Mama Rwakatare aichongea JamiiForums

Mama Rwakatare aichongea JamiiForums

Nyie mnafanya mzaha na hawa watu wa Kiduku...si wazuri hata kidogo!
Hawakawii kumgeuka mtu, kufanya fitna na visasi kwa wingi!'
c8opI5t+2fwAAAABJRU5ErkJggg==
 
Huyo mama nae kumbe huwa anaingia JF kama guest sio?

huyo ana id kabisa. Kwa maelezo yake inaonekana ni mhudhuriaji mzuri wa lile jukwaa la mwisho ambalo ukiwa guest wala huwezi jua kama lipo
 
JF Founder/team ilienda bungeni mwaka jana kama uzee haujafuta kumbukumbu zangu, huyo Mh Mchungaji Dr Mama Rwakatare siku hiyo hakuwepo bungeni?

Alikua akiendesha ibada ya kwenda ulaya bila visa kwa waumini wake

ya kaisali awaachie wenyewe nae abaki na ya Mungu
 
kwa kweli sioni umuhimu wa viti maalumu
hata mbunge wa kawe alijua hilo ndio maana akaamua kujitoa viti maalumu akajiamini
akashinda,hawa wengine hawana ubavu ndio maana wanaibuka na kuzungumza mambo yasiyo ya msingi
huyu mama wasiwasi wake ni nn hadi atake chombo chetu kifungwe?? jibu moja kwa vile ameambiwa ukweli
na tumeibua mengi yaliyofichika kuhusu yeye, na bado mwiba utamchoma sana ndio maana nampenda shetani
huwa akitaka kukupata anakutia kwanza wasiwasi na mashaka na kukupoteza dira mwishoni anakuchanganya na utajisahau utafanya jambo litakalo kuumbua mbele za watu,yeye anabakia kupiga makofi kwa furaha..
long live JF. mwenye ile CD yenye sauti alosikika akipanga jambo na mchungaji mtikila ili wamwangamize kakobe huku akiwaahidi kwenda benki kuchukua hela za kuanza shughuli hebu aiweke hapa,nadhani atazimia kabisa.

Are you serious bro?
 
Huu ni mtandao kwa ajili yetu chadema kujadiliana mambo yetu,sasa hawa magamba vipi tena?
 
Inabidi atwambie na mmiliki wa kanisa la Mlima wa moto ni nani? Toka wapi? Pamoja na St.mary's schools. Pili waongee mambo ya busara yenye kujenga taifa sio kupingana na mabadiliko ya technologia.
 
Are you serious bro?

Unajua kila mara ninapoiangalia avatar yako nashangaa sana, najiuliza hivi huyu mtu kasoma "Mein Kampf"? Anamjua Hitler na nini Hitler kafanya?

Lakini always naamini katika freedom of expression na siamini katika censorship, kwa hiyo nakuacha tu.

Leo nakuja kuona anayempenda Hitler amshangaa ampendaye shetani.

JF has never failed me yet!
 
Mheshimiwa Naibu Spika, Jambo/Jamii Forum ni mtandao wa kijamii ambao haujasajiliwa Tanzania bali umesajiliwa nje ya nchi. Mmiliki wa mtandao huu wa kijamii anaweza kuwa Mtanzania au mwananchi yeyote ambaye siyo Mtanzania.

Kwa sababu tuna jibu la kutoka bungeni (kwa Naibu Spika) linalomtambua "mwananchi yeyote ambaye siyo Mtanzania".

Kuna swali la nyongeza kwa mheshimiwa Naibu Spika hapa.

"mwananchi yeyote asiye Mtanzania" ni mtu gani? Je anatambulika serikalini Tanzania kwamba yeye ni "mwananchi asiye Mtanzania" ?

Kuna tofauti gani kwa "mwananchi asiye Mtanzania" na "mtu asiye Mtanzania"?

Bora wengine tusiingie tu huko biungeni!!!!!
 
huyu tapeli ukweli umemwingia kama kawaida ukweli huwa unauma..... Kama ni mtumishi wa mungu kama anavyojinadi ya nini kujishuku?...... Si atuombee tuache hayo maovu aliyoyaona?.....
 
