Mama Rwakatare aichongea JamiiForums

Mama Rwakatare aichongea JamiiForums

kama JF inmesajiliwa nje hawawezi kuifunga la sivyo wangelikuwa wamefunga muda mrefu sana Hata hivyo lazima tupigane ili isifungwe

Unajua kilicho waudhi ni kitendo cha JF members kushiriki msiba wa REGIA MTEMA (RIP) aliye kuwa mbunge via CHADEMA hilo linawaumiza sana kwani hakuna mbunge wa CCM ambaye JF ilishiriki wanasahau kuwa REGIA alikuwa member wa JF
 
ushabiki wa vyama uwe nje ya jf hapa uwe utaifa kwanza. uchadema na uccm unaharibu jukwaa na kututoa nje ya mada mara kwa mara
 
haiwezi fungwa.
Imesajiliwa nje so nje ndo kwenye sauti na hii forum.
 
Swali lenyewe limekosea na inashangaza Naibu Waziri ameonekana kulielewa! Swali lilikuwa linauliza kuhusu JF kueneza uongo kwa watu mbalimbali. Suala la umiliki ilikuwa ni katika kusisitizia hoja yenyewe.
 
ambao hawana vyama jf sio mahali pao tunawabagua na kuharibu jukwaa.
 
WanaJF, nimeikutia mada imefika mbali sana na sijui hapo kati kama kuna mtu ametoa suggestion za hatua za kumchukulia huyu mama. Kwa maoni yangu, kama kuna mtu ana data za huyu mama ambaye anapenda hela kiasi cha kuchagua kazi mbili za kinafiki na kuziweka pamoja, basi na afungue uzi mpya, aweke data zake na tumchambue kwa kina ili ajue JF inafananaje hasa.

Nasema hivi kwa kuwa tayari hoja yake imenifanya niamini kuwa kuna kitu anacho na anaogopa siku moja tutakibaini na kukijadili ndio maana ameanza kutu- abolish kimtindo.

Napinga unafiki kwa nguvu zote. Mtumishi wa Mungu hawezi kuwa ZAKAYO at the same time. Huyu mama ni wa kuwekwa jamvini ajadiliwe ndani nje. Kuanzia accounts zake mpk imani yake
 
jf haturuhusu washiriki wa mlengo wa kati tunawaona ni wasaliti na hivyo tunaminya uhuru na demokrasia
 
Nashindwa kuelewa kinacho mkwaza huyu Mbunge nini kwani

JF inataratibu zake na zinafuatwa mfano Member anaye toa lugha ya Uchochezi, Matusi, Ukabila, Udini anapigwa ban sasa tatizo ni nini ingelikuwa adhabu hazitolewi hapo ingelionekana JF inashabikia haya mambo

Huyu mama tatizo lake ni nini hasa ELIMU, DINI, SIASA za mlengo aliko UWEZO wa kuelewa mambo au nini hasa ?????????/
 
Si nilisikia nepi anafungua mtandao wa kupambana na jf amefikia wapi, anaye ujua atwambie tuingie tuwape za uso.
 
Mimi sishangai kwa hili...hakuna serekali yoyote duniani inayopenda kukosolewa ama kuanikwa maovu yao hadharani...wana jf kumbukeni ni mara ngapi gazeti la mwanahalisi limepigwa mkwara wa kufungiwa kwa kile walilichokiita kukiuka kanuni zao uandishi au uchochezi mara kuichafua serekali....kwa kiongozi yeyote wa kijamii ikimaanisha kuanzia raid mpaka wenyeviti wa mitaa sharti ease watu waadilifu sasa mbunge akionekana anafanya upuuzi na kudhalilisha wadhfa wake na nchi asinyooshewe kidole?? Mimi naamini si kila linaloandikwa jf ni upuuzi....unajuwa siku zote anaekosa hakubali kuwa ni kosa atajaribu kuhalalisha makosa yake yawe si si makosa....sasa wakisema wanataka wafunge jf basi wafunge mitandao yote yakijamii
 
Huyu mama ni wa ajabu sana. Ameshindwa kumdhibiti mwanae shoga ataiweza JF?
Anafanya haya kufunika madudu yake binafsi yanayojulikana wazi kwa jamii, nitaweka wazi madudu haya wazi hivi karibuni.

Yes yes yes mkuu. Nitafurahi data zake in 'n' out zikiwekwa hapa tumjadili. Ana haofu kuwa siku moja tutafunua majidudu yake.

Kuna ana mpunga nyumbani mwake halafu analaumu watwangaji!
 
WanaJF, nimeikutia mada imefika mbali sana na sijui hapo kati kama kuna mtu ametoa suggestion za hatua za kumchukulia huyu mama. Kwa maoni yangu, kama kuna mtu ana data za huyu mama ambaye anapenda hela kiasi cha kuchagua kazi mbili za kinafiki na kuziweka pamoja, basi na afungue uzi mpya, aweke data zake na tumchambue kwa kina ili ajue JF inafananaje hasa.

Nasema hivi kwa kuwa tayari hoja yake imenifanya niamini kuwa kuna kitu anacho na anaogopa siku moja tutakibaini na kukijadili ndio maana ameanza kutu- abolish kimtindo.

