Kulea watoto na kuwa Mama wa nyumbani hakukupi Haki ya kugawana mali na mumeo pale mnapotalakiana

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Hii NI Kwa Watibeli wote. Wenye HAKI na kupenda Haki, wenye Upendo na kuupenda huo upendo, wenye Kweli na kupenda yaliyokweli, wenye Akili na kupenda maarifa na ufahamu.

Jamii yote ya viumbe wenye utashi ikiwemo binadamu ielewe kuwa Hakuna namna nyingine ya kupata Mali zaidi ya kufanya kazi kwa kuzalisha Mali.

Amri ya Mungu ya kufanya kazi ni amri ya wote. Sio amri ya mwanaume pekee au amri ya Mwanamke. Ni amri ya mtu yeyote anayetaka kumiliki mali. Sikatai zipo kazi zina nguvu ambazo haziwafai wanawake lakini hiyo haizifutí kazi zingine ambazo wanaweza kuzifanya ili kupata Mali.

Mbali na kufanya kazi, njia nyingine halali za mtu kujipatia mali ni kupewa zawadi, au kupewa urithi. Nje ya hapo hakuna njia nyingine halali ambayo mtu anaweza kupata Mali.

Kuolewa na kuwa mke sio kigezo cha kupata mali. Ndoa sio chanzo cha mapato.

Mke anayohaki ya kumiliki mali ya mumewe pale anapokuwa mke halali na mume anahaki ya kumiliki mali ya mkewe pale anapokuwa mume halali na hapo hatuzungumzii mgawanyo wa mali bali tunazungumzia familia na kwenye familia hakuna msamiati wa mgawanyo wa mali.

Mke atapata mali za mumewe, pale mumewe anapokuwa amefariki. Kama vile mume atakavyokuwa na haki ya kupata Mali za mkewe pale mkewe atakapokuwa amekufa. Wote wakiwa wanandoa. Na hapo hatutasema kuwa amegawiwa au kurithi. Bali itakuwa mali yake kwa sababu walikuwa kitu kimoja na hawakuwahi kutengana.

Ni ulaghai, dhulma kwa mume kurithisha Mali kwa watoto na kumuacha mkewe angali yu hai. Kama mke alikosa uaminifu au sababu yoyote ile ambayo inamfanya mume kutommilikisha mali basi hiyo ingetosha kumpa talaka angali yu hai ili akose sifa ya kumiliki mali zake(za mwanaume).

Kuishi na mwanamke ambaye anatambulika kama mkeo alafu kumbe unakinyongo na umeazimia kutommilikisha mali zako ni ishara kuwa aliishi maisha ya kilaghai, kinafikinafiki na hiyo ni dhulma, sio Haki, sio upendo, sio ukweli na sio Akili.

Kama Watibeli, ni haki ya mke kumiliki mali ya Mumewe kama mume alikufa wakiwa ndoani. Halikadhalika na kwa mume ni haki yake kumiliki mali ya mkewe akifa.

Mkeo akichepuka unamambo mawili ya kufanya, kumfukuza, kumpa talaka, na kama hutampa hiyo itamaanisha umemsamehe na hiyo haitakuwa fimbo ya kumnyima haki ya kumiliki mali zako pindi ukiwa haupo. Hiyo ndio Haki.

Ikiwa mkeo atakubadilikia na kutaka kukuchezea michezo ya hila au njama ili muachane kwa talaka, basi kila mtu atachukua alichochuma. Hesabu za kazi na vipato vya mtu ndani ya familia itatoa makadirio ya gawio la kila mmoja.

Ikiwa kutakuwa na njama ya mauaji ili mke amiliki Mali, ikigundulika mke hatakuwa na haki ya kumiliki mali hizo. Watoto ndio watamiliki. Ikiwa watoto ndio walifanya njama na mama yao ya mauaji ili wamiliki mali. Basi wote hawatahusishwa.
Na mali zitagawiwa kulingana na mlivyochuma.

Kisha mali za mwanaume zitaenda kwa wazazi wake. Ikiwa wazazi wake hawapo, basi zitaenda kwa Wajukuu kama wapo, ikiwa hawapo zitaenda kwa ndugu zake. Ikiwa hawapo, zitaenda kwa jamii.

Kwa upande wa mali za mke ambaye amefanya mauaji na kula njama ya kumuua mumewe na mumewe akafariki hatapata kitu. Mali zikishagawiwa kulingana na kila alichochuma mtu. Zilizomuangukia mke watapewa Wazazi wake, au watoto wake(ikiwa hawakula njama) au wajukuu wake, ikiwa wote hao hawapo. Basi zitagawiwa kwa jamii.

Kwa Watibeli Mke ni mmoja, Watibeli hawaoi mke zaidi ya mmoja. Kwa sababu hiyo ndio HAKI, UPENDO, AKILI na KWELI. Ikiwa mwanaume atachuma mali akiwa ndoani. Zile mali zitakuwa za wote, yaani mke na mume wakiwa kwenye ndoa.

Ikitokea mume akafanya hila au njama kwa namna yoyote ya kuathiri ndoa yao hiyo na ikatokea ndoa ikataka kuvunjwa basi na msababishi ni Mume, iwe kwa ku-cheat na wanawake wengine, au tamaa ya mali (kuabudu pesa) kuliko familia yake.

