Malori 25 ya Mahindi yazuiliwa kuingia Kenya

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,638
2,000
Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe akiwa na Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Nchini (TBS) Yusufu Ngenya, pamoja na mkuu wa kitengo cha Afya ya mimea, katika mpaka wa Namanga, ambapo kwa pamoja wameonekana kushangazwa kwa kuzuiliwa kwa malori 25 ya shehena ya Mahindi kutoka Tanzania.

Hata hivyo Bashe akawatoa wasiwasi wafanyabiashara ya mazao nchini kwa kusema Serikali inalifanyia kazi jambo hilo kwa uzito wa kutosha na kwa sasa wawe watulivu huku akitoa wito kwa serikali ya Kenya kutoa taarifa ya zuio hilo kwa utaratibu rasmi.

Chimbuko la sakata hili ni barua iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii na kudaiwa ni kutoka Serikali ya Kenya kuzuia mahindi ya Tanzania na Uganda kuingia Tanzania.

Mahindi.jpgEATV
 

Shift

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
1,051
2,000
Hata hivyo Bashe akawatoa wasiwasi wafanya biashara ya mazao nchini kwa kusema serikali inalifanyia kazi jambo hilo kwa uzito wa kutosha na kwa sasa wawe watulivu huku akitoa wito kwa serikali ya Kenya kutoa taarifa ya zuio hilo kwa utaratibu rasmi.
Kawadanyanga, hawatafanya chochote. Kufanya biiashala Tanzania nikujitia hasala na plesha tu isiyo ya lazima
 

mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
2,011
2,000
Hapo ndipo hasa wanadiplomasia walipaswa kuingilia kati sakata hili likiwa bado changa kabisa. Migogoro kama hii ni sehemu tu ya maisha ya kila siku, viongozi wa kitaifa wanaweza kufanya mazungumzo hata kupitia "zoom meeting" na kusawazisha mambo kama haya. Sijui hata wanafeli wapi?
 

Bombabomba

JF-Expert Member
Dec 23, 2017
1,279
2,000
...midomo ya wanasiasa ndo imetufikisha hapo majigambo ya kishamba kwenye mambo ya msingi kama haya haitakiwi....kwa zuio hili tunapaswa kujitathimini mienendo yetu na majirani zetu tunaumiza wafanya biashara wetu
Halafu ninesoma hiyo BARUA kumbe ni maelekezo tu ya ndani, hivyo inawezekana hakuna too. Ya discussion kwa sababu hatujaandikiwa sisi. Hi mawaisliano yao ya ndani. Matokeo yake ndio haya, kwamba wafanya Biashara wao hawatakuja kuchukua mahibdi yetu
 

Nazgur

JF-Expert Member
Apr 19, 2020
2,910
2,000
Hapo ndipo hasa wanadiplomasia walipaswa kuingilia kati sakata hili likiwa bado changa kabisa. Migogoro kama hii ni sehemu tu ya maisha ya kila siku, viongozi wa kitaifa wanaweza kufanya mazungumzo hata kupitia "zoom meeting" na kusawazisha mambo kama haya. Sijui hata wanafeli wapi?
Huo ni ujinga wako, wafanye mazungumzo gani sasa?

Wazungumze ili sumu iendelee kwenda kenya?

Cha kufanya ni kukagua mahindi kama yana sumu, na kama hayana basi serrikari itafute soko sehemu ingine na siku wakija kutaka kununua inabidi walipe na fidia za usumbufu pia watangaze kuwa wakuongea uongo.
 

mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
2,011
2,000
Huo ni ujinga wako, wafanye mazungumzo gani sasa?...
Mkuu, kupitia mazungumzo hata kwa njia ya simu ndipo ambapo muafaka wa kuweza kukagua upya shehena za mahindi kabla ya kuingia nchini Kenya utapatikana. Ni ujinga kufikiria kuweza kupata ufumbuzi wa mgogoro huu nje ya kutokuwepo kwa mazungumzo ya pande hizi mbili.
 

Nrangoo

JF-Expert Member
May 22, 2017
2,132
2,000
Mitihani kwa Waziri wa Kilimo Prof Mkenda

1. Nzige

2. Kuzuiwa kwa usafirishaji wa mahindi kutoka Tanzania kwenda nchini Kenya

3.


4.
 

Nazgur

JF-Expert Member
Apr 19, 2020
2,910
2,000
Mkuu, kupitia mazungumzo hata kwa njia ya simu ndipo ambapo muafaka wa kuweza kukagua upya shehena za mahindi kabla ya kuingia nchini Kenya utapatikana. Ni ujinga kufikiria kuweza kupata ufumbuzi wa mgogoro huu nje ya kutokuwepo kwa mazungumzo ya pande hizi mbili.
Wewe unadhani hayo mahindi yana sumu?

Na ikionekana hayana hiyo sumu nani wa kulaumiwa tanzania au Kenya?

Kwanza tanzania tunatakiwa kujiridhisha kama hayo mahindi yana sumu, na kama hayana basi hakuna haja ya kuwabembeleza watu wenye nia ovu. Na kama yana hiyo sumu ni wajibu wetu kuiondoa hiyo sumu kisha kuwaambia nao wajiridhishe na watayachukua. Ni haki yao kujilinda.

Hatuwezi kuwabaembeleza kama mahindi hayana sumu na wao wameamua kutoyachuku kwa hila zao.
 

Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
12,219
2,000
Chimbuko la sakata hili ni barua iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii na kudaiwa ni kutoka Serikali ya Kenya kuzuia mahindi ya Tanzania na Uganda kuingia Tanzania
How do we know kuwa hiki ndicho kisababishi because barua tajwa ni ya zamani
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom