Mama Rwakatare aichongea JamiiForums

Mama Rwakatare aichongea JamiiForums

Kwa mwendo wa Jf ya sasa sitashangaa ikifungiwa tumeacha kujenga hoja tumegeuka ni kijiwe ya wahuni na matusi.

KUMBUKA: Wahenga walisema "AKUANZAE MMALIZE, UKIMUACHA ATAKUMALIZA WEWE"

MIZAMBWA
INANIUMA SANA
 
JF haitafungwa leo wala kesho, JF ni kioo cha serikali tawala. Serikali inapata kujua nini kinaendelea, watu wanafikiri nini kuhusu serikali na mambo mengine, hivyo si rahisi kuifungia. Mawaziri, wabunge na viongozi wengi sana wanapitia hapa kila siku kutaka kujua nini kinaendelea.
 
There are currently 413 users browsing this thread. (129 members and 284 guests)
 
mmeo alimfuma na kosa gani mpaka akaamua kumwacha Getrude???
 
Aeleze kwanza hatua zipi alizochukua kwa madereva wa ma bus ya shule zake za st marys wanaowanajisi wanafunzi kila siku
 
Wana JF kutokana na mtandao huu wa kijamii kuibua na kueneza siri za Serikali Wabunge wa CCM wameridhia Mtandao huo ufungwe kama ilivyokuwa Ze Utamu na Mtoa Hoja ni Mchungaji Getrude Lwakatale, Leo pia kapeleka swali lake Bungeni.

Waziri kaitetea JF na kuwashauri wabunge kuwa ni chombo cha habari cha kijamii.
Niliwaambia wajameni hii JF inatishia maslahi ya watu, kwa hiyo ukiona hivyo dalili za mvua ni mawingu!!!! Lakini siku hizi kuna wabunge makini wengine ni member wa JF sijui kama wataingia dili ya kufuta mtandao wetu, akili mu kichwa!!!!
 
Ilikuwa Jambo forum, wakaja waliokuwa na kimbelembele kama Lwakatare, wakaifunga, ikaibuka kali zaidi inaitwa Jamii forums, wakiifunga itaanzishwa wananchi forum na hapo watakuwa kwenye hatari kubwa zaidi hawa wana ccmagamba
 
JF Ni Dunia, Siyo Taanzania Pekee, ukiitazama JF Kwa umakini kabisa utaona kuwa uko ndani ya Dunia, Yenye kukupa kila aina ya Taarifa kutoka kila kona katika Globe yetu na Taarifa nyingi huwa ni Live. Lakini ukirudi kwa upande wa Watawala JF ni mwiba hasa kwa hawa watawala wetu Goigoi wa Kufikiri na kuamua. Mwisho JF ni Gurudmu la Mageuzi ya Fikra kwa wote bila kujali Chama wala Itikadi.Long Live JF.
 
mtu kama huyu mama huwezi kutegemea jambo lolote la maana toka kwake.ni vema kumsamehe bure tu.naibu waziri ameitetea JF,na kwa uweza wa Mungu aliye hai haitafungwa katu.JF aluta continua
 
Tatizo ni hizi posho kaona bora aropoke urojo ili hansard isome..
 
Kama kuna siku magamba watakua wamekosea step ni kufunga JF maana kitakochokuja kitakuwa moto zaidi ya JF.

Nadhani hawawezi lifikiria hili la kutufungia maana wanajua lililowapata na umaarufu waliotuongezea maana ya kutufungia kule Jambo Forums
 
Huyu mama mchungaji kama kayasema hayo basi kuna nyuzi zimemgusa humu. Hawa wana siasa wasikubali kupokea "criticism" walikuwa hawafai kabisa kuwa wana siasa. Anafikiri JF ni kanisa kwake humu, kila atakalo sema watu watamchekelea tu.

Hawa ndio wale wanaoingia siasa kwa sifa na pesa zao na si kwa kuwa ni wana siasa. Mie alivyoingia nikajuwa anhaa sasa, tumepata msemaji ambae atakwenda mjengoni kufanya mambo, kumbe si lolote si chochote. Waondoe tu hivi viti vya kupeana.
Umenena bibi, hapa sio kule kwenye ile business yake...tunajipanga tuanze kukusanya kodi kutoka huko! maana ni biashara kama biashara nyingine.
 
huyu mama siku za weekend kanisani kwake ni mkesha,kelele mpaka majirani wanashindwa kulala,ukipangisha nyumba,wapangaji kutokana na kelele wanahama.hakuna uchungaji wala nini hapo,huyu ni kanjanja na mwizi!
 
Wanashindwa kujadili mambo yanayohusu maendeleo ya taifa, wanataka kulalamika kuhusu JF. Kwani wamechaguliwa na Wananchi ii kwenda kujadili mawazo ya watu au kujadili mambo yanayohusu Taifa.

JF hili ni bunge letu na sisi tunatoa mawazo yetu hapa kama wao wanavyotoa pale Bungeni.

Sasa hili bunge letu la JF ni kwamba linajadili mambo kiunsdani na yaliyo ya kweli ndio maana wanataka kutufunga midomo. haiwahusu wao kujua Owner ni nani!!!! Mbona sisis wao wanajadili mambo yasiyo kuwa na maana lakini hatuwafungi midomo.

Katika ya Tanzanai inaturuhusu kutoa mawazo yetu tupo huru kwa hili. Na kama wanafungua hii Website ni heri kwani watajua kuwa na sisi tuna uwezo wa kujadili mambo ingawa hatulipwi Posho kma wao, lakini tungepewa nafasi huenda matatizo yanayojitokeza Tanzania sasa yangepata muafaka, kwani mawazo yanayotolewa hapa ni mazuri sana na ya kujenga.

Nakumbuka kulikuwa na website moja inayoitwa bcstimes ambayo ilikuwa inamilikiwa na magazeti ya Majira, kutokana na mawazo mazuri tuliyokuwa tunatoa waliamua kuweka mijadala yetu katika gazeti, yaani tulikuwa na ukurasa kabisa kwa ajili ya mijadala ya members. Lakini sasa kila nikijaribu siipati tena ile website, sijui ndio Bunge la Tanzania wameamua kuipiga mkwara nayo.
Pia na hata kwenye gazeti siku hizi hakuna tena ule ukurasa. Nina wasiwasi na wabunge huenda wameshatia mkono kuifunga ile website.

NAOMBA WATUACHE BUNGENI WAJADILI YANAYOWAHUSU NAO WAKITAKA KUJISAJILI HAPA WAPO HURU LAKINI SIYO KUFANYA NDIO HOJA YA KUPELEKA BUNGENI.

MKOMEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE KABISAAAAAAAAAAAAAAAAAA


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!

UKO SAHIHI nadhani kinachosumbua ni pale watu wachache wanapoamua kutumia JF vibaya hadi inataka kugeuka kama mitandao ile yenye kutweza na kudhalilisha watu katika mambo yasiyo ya kweli.Mimi sioni ubaya pale ukweli unaposemwa.Tatizo ni pale watu wanapotumia matusi kuyaelekeza kwa watu ambao hawana fursa kujitetea au pale mtu aliyejificha nyuma ya keyboard anapotumia maficho kutimiza azma ya kisasi au kuonea kwa makusudi kwa vile tu ameamua kumuumiza mtu.

Uhuru wa mawazo ni haki ya kikatiba na kila mtu mtu anayo hiyo haki mradi havunji sheria.Kutukana matusi ya nguoni siyo haki ya mtu na ni uvunjifu wa sheria.Ninaamini kabisa kwamba pale mtu anaposema mambo ya kweli kwa lugha ya staha atakuwa anajiamini na ujumbe utawafikia wahusika.

Haina haja kutumia matusi ya nguoni kwa mtu yeyote awe raia wa kawaida au kiongozi.
 
Back
Top Bottom