Mali za CCM zilizotokana na makato kwa raia wote wakati wa chama kimoja ni haki ya nani?

Rwaz

JF-Expert Member
May 3, 2013
1,933
3,255
Mada yangu iko wazi wazi.

Naomba wajuvi wa mambo ya haki na umiliki, bila mahaba ya kisiasa waniweke sawa. Hivi mali zilizopatikana kwakuwakata tozo na kodi na ushuru, raia wote wakat wa chama kimoja cha CCM leo hii kwa nini wazimiliki raia wa chama kimoja?

Hapa namaanisha majumba, viwanja, maeneo ya wazi, hisa n.k. Au ni bomu linalosubiri chama kingine kikichukua nchi ndo ifanyike marekebisho!

Enzi hizo wananchi wote tulikatwa katika mauzo mbali mbali na huduma kama mazao, uvuvi, madini kupitia vyama vya msingi na beria mbali mbali.

Kuukataa ukweli ni sawa na kujificha mbuni style.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Uwanja was Mapinduzi mkoani Mbeya ulijengwa na wananchi, meaka 1984 alipofariki EDWARD MORINGE SOKOINE, uwanja ukabadilishwa jina.

Nikishangaa mwaka 1991 CCM wakatangaza kuwa ni uwanja wao.

Kuna siku raia wapenda hakiwatatambua kuwa adui yao mkubwa NI CCM, huo utakuwa ni mwanzo TU, CCM Chanzo Cha Matatizo
 
Ohoooo, shauri yako! Afadhali zamani hizo. Hivi leo hawamiliki mali tu, wanamiliki hadi watu. Hawamiliki tu sheria, wanamiliki hadi haki, Hawamiliki tu usalama wako, wanamiliki haki hewa unayopumua. Hawamiliki tu uhuru wako wa kuongea, wanamiliki hadi kile unachosikia. Wanamiliki anga na vyote vinavyopaa huko, wanamilki ardhi na vyote vinavyotembea juu yake na wanamiliki maji na vyote vinavyoogelea ndani yake. Kwa kifupi CCM wanaimiliki Tanzania na vyote vilivyomo. Halafu wewe una jeuri ya kuulizia eti viwanja, majengo na magari ni vya nani...kweli?
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Uwanja was Mapinduzi mkoani Mbeya ulijengwa na wananchi, meaka 1984 alipofariki EDWARD MORINGE SOKOINE, uwanja ukabadilishwa jina.

Nikishangaa mwaka 1991 CCM wakatangaza kuwa ni uwanja wao.

Kuna siku raia wapenda hakiwatatambua kuwa adui yao mkubwa NI CCM, huo utakuwa ni mwanzo TU, CCM Chanzo Cha Matatizo
Viwanja vyote vilipaswa kurudishwa kwa wananchi kwa kukabidhiwa Halmashauri ya maeneo husika kwa sababu ni michango ya wananchi ndio iliyojenga viwanja hivyo.
Tungekuwa mbali sana,viwanja vingekuwa sasa vina hudumiwa na Serikali kupitia Halmashauri,tungekuwa tunazungumzia namna ya kuweka viti,taa na kuweka nyasi bandia.
Mahudhurio katika michezo ingeongezeka.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom