TANU na CCM walikuwa wanawasomesha watu wa propaganda nje ya nchi kwa ajili yakukabiliana na Nani wakati wa chama kimoja?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
495
1,000
Chama Cha mapinduzi pamoja na TANU enzi zetu vilikuwa vinapeleka vijana kwenda kusoma propaganda na mambo ya siasa nje ya nchi. Baadhi yao ni akina Mrema wa TLP, baada ya watu hao kurejea nchini hakukuwa na propaganda tena kwa sababu walikuwa chama kimoja. Hata tulipoingia vyama vingi bado watu Hawa awakutumika kwa sababu wale wale watu waliosoma nje ndio waliomeguka kwenda upinzani nakutafuta Uhuru wao na popularity.

Huwa tunaaminishwa kwamba Wana CCM Hawa walikuwa wamejiegesha upinzani kwa lengo la kuua upinzani lakini wote ni mashahidi kwamba upinzani au vyama vya upinzani vilivyoyumba havikuyumbishwa na Hawa tunaoambiwa walisoma nje au walikuwa TISs. Mara zote kinachofanyika nikutumia mifumo ya haki kuminya haki isitendeke.

Sasa hivi najiuliza kwanini mwalimu aliamini kwamba tunatakiwa kuwa na watu ndani ya mfumo wa siasa waliosoma nje ya nchi nakubobea siasa wakati watu hao hawajawahi kutumika kusaidia siasa?

Leo tukiviweka vyombo vya dola pembeni tukawapa wanapropaganda kazi yakuipigania ccm ibaki madarakani wataweza kutumia elimu zao kushawishi watu wakubaliane nao? Je, Dunia iliacha lini kuendeshwa kwa propaganda na sisi kuacha kuwekeza kwenye eneo hili?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom