Mama Rwakatare aichongea JamiiForums

Mama Rwakatare aichongea JamiiForums

Kiranga ini bora kumpenda shetani kuliko Hitler..kwani inawezekana existence ya shetani ni kama hoax tu na unaweza kukuta shetani ha exist.huyu jamaa inawezekana kweli hamjui wala hajasoma historia ya hitler vizuri.
Mkuu, nimeipenda posting yako, FYI, kabla ya wazungu kupeleka dini uchagani,kuna wanaoamini kuwa mashetani ni watu.

Bob Marley aliweka uzito kwenye hoja aliposema most people look at the sky for almighty God, ila aliamini kuwa hata Mungu yulo pamoja nasi na si mawinguni or smewhere else.

Ndo maana Kiranga mwanasayansi anawashinda kwa hoja kwasababu haamini.
 
kweli wana jf wanaipenda jf yao'member wengi wa jf wana uchungu na nchi yao'najua jf ina watu wa aina mbalimbali'matajiri'maskini'na wenye uwezo wa kawaida'lakini wote hao wana nia nzuri na taifa hili'matajiri walioko hapa ujue walipata hela kihalali'hongera jf na wana jf wote'nimesoma comment zote'jf is family!
 
Nadhani Naibu Waziri amejibu vyema na kwa werevu mkubwa. Wanataka kufanya nini na blog za watu? Mchambuzi kaeleza vizuri pia. Kazi yao kubwa ni kukanusha kwa bandiko ambazo zitaonekana za uongo na si kuwaza kufunga JF. Hayo ni mawazo mgando. Watoto wakiwa na maadili wala hawatafungua INTERNET na kuangalia ngono. Wazazi wanajaribu kuachia kazi yao ya msingi ya kulea watoto katika maadili mema kwa watu wengine. Huyu Mama Rwakatare akahangaike na kondoo wake huko mlima wa moto. Si wote ni kondoo.
 
JF ni zaidi ya chama chochote cha siasa! Hapa, watu wanathubutu kuongea kwa Uhuru kuliko taasisi yeyote hapa Tg!
Hapa kwa viongozi wote wenye uchungu na uzalendo wa nchi hii, jukwaa hili ndio kioo chao.
A luta continua.
 
kweli wana jf wanaipenda jf yao'member wengi wa jf wana uchungu na nchi yao'najua jf ina watu wa aina mbalimbali'matajiri'maskini'na wenye uwezo wa kawaida'lakini wote hao wana nia nzuri na taifa hili'matajiri walioko hapa ujue walipata hela kihalali'hongera jf na wana jf wote'nimesoma comment zote'jf is family!

Mmmh, hata Ritz!!!!!?????
 
Rwakatare si mchungaji? Mbona anakuwa na chuki? Kauli kama alizototoa walipaswa kuzitoa watu wa mataifa. Yeye kama ni msafi akapige goti kwa Mungu wake, na jinsi Mungu aishivyo, na kama ni msafi kweli basi ombi lake litasikilizwa. Asiandikwe amekuwa nani? Huyu si huwa anaendesha semina za ndoa na kuombea wasio na ndoa na wale ndoa zao zina matatizo? Yeye ndoa yake iko wapi? Watu wa Mungu wanalishwa kasa tu kila leo
 
Lwakatale ni tapeli, mwizi wa roho za watu wenye shida. Anawadanganya kuwa shida zao zitaisha. Ikitokea kuwa na forum za kumwambia ukweli anakuwa mbogo. Anawadanganya watu wasio na matumaini, kama waliokosa watoto/uzazi, mahanisi (wanaume, magonjwa yasiyotibika eti kwa kuwaombea watapona.