Getrude Lwakatare Kazi Yake ni nini bungeni? NAOMBA MWENYE CV YAKE A-Z, Including mambo ya mume wake na ndoa kwa ujumla.
Ndio wale wehu wanaopiga meza na kuitikia ndiooooo bila kujua wanachoshabikia. Anaacha kondoo wake mikocheni anakimbilia siasa bungeni
 
Hao wabunge wote sijaona walichofanyia wananchi tangu kuteuliwa/kuchaguliwa kwao.
Hawana mashiko kwa watanzania, zaidi huyo Rwakatare ambaye ametahifisha kiwanda cha mang'ula machine tools!

Ajipange kuwa mjasiliamari tu siasa haiwezi kwa sababu hana awasaidialo wananchi!
 


Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Charles Kitwanga, amewaeleza wabunge kuwa, mmiliki wa mtandao wetu wa jamii forum anaweza kuwa Mtanzania au si Mtanzania.

Ameyasema hayo bungeni mjini Dodoma wakati anajibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Getrude Lwakatare (CCM).

Mbunge huyo amedai kuwa, Mtandao huo umekuwa ukisambaza habari za uongo kwa watu mbalimbali na haujachukuliwa hatua hivyo alitaka kumfahamu mmiliki wa mtandao huo.

Kitwanga amesema, uanzishwaji wa tovuti za kijamii haulazimishi mtu kujisajili wala kujitambulisha , na huanzishwa na mtu yeyote popote duniani.

“Kutokana na asili na miundo ya tovuti za kijamii, mamlaka haisajili wala kutoa leseni kwa tovuti hizo, kimsingi maudhui yanayoadikwa katika tovuti hizo za kijamii ni maoni binafsi ya watu yasiyoangaliwa iwapo ni ya kweli au la” amesema Kitwanga.

Baada ya Mbunge wa Viti Maalum, Hilda Ngoye (CCM) kuuliza swali la nyongeza, wakati Kitwanga anajiandaa kumjibu, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, alimtaka kiongozi huyo wa Serikali, ajibu hasa swali kuhusu ‘ Jamii Forum na matatizo yake makubwa’

Ngoye amedai kuwa, baadhi ya mambo yanayoandikwa kwenye mtandao wa Jamii Forum yana madhara katika jamii yakiwemo matusi ya nguoni na ni kinyume cha utamaduni wa Mtanzania.

Aliuliza kama Serikali ipo tayari kuwasilisha bungeni muswada , Bunge litunge sheria ili mtandao huo uache kuandika mambo ya maudhi na uchochezi.

Alitaka pia kufahamu kama Serikali ipo tayari kuwasilisha bungeni muswada ili Bunge litunge sheria itakayozuia watoto kusoma ‘mambo machafu’ kwenye ‘internet café’ vikiwemo vitendo vya ngono.

Kitwanga amesema, suala la kudhiti mitandao ya kijamii litakuwa kwenye Muswada wa Sheria ya Habari.

Amesema, suala la maadili ya watoto ni jukumu la wazazi, na kwamba ndiyo wanaowapa fedha za kwenda ‘Internet café’.

Amesema, kutokana na kukua kwa teknolojia ya mawasiliano, kuna namna nyingi zinazowawezesha watoto kuona ‘mambo yasiyofaa’ zikiwemo simu za mkononi, ipad, na laptops.

Amesema ni wajibu wa wazazi kuhakikisha kuwa watoto wao wanakua kwa mujibu wa maadili ya taifa.
 
Kama anamtaka mwenye jf ni mimi wala asisumbue mawaziri kutaka kunijua .afanye hivi kama anaenda mang'ula kule alikochakachua kiwanda akifika moro pale njia panda ya kilosa akate kulia kuhelekea kilosa atapita ranchi ya mkata na kuvuka ile reli haende kidogo kama km 15 akimuona mmasai aulize tu wapi ? TWATWATWA Watamleta mpaka nyumbani aje nimfamishe mambo yavyoenda hapa jukwaani kisha anitoe pepo langu jf maana siwezi kuliacha kabisa
 
Huyu mama ni wa ajabu sana. Ameshindwa kumdhibiti mwanae shoga ataiweza JF?
Anafanya haya kufunika madudu yake binafsi yanayojulikana wazi kwa jamii, nitaweka wazi madudu haya wazi hivi karibuni.
 
Ma ccm yanatamani zile enzi za fikra za mwenyekiti zirudi, fanya mema uone kama utaandikwa vibaya!
 
imesajiliwa mbinguni pandeni juu mkazibe awatuwezi tupo juu kama tai ni kama aljazeera tv ukiripua doha tunarushia dubai
 
Back
Top Bottom