Mali za CCM zipigwe mnada; nyingi ziliibwa kwenye mfumo wa Chama kimoja TANU na ASP

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,300
2,000
Ni mali nyingi sana Chama hiki kimejimilikisha kama tunavyoona kila CCM anaepata uongozi serikalini nae hukwapua mali na hata kugonga milango ya BoT na kufanya mazabe mpaka hufanikiwa kumega, tumesikia kutoka kwa mkaguzi ya kuwa kuna hela haioni.

Na ndio tukaona hakuna MCCM anaeendelea, mwisho wao wengi huumbuka na kuadhirika mchana kweupe, tunawaona wanavyoshikana mashati na kukwidana eti wanapelekana mahakamani, nchi hii ina maajabu sana, naukumbuka msemo usemao mwenye nguvu mpishe.

Aibu kila uongozi unaoingia unasonyesha dalili za uongozi uliopita walikuwa na vibaka wakabaji wauawaji.
 
Kabugula

JF-Expert Member
May 25, 2021
1,716
2,000
Kwani ripoti ya uhakiki was Mali za chama itasomwa lini?

Bashiru alikuwa Mkiti wa uhakiki, sasa inakuwaje chama kongwe taarifa hatupati.
 
Idimi

JF-Expert Member
Mar 18, 2007
14,259
2,000
Kwani ripoti ya uhakiki was Mali za chama itasomwa lini?
Bashiru alikuwa Mkiti wa uhakiki,sasa inakuwaje chama kongwe taarifa hatupati.
Ile ripoti haitakuja kusomwa KAMWE. Mwendazake alikuja moto sana kutaka kuiweka hadharani, lakini akakuta waliokuwa wamehodhi zile mali za chama ni watu wanene sana ndani ya CCM (na wengine ndo walimfikisha pale alipokuwa), akaishia kuufyata pamoja na ukali wake wote! Kumbuka kwamba chama KINA WENYEWE.
 
untimwenge

Member
Apr 27, 2020
43
125
Ni mali nyingi sana Chama hiki kimejimilikisha kama tunavyoona kila CCM anaepata uongozi serikalini nae hukwapua mali na hata kugonga milango ya BOT na kufanya mazabe mpaka hufanikiwa kumega ,tumesikia kutoka kwa mkaguzi ya kuwa kuna hela haioni...
Viwanja vyote vya michezo nchini wamejitwalia kiharamu. Unatakiwa ifike mahali hizi mali zitaifishwe.

Inashindikana nini kutaifisha mali walizochuma watanzania pamoja, wakati ilikuwa rahisi kutaifisha shule za mashirika ya dini, au mkoloni mweusi anatisha kuliko mkoloni mweupe?
 
Bunsen Burner

JF-Expert Member
Feb 25, 2009
591
1,000
Viwanja vyote vya michezo nchini wamejitwalia kiharamu. Unatakiwa ifike mahali hizi mali zitaifishwe.
Inashindikana nini kutaifisha mali walizochuma watanzania pamoja, wakati ilikuwa rahisi kutaifisha shule za mashirika ya dini, au mkoloni mweusi anatisha kuliko mkoloni mweupe?
Kweli aiseee,yaani kama vile viwanja kuna pesa watz wote tulilazimika kuchangia kupitia bei za bidhaa mbalimbali zilizokuwa tunanunua kama sabuni,mafuta,sukari ili vijengwe.... ilibidi tuwe wapole tu ....
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
24,332
2,000
Ni kweli, Kwa mfano viwanja vya mpira vingi tu tulivijenga kwa kushututishwa aka Nguvu Kazi - tukachangishwa Mbuzi, ngombe, kuku, bata na kama huna basi utafyatua matofali hadi ukome - sasa vyoote wamevibatiza majina eti viwanja vya CCM - Mungu anawaona nyiee CCM.
 
sweettablet

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
7,476
2,000
Ni mali nyingi sana Chama hiki kimejimilikisha kama tunavyoona kila CCM anaepata uongozi serikalini nae hukwapua mali na hata kugonga milango ya BoT na kufanya mazabe mpaka hufanikiwa kumega, tumesikia kutoka kwa mkaguzi ya kuwa kuna hela haioni.

Na ndio tukaona hakuna MCCM anaeendelea, mwisho wao wengi huumbuka na kuadhirika mchana kweupe, tunawaona wanavyoshikana mashati na kukwidana eti wanapelekana mahakamani, nchi hii ina maajabu sana, naukumbuka msemo usemao mwenye nguvu mpishe.

Aibu kila uongozi unaoingia unasonyesha dalili za uongozi uliopita walikuwa na vibaka wakabaji wauawaji.
Ndio maana Chadema hawajengi ofisi. Wanaogopa hoja kama hizi.
 
Izia

JF-Expert Member
Jun 9, 2021
304
500
Ndio maana Chadema hawajengi ofisi. Wanaogopa hoja kama hizi.
CHADEMA wanajenga ofisi kwa nguvu za wanachama wao hivyo zitabaki kuwa za chama tofauti na CCM baadhi ya nyumba zao na viwanja vyote vya mpira na sabasaba vimejengwa kwa fedha za umma na rasilimali za serikali kama watumishi na vyombo vya ujenzi na pia wananchi wa kawaida na pia wafanyabiashara ambao wala si wanachama wao!
 
Kamakabuzi

JF-Expert Member
Dec 3, 2007
2,288
2,000
Viwanja vyote vya michezo nchini wamejitwalia kiharamu. Unatakiwa ifike mahali hizi mali zitaifishwe.

Inashindikana nini kutaifisha mali walizochuma watanzania pamoja, wakati ilikuwa rahisi kutaifisha shule za mashirika ya dini, au mkoloni mweusi anatisha kuliko mkoloni mweupe?
Utasikia jina la uwanja wanatanguliza ccm, ujue tayari wameuchukua huo, Wa hivi karibuni ni ule wa Jamhuri Dodoma, Walianza kuuita eti ccmJamhuri!
 
Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
1,773
2,000
Nashangaa sana uwanja mkubwa hapa Mwanza unaitwa CCM-Kirumba wakati wananchi wote bila kujali itikadi zao za kisiasa walichangia ujenzi wa uwanja huo.
 
sweettablet

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
7,476
2,000
CHADEMA wanajenga ofisi kwa nguvu za wanachama wao hivyo zitabaki kuwa za chama tofauti na CCM baadhi ya nyumba zao na viwanja vyote vya mpira na sabasaba vimejengwa kwa fedha za umma na rasilimali za serikali kama watumishi na vyombo vya ujenzi na pia wananchi wa kawaida na pia wafanyabiashara ambao wala si wanachama wao!
Ofisi gani hizo zinazojengwa na wanachama wa Chadema? Watu tumetoka kazini tumechoka wewe unaleta mizaha!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom