Tanzania bado tuko kwenye Mfumo wa Chama Kimoja ambapo Mwenyekiti wa CCM ndio Mdhibiti Mkuu wa Siasa za nchi!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,840
141,759
Huu ndio Ukwelik wamba Mwenyekiti wa CCM ndiye Mdhibiti Mkuu wa Siasa nchini.

Na ndio sababu Rais wa JMT akishachaguliwa faster anapewa Uenyekiti wa Chama lakini Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Mwenyekiti atasubiri hadi Mkutano Mkuu wa Uchaguzi ufike.

Ikumbukwe Katiba ya JMT ni ya 1977 na Katiba ya CCM ni ya 1977 zote zimefanyiwa tu marekebisho kadhaa.

CHADEMA ni lazima walielewe hili hasa hawa CHADEMA wadogo wadogo akina Mdude.

Mwenyekiti Mkuu wa Vyama vyote vya Siasa ni Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Rais wa JMT na Amiri Jeshi Mkuu na kwa sasa ni mpendwa wetu Dr. Samia.

Tunakumbushana tu kwa sababu Chama Kimoja kususa hakutafanya Uchaguzi uhairishwe. CUF walisusa kule Zanzibar lakini Uchaguzi unafanyika na CHADEMA na Wapinzani wengine walishiriki.

Mungu wa mbinguni akubariki!
 
Huu ndio Ukwelik wamba Mwenyekiti wa CCM ndiye Mdhibiti Mkuu wa Siasa nchini.
hatuna chama cha siasa kinaitwa CCM, bali tuna dola iliyojipa jina la CCM ambayo ndiyo inaongoza nchi ambapo Mwenyekiti wake ndiye Rais wa nchi na amiri jeshi mkuu wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama. Na mwenyekiti huyu wa CCM ndiye anachagua Jaji Kiongizi na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi - Tume ambayo ndiyo itasimamia uchaguzi mkuu ambayo Rais ama mwenyekiti huyu huyu na naye atakuwa mgombea.

Mtanzania unaona mchezo ulivyo mtaam?
 
hatuna chama cha siasa kinaitwa CCM, bali tuna dola iliyojipa jina la CCM ambayo ndiyo inaongoza nchi ambapo Mwenyekiti wake ndiye Rais wa nchi na amiri jeshi mkuu wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama.
Chama Dola
 
Back
Top Bottom