Napinga unafiki kwa nguvu zote. Mtumishi wa Mungu hawezi kuwa ZAKAYO at the same time. Huyu mama ni wa kuwekwa jamvini ajadiliwe ndani nje. Kuanzia accounts zake mpk imani yake

naunga mkono hoja,subiri nikusanye madudu yake yote na ushahidi wa kutosha wa kesi iliyofunguliwa na wafanyakazi wake pale TUICO jinsi alivyokuwa akiichakachua na kudhulumu haki za wafanyakazi wake nitayamwaga madudu yake yasiyopingika
 
Baada ya gazeti la habari leo, Tanzania Daima na mengineyo kuandika habari kuhusu Jamii Forums watu makini wameanza kuingia kwenye mitandao na kuanza kuitafuta JF waone kuna nini hadi baadhi ya Wabunge wailalamikie. Mdau mmoja kutoka dodoma anasema baadhi ya wabunge waliokuwa hawaijui JF waliamua jana jioni kuulizana na weng wao wakaingia kuona kuna nini. Zoezi hili si kwa wabunge tu bali hata watu wengine makini.......wameanza kuperuzi kuon JF kuna nini. Leo JF itakuwa na guests wengi kuliko Members katika baadhi ya thread. Then baadhi ya wadau wanahoji matusi yanayoongelewa na Mchungaji Rwakatare.......yako Mambo ya Kikubwa na nilazima uwe member......sasa yeye kilichomtuma kuwa member tena inawezekana Premium Member ili aone mambo ya kikubwa ni nini? Alienda kutafuta nini kule?

Baadhi ya habari kuhusu Jamii Forum kama ilivyopewa kipaumbele leo ni hii hapa



Habari za Kitaifa

Jamii Forum haijasajiliwa Tanzania


MTANDAO wa kijamii wa Jamii Forum haujasajiliwa Tanzania, Bunge limeelezwa.

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Charles Kitwanga, amewaeleza wabunge kuwa, mmiliki wa mtandao huo anaweza kuwa Mtanzania au si Mtanzania.

Ameyasema hayo bungeni mjini Dodoma wakati anajibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Getrude Lwakatare (CCM).

Mbunge huyo amedai kuwa, Mtandao huo umekuwa ukisambaza habari za uongo kwa watu mbalimbali na haujachukuliwa hatua hivyo alitaka kumfahamu mmiliki wa mtandao huo.

Kitwanga amesema, uanzishwaji wa tovuti za kijamii haulazimishi mtu kujisajili wala kujitambulisha , na huanzishwa na mtu yeyote popote duniani.

“Kutokana na asili na miundo ya tovuti za kijamii, mamlaka haisajili wala kutoa leseni kwa tovuti hizo, kimsingi maudhui yanayoadikwa katika tovuti hizo za kijamii ni maoni binafsi ya watu yasiyoangaliwa iwapo ni ya kweli au la” amesema Kitwanga.

Baada ya Mbunge wa Viti Maalum, Hilda Ngoye (CCM) kuuliza swali la nyongeza, wakati Kitwanga anajiandaa kumjibu, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, alimtaka kiongozi huyo wa Serikali, ajibu hasa swali kuhusu ‘ Jamii Forum na matatizo yake makubwa’

Ngoye amedai kuwa, baadhi ya mambo yanayoandikwa kwenye mtandao wa Jamii Forum yana madhara katika jamii yakiwemo matusi ya nguoni na ni kinyume cha utamaduni wa Mtanzania.

Aliuliza kama Serikali ipo tayari kuwasilisha bungeni muswada , Bunge litunge sheria ili mtandao huo uache kuandika mambo ya maudhi na uchochezi.

Alitaka pia kufahamu kama Serikali ipo tayari kuwasilisha bungeni muswada ili Bunge litunge sheria itakayozuia watoto kusoma ‘mambo machafu’ kwenye ‘internet café’ vikiwemo vitendo vya ngono.

Kitwanga amesema, suala la kudhiti mitandao ya kijamii litakuwa kwenye Muswada wa Sheria ya Habari.

Amesema, suala la maadili ya watoto ni jukumu la wazazi, na kwamba ndiyo wanaowapa fedha za kwenda ‘Internet café’.

Amesema, kutokana na kukua kwa teknolojia ya mawasiliano, kuna namna nyingi zinazowawezesha watoto kuona ‘mambo yasiyofaa’ zikiwemo simu za mkononi, ipad, na laptops.

Amesema ni wajibu wa wazazi kuhakikisha kuwa watoto wao wanakua kwa mujibu wa maadili ya taifa.
 
Ubovu wa kufikiri wa mkuu wa kaya. Hii huyu mama alipewa huo ubunge kwa kigezo gani ?
Au Jk alitaka tu kuweka hata vilaza ili kutimiza idadi ya wateule aliotakiwa kuwaweka !
 
....hatuwezi sema nini kifanyike humuhumu janvini kwa misingi siri zinaweza kuwafikia maadui, hivyo tukiona kuna haja ya ku-mentain status ya JF tutatafuta mahala kwa muda muhafaka na kuweka mkakati mpya:
 
Back
Top Bottom