Dina, unapokopeshwa na benki, miongoni mwa vipengele vya mkopaji na mkopeshwaji ni kipengele cha confidentiality, kama ili kwa mwanasheria na mteja wake, mwalimu na mwanafunzi, daktari na mgonjwa, benker na mteja etc!.
Kwenye ulimwengu wa biashara kuna kinaitwa "corporate veil", unapokopeshwa kama kampuni, jina rasmi la kutumika ni jina la taasisi, benki hairuhusiwi to dislose details za wadeni wake, mpaka kwanza waende mahakamani kuomba kibali cha ku unveil ile corporate veil, ndipo wamiliki wanakuwa disclosed na kushitakiwa as individuals!.
Bahati mbaya wengi humu ni vijana wajuzi juzi tuu, kwa wale wazamani wanaweza kukumbuka kisa cha Gazeti la Mtanzania na Banki ya NBC kushitakiwa katika kesi ya madai ya mabilioni ya shilingi, baada ya gazeti hilo kutoa story ya jinsi tajirti fulani anavyodaiwa na NBC.
Tajiri yule alikwenda mahakamani kuishitaki NBC kwa breach of confidentiality kwa ku leak details za madeni ya mteja, mshtakiwa wa pili lilikuwa ni gazeti la Mtanzania enzi hizo chini ya Generali Ulimwengu, ilikuwa gazeti lifilisiwe!. NBC na Mtanzania waka opt for out of court, wakamalizana!.
Japo siyajui mazingira haswa ya deni husika, Komba ni VIP, Mhe. Mbunge, Mjumbe wa NEC ya CCM ni heavy weight, kitendo cha kutajwa tuu anadaiwa ni aibu!. Miradi yake kudaiwa is fine not him!. Kuandika kuwa anafilisiwa kwa kumtaja jina at personal capacity ni kumchafulia jina!. Akipata mwanasheria nguli, anafungua kesi ya madai kuchafuliwa jina na anashinda!.
Pasco.