Mambo mazito CCM Dodoma: Wajivua gamba?

Mambo mazito CCM Dodoma: Wajivua gamba?

Kuna kipindi alikuwa mkuu wa Wilaya ya Dodoma vijijini (Hahi kwa sasa)
 
Mie sioni na sijui kwanini EL aliekubali kujiuzulu bado mna mfuata fuata, kuna mijizi mingi bado imo humo ndani wala hamuwasemi!!!
Edward Lowassa ni BORA mara millioni Trillioni zaidi ya wengi waliomo CCM, mtabisha lakini ukweli mnaujua na upo wazi.

EL was getting things DONE.... Mnataka kuwa na viongozi legelege wanaolalamika kama sisi wananchi tulio vijijini?
Mnataka viongozi wasio na MENO?, EL tayari ana hela kaiba au hakuiba haijalishi...ataingia kuchapa kazi ndo alichobakisha.

Jaribuni ku focus kwenye real issues zilizopo na sio kumwandama asiyekuwepo hata kwenye system!
 
....ccm wamemwaga maji na mtoto ndani ya besen........


 
Aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Jiji la DSM......Mtu wa madili pia

Ni rafiki mkubwa wa familia ya Kingunge Ngombale-Mwiru. Akiwa Jiji, bila shaka ndiye aliyesaidia familia hiyo ikapata miradi ya kukusanya ushuru katika Kituo cha Mabasi Ubungo na Mradi wa Maegesho ya magari Dar es Salaam.
 
Ninavyomfahamu kwa uchache Mukama ni Political Scientist. Amewahi kuwa tutor chuo cha Kivukoni, Mkurugenzi wa Jiji la DSM, Naibu Katibu Mkuu Tamisemi, Katibu Mkuu Afya, Katibu Mkuu-Maji na baada ya kustaafu aliteuliwa na Rais kuwa Mwenyekiti wa Bodi wa TSN. Pia ni Strategist wa CCM.
CCM hawaangalii sifa hizo za political scientist wanaangalia nani mwenye mdomo mkubwa wa kupambana na wapinzani wao wakuu CDM.
 
anything for ukatibu mkuu is better than makamba hata wangeteuua meza au kiti!ila sasa meghji hata kama ni gender sasa imezidi,they cant know kama kuna anayeweza zaidi yake kama hawapewi nafasi wengine...
 

Haya kisha iva:-


WILSON MUKAMA KATIBU MKUU CCM,
NAPE MOSES NNAUYE KATIBU ITIKADI NA UENEZI,
ZAKIA MEGHJI KATIBU FEDHA NA UCHUMI,
Dr REHEMA NCHIMBI KATIBU ORGANISATION
 
Kama haya ni ya kweli, basi CCM haina shukrani. Makamba kawapigania siku zote! Alikubali kupakwa matope ya chama akabaki nayo ili chama kinusurike! Eti kaondoka kirahisi hivyo? Makamba usijali Mungu atakulipia!
 
Inawezekana Mukama akawa hana makuu kwani namfahamu Binti yake mmoja ni mfanyakazi tu wa kawaida manispaa. Kwa vyeo alivyowahi shika baba yake angekuwa Makamba type bintiye angekuwa mkurugenzi mahali fulani. Kwa kifupi Mukama hana makuu na si selfish. Ila issue ni kwamba can he change m=the mind sets of CCM. Anaweza kubadili tabia za kifisadi za wana CCM?

Mapema sana kuzungumzia maadili ya mteule yeyote aliyewahi kuwa mtendaji ndani ya CCM, Hapa tuzungumzie qualifications na uwezo wa kusoma alama za nyakati ikiwamo kuhakikisha kuwa anamshawishi mwenyekiti wake kuacha kuwalinda wale wote walioliibia Taifa hili kwa kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria bila kujali majina ni kina nani. Otherwise itakuwa ni yaleyale ya kumchukua kunguru mweupe na kumfungia kwenye boksi lenye uchafu ukitarajia kwa kufanya hivyo box nalo litakuwa jeupe.
 
Hahahhhaaa, kweli wamejivua gamba.... ila nyoka ni yule yule!!! niliwashauri sana badala ya kuvua gamba ambalo najua hawanalo....wangekata govi! ambalo lingewaletea heshima kwa jamii sasa wameruka mkojo na kukanyaga mavi!!!!!
 
Kama haya ni ya kweli, basi CCM haina shukrani. Makamba kawapigania siku zote! Alikubali kupakwa matope ya chama akabaki nayo ili chama kinusurike! Eti kaondoka kirahisi hivyo? Makamba usijali Mungu atakulipia!
Kawapigania kuingia madarakani leo wanatupa jongoo na mti wake, lakini ndiyo siasa usijali baba yangu Makamba.
 
sasa na sisiem B aka KAFU nao wafanye mabadiliko .... yaani professor pumba ni mwenyekiti wa sisiem B Miaka mingi sasa na katibu wake
 
Habebwi na mtu, huombwa na kuangukiwa, ni mchapa kazi sana, na kichwa, wacha. Waulize wanaomjuwa. Si mwanamke wa kawaida.
Wapi bwana usitake kumpa misifa ya bure tu, kwa nini alijiuzuru uwazi wa fedha? hana lolote zaidi ya kubebwa tu!
 
Huyu mukama ni fisadi hakuna mfano. Alifanya ufisadi mkubwa sana alipokuwa katibu mkuu wizara ya afya kabla hajastaafu. Aliacha accounts systems in big shame! Kwa hiyo hapo amefika na mafisadi wajipange mkao wa kula zaidi
 
Alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na sasa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TSN
Teh teh kumbe kweli na jk ulikuwa kimkakati tumekutafuta sana kwenye kongamano udom
Watu wakasema unashauriana na jk kuokoa jahazi nikajua wanakuonea wivu kama kawaida yao .teh teh uko kiccm zaidi .
 
Back
Top Bottom