Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Charles Kitwanga, amewaeleza wabunge kuwa, mmiliki wa mtandao wetu wa jamii forum anaweza kuwa Mtanzania au si Mtanzania.
Ameyasema hayo bungeni mjini Dodoma wakati anajibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Getrude Lwakatare (CCM).
Mbunge huyo amedai kuwa, Mtandao huo umekuwa ukisambaza habari za uongo kwa watu mbalimbali na haujachukuliwa hatua hivyo alitaka kumfahamu mmiliki wa mtandao huo.
Kitwanga amesema, uanzishwaji wa tovuti za kijamii haulazimishi mtu kujisajili wala kujitambulisha , na huanzishwa na mtu yeyote popote duniani.
"Kutokana na asili na miundo ya tovuti za kijamii, mamlaka haisajili wala kutoa leseni kwa tovuti hizo, kimsingi maudhui yanayoadikwa katika tovuti hizo za kijamii ni maoni binafsi ya watu yasiyoangaliwa iwapo ni ya kweli au la" amesema Kitwanga.
Baada ya Mbunge wa Viti Maalum, Hilda Ngoye (CCM) kuuliza swali la nyongeza, wakati Kitwanga anajiandaa kumjibu, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, alimtaka kiongozi huyo wa Serikali, ajibu hasa swali kuhusu ' Jamii Forum na matatizo yake makubwa'
Ngoye amedai kuwa, baadhi ya mambo yanayoandikwa kwenye mtandao wa Jamii Forum yana madhara katika jamii yakiwemo matusi ya nguoni na ni kinyume cha utamaduni wa Mtanzania.
Aliuliza kama Serikali ipo tayari kuwasilisha bungeni muswada , Bunge litunge sheria ili mtandao huo uache kuandika mambo ya maudhi na uchochezi.
Alitaka pia kufahamu kama Serikali ipo tayari kuwasilisha bungeni muswada ili Bunge litunge sheria itakayozuia watoto kusoma ‘mambo machafu' kwenye ‘internet café' vikiwemo vitendo vya ngono.
Kitwanga amesema, suala la kudhiti mitandao ya kijamii litakuwa kwenye Muswada wa Sheria ya Habari.
Amesema, suala la maadili ya watoto ni jukumu la wazazi, na kwamba ndiyo wanaowapa fedha za kwenda ‘Internet café'.
Amesema, kutokana na kukua kwa teknolojia ya mawasiliano, kuna namna nyingi zinazowawezesha watoto kuona ‘mambo yasiyofaa' zikiwemo simu za mkononi, ipad, na laptops.
Amesema ni wajibu wa wazazi kuhakikisha kuwa watoto wao wanakua kwa mujibu wa maadili ya taifa.
I have picked three things from HildaNaibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Charles Kitwanga, amewaeleza wabunge kuwa, mmiliki wa mtandao wetu wa jamii forum anaweza kuwa Mtanzania au si Mtanzania.
Ameyasema hayo bungeni mjini Dodoma wakati anajibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Getrude Lwakatare (CCM).
Mbunge huyo amedai kuwa, Mtandao huo umekuwa ukisambaza habari za uongo kwa watu mbalimbali na haujachukuliwa hatua hivyo alitaka kumfahamu mmiliki wa mtandao huo.
Kitwanga amesema, uanzishwaji wa tovuti za kijamii haulazimishi mtu kujisajili wala kujitambulisha , na huanzishwa na mtu yeyote popote duniani.
"Kutokana na asili na miundo ya tovuti za kijamii, mamlaka haisajili wala kutoa leseni kwa tovuti hizo, kimsingi maudhui yanayoadikwa katika tovuti hizo za kijamii ni maoni binafsi ya watu yasiyoangaliwa iwapo ni ya kweli au la" amesema Kitwanga.
