Baada ya tamko la Rais kuzuia mahindi kwenda nje malori yenye shehena za mahindi yamezuiwa kwenda nchi za nje, Ukitembelea maeneo mengi ya mpakani hasa kule Sirari na Namanga kuna malori mengi sana yamezuiwa kuingia Kenya.
Zuio hili la mahindi litawanufaisha wachache maana Tanzania sio kisiwa, haiwezekani mahindi gunia Tanzania liuzwe 50,000/- halafu Kenya liuzwe 150,000/- sisi Tanzania tuwe salama, kwa vyovyote vile mahindi hayo yatatoroshwa kwenda nje maana nchi yetu sio kisiwa.
Zuio hili litaleta hasara kubwa kwa wakulima maana wajanja wachache watalangua mahindi hayo kwa bei ndogo na kuyatorosha kwenda nje matokeo yake nchi itakosa mapato pia na wakulima kupata hasara, Ukitembelea maeneo ya mpakani tayari imeishakuwa dili la polisi na watu wa Tra.
Wito wangu kwa serikali iruhusu mahindi yaende nje tupate mapato na vile vile wakulima wetu wapate faida na kufurahia matunda ya kazi, hii pia itaweza kuwavutia wengi kujishughulisha na shughuli za kilimo na ile dhana ya kudharau kilimo na wakulima itafutika.
Lakini pia serikali ikumbuke gharama za kilimo zimepanda sana mathalani kulima ekari moja mkulima hutumia wastani wa 700,000/-~ 900,000/-, ekari moja hutoa wastani wa gunia 15~20, hivyo mkulima akiuza mazao yake kwa bei ndogo atapata hasara na msimu unaofuata hatajihusisha tena na kilimo au atapunguza uzalishaji.
Serikali itumie hii kama fursa kuhakikisha tunaboresha kilimo chetu ili tuweze kuwaalisha majirani zetu, na kutengeneza ajira pia.