Mali za CCM zilizotokana na makato kwa raia wote wakati wa chama kimoja ni haki ya nani?

Rwaz

JF-Expert Member
May 3, 2013
1,970
3,325
Mada yangu iko wazi wazi.

Naomba wajuvi wa mambo ya haki na umiliki, bila mahaba ya kisiasa waniweke sawa. Hivi mali zilizopatikana kwakuwakata tozo na kodi na ushuru, raia wote wakat wa chama kimoja cha CCM leo hii kwa nini wazimiliki raia wa chama kimoja?

Hapa namaanisha majumba, viwanja, maeneo ya wazi, hisa n.k. Au ni bomu linalosubiri chama kingine kikichukua nchi ndo ifanyike marekebisho!

Enzi hizo wananchi wote tulikatwa katika mauzo mbali mbali na huduma kama mazao, uvuvi, madini kupitia vyama vya msingi na beria mbali mbali.

Kuukataa ukweli ni sawa na kujificha mbuni style.
 
Uwanja was Mapinduzi mkoani Mbeya ulijengwa na wananchi, meaka 1984 alipofariki EDWARD MORINGE SOKOINE, uwanja ukabadilishwa jina.

Nikishangaa mwaka 1991 CCM wakatangaza kuwa ni uwanja wao.

Kuna siku raia wapenda hakiwatatambua kuwa adui yao mkubwa NI CCM, huo utakuwa ni mwanzo TU, CCM Chanzo Cha Matatizo
 
Ohoooo, shauri yako! Afadhali zamani hizo. Hivi leo hawamiliki mali tu, wanamiliki hadi watu. Hawamiliki tu sheria, wanamiliki hadi haki, Hawamiliki tu usalama wako, wanamiliki haki hewa unayopumua. Hawamiliki tu uhuru wako wa kuongea, wanamiliki hadi kile unachosikia. Wanamiliki anga na vyote vinavyopaa huko, wanamilki ardhi na vyote vinavyotembea juu yake na wanamiliki maji na vyote vinavyoogelea ndani yake. Kwa kifupi CCM wanaimiliki Tanzania na vyote vilivyomo. Halafu wewe una jeuri ya kuulizia eti viwanja, majengo na magari ni vya nani...kweli?
 
Reactions: BAK
Viwanja vyote vilipaswa kurudishwa kwa wananchi kwa kukabidhiwa Halmashauri ya maeneo husika kwa sababu ni michango ya wananchi ndio iliyojenga viwanja hivyo.
Tungekuwa mbali sana,viwanja vingekuwa sasa vina hudumiwa na Serikali kupitia Halmashauri,tungekuwa tunazungumzia namna ya kuweka viti,taa na kuweka nyasi bandia.
Mahudhurio katika michezo ingeongezeka.
 
Mali ni haki ya Serikali,zirudishwe kwenye Serikali kwa maeneo husika(Halmashauri),wasikae kimya historia itawahukumu kwa kuwa mfano wa chama kilichodhulumu haki ya wananchi.
 
Kuna jamaa, Mhozya alipeleka shauri mahakamani kuitaka ccm irudishe mali zote ilizopata kabla ya kuanza mfumo wa vyama vingi. Bahati mbaya mahakama ilitumia technicality kuifukuza kesi mahakamani bila kusikiliza na kuamilua kwenye merits za kesi.
 
Kuna jamaa, Mhozya alipeleka shauri mahakamani kuitaka ccm irudishe mali zote ilizopata kabla ya kuanza mfumo wa vyama vingi. Bahati mbaya mahakama ilitumia technicality kuifukuza kesi mahakamani bila kusikiliza na kuamilua kwenye merits za kesi.
Ndo kusema tunamsubiri *masiha*mwingine katika jambo hili ambaye anajua kukwepa mishale ya technicalities!
 
Jib Jibu liko wazi, mali ni ya kwao CCM. Changisheni za kwenu acheni wivu wa kike.
 
Kusingekuwa na uhuru haya ungeyaandikaje? Nenda Korea Kaskazini uandike hivi km utapata ht pa kukimbilia
 
Kuna jamaa, Mhozya alipeleka shauri mahakamani kuitaka ccm irudishe mali zote ilizopata kabla ya kuanza mfumo wa vyama vingi. Bahati mbaya mahakama ilitumia technicality kuifukuza kesi mahakamani bila kusikiliza na kuamilua kwenye merits za kesi.
Not quite true. What you are trying to say is that this property belongs to everybody. But everybody's property is nobody's property. So what do we do with it? Ni nani aliitafuta? Ni nani aliwaongoza? Ni CCM, mpe CCM. Uingereza mali yote isiyo na meenyewe ni ya Malkia.
 
Nyie mnajichetua tu,kwani hao wananchi si walikuwa wanachama wa chama cha mapinduzi?!.
 
Kipindi hicho chama kilishika hatamu dhidi ya serikali. Serikali na Chama ilikuwa kitu kimoja. Mipango yote ya chama ilitekelezwa na serikali.Kukatisha story, Mali za CCM kabla ya kuanza kwa vyama vingi, zitabaki kuwa mali za CCM. Tanzania bado ina rasimali za kutosha, vyama vya upinzani vinaweza kujitafutia mali zao pia 🤔
 
Ni mali ya CCM.
 
WAKATI WA CHAMA KIMOJA ILIKUWA SAWA LAKINI BAADA YA MFUMO WA VYAMA VINGI MALI HIZO ZINGEPELEKWA SERIKALINI CCM NA VYAMA VINGINE VITAFUTE MALI ZAO KWA RUZUKU WANAZOZIPATA
 
Mwaka 1977 mimi nilichangia shilingi 100 kwa ajili ya ujenzi wa makao makuu Dodoma na hiyo ilkuwa kwa kila mfanyakazi Tanzania nzima, bara na visiwani. Kipindi hicho mshahara wangu ulikuwa sh. 760/- take home 660 au 690 (sikumbuki vizuri) kwa hivyo 100 ilikuwa na thamani kubwa sana na ilikuwa noti kabisa.

Hata sijui zile fedha zilizokusanywa ziliishia wapi. Watu waliuliza uliza lakini enzi zile za chama kimoja ilikuwa huwezi kufika mbali.
 
Shikamoo Bibi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…