Uongo hakuna atakayezaa na umri wa miaka 60 mwanamke!!! anampa hope eti ana nguvu za kumwombea akazaa. Ukiwafumbua macho kwa uongo kama huo ndani ya JF tukufu, anapeleka bungeni ufungwe!1 Shame!!

tena huyu mama ana roho mbaya na ni tapeli mtoa rushwa na matusi aliyonayo sijui kama kweli ni mchungaji niliishawahi kumshuhudia akitoa rushwa kwa wafanyanyakazi wa TUICO ili wamtetee ktk kesi na wafanyakazi wake pale CMA hana maana huyu mama anaogopa maovu yake kuanikwa humu ndani
 
Huyo mamaa Raa kaa tale ana mawazo mgando, mi nlfkiri ataomba facebook ifungwe, mi nlfkiri ataulza n kwann mpaka kesho ikulu inatumia "yahoo" eg. Ikulumawasiliano@yahoo.com, ivi anajua madhara ya aina gan yanapatkana kule facbuk? Huyu n mchumia tumbo tu
 
kwa kadri siku sinavyoenda kama jamii haitasimama basi tutaamka siku moja na kukuta JF imefungwa kwani serikali inaweza kuanza kuwasiliana na makampuni makubwa yenye teknolojia kubwa duniani hili kuhujumu mtandao unaoleta mabadiliko na kufumbua watu macho wa jamii forum.

Nini kifanyike dhidi ya hujuma kwa JF?
 
Atuache na Jf yetu kwenu yeye ndo katuchokonoa wakati anajua si msafi ktk jamii tutaanika maovu yake yote na ajue tunajua kila kitu kuhusu yeye na dereva wake
 
nashauri members wa jf wafahamiane ili wakiifunga jf tunaanzisha forum yenye jina jipya lakini members ni wale wale.huyu mama kakosa heshima kwa waheshimiwa walioko na waliokuwepo humu jamvini(akiwemo katibu mwenezi wa chama kilichompa ulaji),kakosa heshima kwa wafanyakazi waliopo jamvini,kakosa heshima kwa wananchi wanaopata habari kwa wakati kutoka kwa watoa taarifa mbalimbali.kumbe hana heshima na kazi yake ni kuzungukia jukwaa la wakubwa halafu huyooo anaenda kulala.kwa dunia ya leo huwezi kuzuia upashanaji habari...
 
Labels,titles really dont count,its the content that matters. Oh Father forgive them for they know not what they do.
 
kwa kadri siku sinavyoenda kama jamii haitasimama basi tutaamka siku moja na kukuta JF imefungwa kwani serikali inaweza kuanza kuwasiliana na makampuni makubwa yenye teknolojia kubwa duniani hili kuhujumu mtandao unaoleta mabadiliko na kufumbua watu macho wa jamii forum.

Nini kifanyike dhidi ya hujuma za JF?

tutahamia facebook na kuibadlisha sura,wakiifunga nayo tutahamia twitter,wakiifunga twitter tutaenda google,wakiifunga google tutaenda yahoo,nayo wakiifunga tutaanza kutumia sky.com,mpaka wafungie mitandao yote tanzania,turudi enzi za mababu..hii issue itakuwa nzito itofautishe na ************
 
Kuhusu huyo mama na uchungaji wake ulivyo soma Ezekiel 34, utapata jibu
 
Tatizo kubwa la wanasiasa wetu ni kudhani JF inamilikiwa na CDM!!! Wazo hili ni la kishetani kabisa kwani JF ina mmliki wake ambaye ni kama hana mamlaka ya nini afanye zaidi ya kumentani sheria,kanuni na taratibu zinafuatwa ipasavyo.

Ukitoa hilo hana access ya Losambo atapost nini na nini msimamo wangu. Katika kipindi hiki cha watu kupenda mabadiliko ni wazi mitandao mingi sana itachukiwa kwa kuihusisha na siasa za vyama vya upinzani.

Suluhisho ni watu kubadilika na kusoma alama za nyakati kuwa mtu wa jana si wa leo. Watu wanahitaji mabadiliko na wao hawataki mabadiliko hapo ndipo mgongano unapoanzia.
 
Kama vipi tuanze kupanga eneo maalumu kwa kila mkoa ambapo tukishaona tu wamefunga JF hapo ndipo pawe sehemu ya kujadilia mambo/hoja zetu. Yaweza kuwa mara moja kwa mwezi.
 
waziri jana alitumia akili ya ziada kuikingia mkifua jf kwanini? kwa sababu:

hapa jf tunakutana, tunabadilishana mawazo na tunaijenga nchi yetu, na mambo ya humu yanaishia ndani ya mipaka yetu...

itakapobidi kusambaa twitter facebook na kungine...mchele huu utamwagwa kwa wigo mpana zaidi..tena kwa wanaohusika na wasiohusika....
 
Back
Top Bottom