Baada ya Mbunge wa Viti Maalum, Hilda Ngoye (CCM) kuuliza swali la nyongeza, wakati Kitwanga anajiandaa kumjibu, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, alimtaka kiongozi huyo wa Serikali, ajibu hasa swali kuhusu ' Jamii Forum na matatizo yake makubwa'
Ngoye amedai kuwa, baadhi ya mambo yanayoandikwa kwenye mtandao wa Jamii Forum yana madhara katika jamii yakiwemo matusi ya nguoni na ni kinyume cha utamaduni wa Mtanzania.
Aliuliza kama Serikali ipo tayari kuwasilisha bungeni muswada , Bunge litunge sheria ili mtandao huo uache kuandika mambo ya maudhi na uchochezi.
Alitaka pia kufahamu kama Serikali ipo tayari kuwasilisha bungeni muswada ili Bunge litunge sheria itakayozuia watoto kusoma ‘mambo machafu' kwenye ‘internet café' vikiwemo vitendo vya ngono.
Kitwanga amesema, suala la kudhiti mitandao ya kijamii litakuwa kwenye Muswada wa Sheria ya Habari.
Amesema, suala la maadili ya watoto ni jukumu la wazazi, na kwamba ndiyo wanaowapa fedha za kwenda ‘Internet café'.
Amesema, kutokana na kukua kwa teknolojia ya mawasiliano, kuna namna nyingi zinazowawezesha watoto kuona ‘mambo yasiyofaa' zikiwemo simu za mkononi, ipad, na laptops.
Amesema ni wajibu wa wazazi kuhakikisha kuwa watoto wao wanakua kwa mujibu wa maadili ya taifa.
Mama rwakatare hivi anajua hata matumizi ya mtandao? Manake ukisema usajili blogs zote, mbona kutakucjhwa?
Ingekuwa imesajiliwa bongo wangeshaifungia, so owners wamecheza game safi.Kama kuna siku magamba watakua wamekosea step ni kufunga JF maana kitakochokuja kitakuwa moto zaidi ya JF.
Kiranga ini bora kumpenda shetani kuliko Hitler..kwani inawezekana existence ya shetani ni kama hoax tu na unaweza kukuta shetani ha exist.huyu jamaa inawezekana kweli hamjui wala hajasoma historia ya hitler vizuri.Unajua kila mara ninapoiangalia avatar yako nashangaa sana, najiuliza hivi huyu mtu kasoma "Mein Kampf"? Anamjua Hitler na nini Hitler kafanya?
Lakini always naamini katika freedom of expression na siamini katika censorship, kwa hiyo nakuacha tu.
Leo nakuja kuona anayempenda Hitler amshangaa ampendaye shetani.
JF has never failed me yet!
wameshindwa kujadili MGOMO WA MADAKTARI na hali mbaya ya uchumi WANAJADILI JF? Kweli magamba wamezeeka akili
Namimi nimeshangaa mchungaji aliyesahau hata biblia anayoihubiri kila siku. Kama yeye hana uozo wowote Mungu wa kweli atamlinda siku zote; Yeye asimamie tu ukweli; and (the truth will always set her free). Kwa mtindo huu wengi tumeanza ku-question imani yake .Ni ile thread ya yeye kuua kiwanda ndio imemwamsha nini???
Mama Mchungaji Wananchi bungeni hamtuzungumzii ndio mana tuko huku kufarijiana. Wewe tenda mema utasifiwa tu.
Na uoga wa nini?
kwa nini haitakiwi na Magambaz? Tutumie busara kutafakari ili tupate jibu inawezekana na sisi wana JF tuna matatizo. Lakini kweli sometimes baadhi yetu wanakwenda nje ya maudhui ya JF. Sasa kama utaanza kusema fulani mjinga, Kilaza, kubeza kitu kitu na mambo kama hayo hayo, kweli tunakuwa hatuko tena kwenye lengo la kukosoa, kuboresha, kushirikisha ili mwisho wa siku maendeleo kwa watanzania.
Mimi nahisi kama yeye ndo Faiza Foxy vile.