Talaka itatolewa lakini robo ya mali ya mume atapewa Huyo Mwanamke. Na hiyo robo ya mali haitahusisha mali za Mwanamke alizochuma. Hiyo itakuwa ni gharama za ulaghai, maumivu ya kumuumiza Mwanamke.

Ikiwa Mwanaume hajafanya kosa lolote la talaka lakini anaviashiria vya kutaka kuacha mkewe, ikiwa ni pamoja na kutompa haki mkewe kama upendo, kumjali na kumzingatia mkewe. Na akiambiwa atoe talaka hataki bali anataka Mwanamke ndiye ajichanganye ajitoe mwenyewe kwenye ndoa ili asipate chochote zaidi ya kile kilichochake basi ushahidi usiotia shaka utatolewa kwenye vyombo husika ikiwemo baraza la wazazi au ukoo, au taasisi za kidini au Serikali. Kisha itaamuliwa robo ya mali za mume apewe huyo Mwanamke bila kuzihusisha mali za Mwanamke alizochuma.

Mke na mume atakuwa na mamlaka ya kutompa au kutomrithisha yeyote mali isipokuwa wao wenyewe. Wazazi, ndugu na jamaa wa Pande zote mbili hawataki wa na haki ya kurithi wala kudai urithi kutoka kwa Mke na Mume katika ndoa fulani.

Watapewa Mali au kurithi mali kulingana na utashi na hiyari ya Wahusika. Au watapewa mali au kurithi mali katika mazingira maalumu kama Kifo kwa wahusika wote wawili, uhalifu au njama ya mauaji kwa mmoja wa wanandoa.

Watoto Watakuwa na Haki ya kurithi mali za wazazi wao kwa hiyari ya wazazi wao. Mtoto hatakuwa na haki ya kulazimisha kurithi mali ya wazazi wake ikiwa hakutajwa kwenye urithi. Mtoto atakuwa na haki ya kukataa urithi wa wazazi wake kwa hiyari na mapenzi yake na hakuna mwenye mamlaka ya kumlazimisha arithi.

Watoto wote watakuwa sawa kwenye kurithi mali za wazazi wao ikiwa wazazi hawakuacha Wosia. Wote watapewa sawa kwa sawa bila kujali tofauti zao iwe za kidini, kinasaba(mama tofauti), kielimu n.k.

Watoto wa Mwanamke ambao sio wa mwanaume husika hawatarithi mali za mwanaume ikiwa mwanaume huyo hakuwataja kwenye Wosia na hata kama akifa kwa ghafla bila kuandika Wosia. hawana haki sawa kwa sababu sio wa mwanaume huyo. Lakini watakuwa na haki ya kurithi mali za Mama yao. Kama ilivyo Watoto wa mwanaume ambao sio wa Mwanamke hawatakuwa na haki ya kurithi mali za Mama wa kambo kama mama wa kambo.

Hivyo ndivyo Watibeli tulivyo.

Acha Nipumzike sasa.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
 
Nilisha mwachia mwanamke kila kitu nilichokipata kwenye maisha yangu , kutokana na umri wangu bado nilikua mdogo nikaona nikimbie tu ili niwe na amani

Kuna mda inafika amani na furaha yako ni muhimu kuliko mali .

Mimi ni kati ya watu walioikataa ndoa kwa vitendo na sio maneno tu tena kwa maamuzi ambayo kila mtu aliniona mimi ni fala
 
Mali ziwe haki ya mke iwapo tupo pamoja au nimekufa tukiwa pamoja. Sio nimekufamania huko nakuacha unataka mali. Vile vile ukinifumania wazi wazi ukataka talaka ni sawa kupewa sehemu ya mali maana mm ndo mharibifu wa ndoa yetu.
 
Nilisha mwachia mwanamke kila kitu nilichokipata kwenye maisha yangu , kutokana na umri wangu bado nilikua mdogo nikaona nikimbie tu ili niwe na amani

Kuna mda inafika amani na furaha yako ni muhimu kuliko mali .

Mimi ni kati ya watu walioikataa ndoa kwa vitendo na sio maneno tu tena kwa maamuzi ambayo kila mtu aliniona mimi ni fala
Ukaona uokoe roho yako.
 
Mali ziwe haki ya mke iwapo tupo pamoja au nimekufa tukiwa pamoja. Sio nimekufamania huko nakuacha unataka mali. Vile vile ukinifumania wazi wazi ukataka talaka ni sawa kupewa sehemu ya mali maana mm ndo mharibifu wa ndoa yetu.

Huu ni muhtasari wa kile nilichoandika Mkuu.
 
Nilisha mwachia mwanamke kila kitu nilichokipata kwenye maisha yangu , kutokana na umri wangu bado nilikua mdogo nikaona nikimbie tu ili niwe na amani

Kuna mda inafika amani na furaha yako ni muhimu kuliko mali .

Mimi ni kati ya watu walioikataa ndoa kwa vitendo na sio maneno tu tena kwa maamuzi ambayo kila mtu aliniona mimi ni fala

Pole sana mkuu
 
Back
Top Bottom