Uelewa mdogo wa jamii juu ya Uzazi wa Mpango, ni chanzo cha ndoa na mimba nyingi za utotoni

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
304
518
Ukosefu wa Elimu ya Uzazi wa Mpango katika Jamii nyingi hasa Wazazi, hupelekea watoto wao kupata mimba za Utotoni ambazo nyingi husababisha ndoa za utotoni.

Vijana wengi hawana Uelewa juu ya mabadiliko yao ya kimwili yanayoambatana na kuanza mahusiano ya kimapenzi kwenye Umri mdogo bila kuwa na Elimu ya Uzazi wa Mpango jambo ambalo husababisha mimba zisizotarajiwa pamoja na ndoa za utotoni.

Mara nyingi Watoto wanapopata mimba huozeshwa kwa nguvu na Wazazi wao kwa kile wanachodai ni kupndoa aibu kwenye Familia ya mtoto kuzalia nyumbani.

Wazazi wangekuwa na uelewa sahihi, juu ya umuhimuwa wa Elimu ya Uzazi wa Mpango kwa Watoto wao, ingepungunza mimba za Utotoni na na Ndoa za Utotoni.

Mimba na Ndoa za utotoni zimezima ndoto za Watoto wengi. Kwani Myoto akishaolewa na kuoa utotoni, kinazima kabisa ndoto zake za maisha.

Kuhusu madhara ya ndoto za Utotoni, Daktari anaelezea kwa Mapana

=====

Ndoa ya utotoni’ ni muungano rasmi au usio rasmi ambao angalau mmoja kati ya wanandoa ni chini ya umri wa miaka 18.

Dkt. Bernard Kivuma ambaye ni Mtafiti kutoka Taasisi ya Afya ya Ifakara akiwa anahusika na Afya ya Uzazi, Magonjwa ya Kuambukiza, UKIMWI na Kifua Kikuu, anaelezea changamoto mbalimbali ambazo zinazohusu masuala ya Afya ya Uzazi hasa kwa wale wanaokumbana na hali hiyo wakiwa na umri chini ya miaka 18 kutokana na Ukosefu wa Elimu ya Uzazi wa Mpango.

Dkt Kivuma anaanza kwa kuelezea kitaalam kuhusu changamoto za Ndoa za Utotoni hasa kwa wasichana wenye umri chini ya miaka 18
IMG_20230712_144231_022.jpg

Dkt. Bernard Kivuma

Anasema: “Kuna matukio kadhaa yanayohusisha Ndoa za Utotoni Nchini, kwanza tunatakiwa kutambua kuwa Ndoa za Utotoni ni zile ambazo tunatafsiri kuwa zinawahusisha wahusika wenye chini ya umri wa miaka 18 ambazo nyingi ni matokea ya Mimba za Utotoni zinazotokana na Wahusika kuyokuwa na Elimu ya Uzazi wa Mpango.

“Kitaalam msichana chini ya 18 anaweza kupata Mimba, na ikitokea hivyo mara nyingi huwa hali hiyo inaambatana na changamoto mbalimbali kabla, wakati na hata baada ya kujifungua.

Wenye umri huo wanapokuwa na ujauzito huwa wanakabiliwa na wakati mgumu wa malezi kutokana na kutokuwa na uelewa mzuri wa kipindi cha ujauzito na jinsi ya kuzifikia Huduma za Mama na Mtoto.”

Ndoa za Utotoni zinachangia ukatili.

Daktari anasema mara nyingi Ndoa za Utotoni zinachangia uwepo wa matukio ya ukatili wa kijinsia kwa Wanandoa, tafiti mbalimbali zinaonesha hali hiyo zinatokea kwa kiwango cha 15-60% Nchini.

Waathirika wakubwa katika ukatili huo ni Wanawake ambao unakuta wanalazimika kuvumilia kwa kuwa hawajui vitu vingi pia wanaingia katika ulimwengu ambao wanakuwa hawajawa tayari kisaikolojia na kimwili.

Ukatili unapoendelea unaweza kusababisha madhara katika Afya ya Akili na mwili kwa jumla.”

Ushauri kwa Serikali
Nashauri Serikali iendelee kujikita katika kumsaidia mtoto wa kike kwa njia mbalimbali kutoa Eimu ya Uzazi wa mpango. Pia Serikali iendelee kudhibiti Ndoa za Utoto kwa ajili ya kuwasaidia waathirika.”

Sheria ya Ndoa
Andiko la Mwanasheria Frolian Mwesiga Matungwa ameandika kupitia JamiiForums akielezea Sheria ya Ndoa na kushauri mabadiliko kutokana na mkanganyiko uliopo.

SoC03 - Mabadiliko ya haraka yanahitajika katika sheria ya ndoa

Anasema Sheria ya Ndoa Sura ya 29 ya Mwaka 1971 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2019 inaruhusu ndoa za utotoni; Kifungu cha 13 na 17 vinachochea uwepo wa ndoa za utotoni nchini Tanzania kwa kuruhusu mtoto wa kike kuolewa akiwa na umri wa miaka 15.

“Mahakama ya Rufani katika kesi ya Loveness Mudzuru na wengine dhidi ya Waziri wa Sheria na wengine ya mwaka 2015 Mahakama ilisema kwamba ndoa za utotoni zinasababisha Wasichana kutotimiza ndoto zao hasa za kielimu, hivyo Serikali haina budi kufanya marekebisho ya haraka ya sheria hiyo ili kuwanusuru watoto wa kike wasipoteze haki yao.

Lakini Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009 ambayo inamwelezea Mtoto kama mtu mwenye umri chini ya miaka 18, katika Mahakama ya Rufani katika kesi ya Rebeca Gyumi dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya mwaka 2016 mahakama ilitoa amri ya kwamba kifungu cha 13 na 17 cha Sheria ya Ndoa kinakinzana na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, hivyo inatakiwa kufanyiwa marekebisho.

“Jitihada mahususi zinatakiwa kufanyika kuanzia ngazi ya mtu mmoja mmoja, jamii, viongozi wa dini pamoja na Serikali kwa jumla kwa kutoa ushirikiano katika kupambana, kukemea na kutokomeza vitendo ambavyo vinachochea ukiukwaji wa sheria kama vile ndoa za utotoni, unyanyasaji.nk.

“Serikali haina budi kufanya jitihada ya haraka katika kufanya marekebisho na maboresho ya Sheria ya Ndoa kwa kupitia upya sehemu zenye mapungufu kwa kuchukua hatua za kuvifuta vifungu ili kuendana na kasi ya maendeleo nchini.”
Screenshot_20230712-152328.png

Tanzania ina ndoa za utotoni 779,000.Huku ikishika namba 11 duniani kutokana na takwimu za UNICEF.​


Kwa mujibu wa takwimu kutoka @UNICEFTanzania Tanzania hadi kufikia mwaka 2023, inashika nafasi ya 11 Duniani kuwa na ndoa za utotoni takribani 779,000

Hii ni kwa sababu 31% ya wasichana wanaolewa kabla ya kufikisha miaka 18 na 5% kabla ya kufikisha miaka 15,Kama taifa njia moja wapo ya kukomesha ndoa
za utotoni kwa kutoa elimu kwa jamii kuhusu madhara yatokanayo na ndoa za utotoni ikiwemo kukosa fursa ya kupata elimu, Lakini pia kuhakikisha bunge letu linaharakisha kufanya mabadiliko ya sheria ya ndoa ya mwaka 1971 hasa kifungu cha 13 na 17.
 
Back
Top Bottom