Mama Samia : Utafiti unaonesha Zaidi ya nusu ya Tanzania wenye umri wa kuoa au kuolewa hawajaingia kwenye ndoa . Je sababu yako ni nini ?

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
8,822
33,527
Ameyasema hayo leo Jumapili, Januari 21, 2024 alipokuwa akizungumza kwenye Ibada Maalumu ya kumuingiza kazini Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Alex Malasusa iliyofanyika katika viwanja vya Kanisa Kuu la Azania Front, Dayosisi ya Mashariki na Pwani.

“Kwa wakazi wa mijini ni wastani wa asilimia 61 na vijini 55.5 na kwamba wanaofanikiwa kuingia kwenye ndoa kuna changamoto mbalimbali zinazosababisha migogoro ya ndoa, kwa mfano mwaka 2022/23 kulikuwa na mashauri 39,571 ya migogoro ya ndoa na katika nusu ya kwanza ya 2023/24 tayari tumeshapokea mashauri 28,773

nawaza tu ndani ya mwaka mmoja mahakamani kuna kesi za talaka za ndoa 39,571

Nusu mwaka kuna kesi za divorce za ndoa 28773

Taasisi ya Ndoa inaelekea wapi ?
 
Nime give up kwenye swala la kuoa na Sababu ni wadada kuwa waovu. Wametanguliza maslahi ya kifedha kuliko nia ya kuolewa.

Wiki iliyopita Nilimtongoza mwanamke asubuhi alafu jioni akanitumia orodha mahitaji ya vitu vyenye thamani ya laki sita bila aibu! Jambo hili limenitokea kwa zaidi ya mara moja.

Kwa sasa nimejikita kwenye kuimarisha ustawi wangu binafsi. Mambo ya ndoa hapana aisee
 
Nime give up kwenye swala la kuoa na Sababu ni wadada kuwa waovu. Wametanguliza maslahi ya kifedha kuliko nia ya kuolewa...
Tatizo lenu mnataka kuoa wanawake full package yani awe mzuri wa sura na umbo, mcha mungu, mpole, mvumilivu, mwenye akili ya maisha, anayejua kufanya kazi za nyumbani pamoja na kulea mume nk, mnataka wanawake wakamilifu ili hali ninyi siyo wakamilifu na huwa hamyaoni maovu yenu kutwa kusema ya wanawake tu
 
Vijana wa kiume wanaamini kwenye kujipanga kimaisha awe na vitu ambavyo vitawavutia wanawake. Umri nao hauwasubiri

Wanawake vijana wanaishi kwa ndoto kuwa atatokea mwenye kibunda huku wenye nia ya kuwaoa wakiwakaataa. Wanajikuta umri unaenda wanakuwa wasimbe

Vijana wengi wa kiume hawana kazi au vipato vya uhakika bado wanajitafuta
 
Takwimu zinaonesha watanzania wengi wanaishi kwa kipato cha chini ya dola moja kwa siku, kwa kipato hicho unaoa ili iweje?
Kama kweli anataka watu waoane kwa wingi basi ajikite zaidi katika kuboresha kipato cha wananchi.
 
Ameyasema hayo leo Jumapili, Januari 21, 2024 alipokuwa akizungumza kwenye Ibada Maalumu ya kumuingiza kazini Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Alex Malasusa iliyofanyika katika viwanja vya Kanisa Kuu la Azania Front, Dayosisi ya Mashariki na Pwani.

“Kwa wakazi wa mijini ni wastani wa asilimia 61 na vijini 55.5 na kwamba wanaofanikiwa kuingia kwenye ndoa kuna changamoto mbalimbali zinazosababisha migogoro ya ndoa, kwa mfano mwaka 2022/23 kulikuwa na mashauri 39,571 ya migogoro ya ndoa na katika nusu ya kwanza ya 2023/24 tayari tumeshapokea mashauri 28,773

nawaza tu ndani ya mwaka mmoja mahakamani kuna kesi za talaka za ndoa 39,571

Nusu mwaka kuna kesi za divorce za ndoa 28773

View attachment 2879174
Taasisi ya Ndoa inaelekea wapi ?
Huyu mama, ni mpuuzi sana, ndoa sio tatizo la vijana! Tatizo kubwa ni ajira! Kipato duni, elimu duni.
Anaji tripisha, kuhamisha mjadala! So fucking pathetic
 
Acheni ku kocmplicate Mambo! Tafuta ka mwalimu weka ndani, wapo wengi tu, nenda kwenye halamashauri
 
Back
Top Bottom