukweli utakuponya. Wao walibenk kwa LA. kiko wapi. Nape alijitahidi kujiepusha na mafisadi mwisho wa siku analia kivulini. Vijana wadogo kama msomari kuanza kuwa groomed kuwa mafisadi inasikitisha. Anyway for the sake of our country hii timu mpya iangamize mafisadi wote vijana na wazee! I am for change regardless inaletwa na Chadema au CCM. Hatuhitaji tu sura mpya ila tunataka mtusafishie hii nchi jamani.
 
Kuna kipindi alikuwa katibu mkuu wizara ya Afya

Jamaa kwa sasa ndio Mwenyekiti wa Bodi ya TSN inayosimamia magazeti ya Daily News na Habari Leo. Kama ni kweli ameondoka bila kumudu kuyapa magazeti hayo Mhariri Mtendaji nafasi iliyoibua utata sana. Hii inaweza kuhesabiwa kuwa moja ya failures zake za kiutendaji za kukumbukwa. Otherwise kisiasa simjui. Nampa nafuu ya mashaka.
 
Pamoja na baadhi ya members wa JF kutarajia Mkama angeteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mafisadi mie nilihofia ungeweza kuteuliwa wewe maana nasikia hata Uenyekiti wa Kamati ulimwomba JK akusaidie baada ya kuona chama unachoigiza kuwa mwanachama wake kinafitiniwa. Lini unahamia CCM rasmi?

Alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na sasa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TSN
 
Mukama katulia sana alikuwa utendaji wake si wa kubwabwaja ni msomi anapenda kujibu hoja alikuwa JIJI THEN katibu mkuu afya then katibu mkuu maji mpaka akastaafu.akateuliwa na rais kuwa mkurugenzi wa bodi habari.na amehusika sana kutunga ilani ya ccm 2010-2015 hivyo watu wenye bongo zao wanarudi chamani pia ni mtu wa system.

Ama kweli sasa nimeamini ziro ukiongeza moja inakuwa ngapi vile? I told you somebody has made it a point to be a new Nyerere in this country wait and see plan A inakaribia ku tick, acha niwasome tena enhe!
 
Back
Top Bottom