Makosa 10 aliyotenda Mungu

Makosa 10 aliyotenda Mungu

1.KUMUUMBA SHETANI:
Hili lilikuwa kosa kubwa sana. Makosa yate yamechepuka kutoka hapa. Shetani anawasababishia watu maovu, then Mungu anawahukumu watu dhaifu. Hapa Mungu inambidi amkamate shetani na kumtokomeza ili maovu yaishe, kama wote wanatoshana nguvu basi wasuluhishe ugomvi wao na kupatana ili maisha yawe ya amani.

2.KUISHI MAFICHONI:
Toka enzi na enzi, Mungu amekuwa akiishi mafichoni, kwanini asijitokeze na kujionesha kwa viumbe vyake? Anaishi mafichoni kwani yeye ni Joseph Kony? Hili limepelekea watu wake kudanganywa na manabii wa uongo na kutapeliwa bure. God come from your hidings and reveal yourself to your people.

3.MAFURIKO YA WAKATI WA NUHU:
Mungu alisababisha mafuriko ili kuangamiza watu waovu na kubakiza watu wema, Yes he did, sasa waovu wa leo wametoka wapi? mbona aliuwa watu wengi bila huruma? Kama mafuriko yalikuwa ni suluhisho la maovu, Yesu na mitume walijia nini? It seems he fought effects instead of causes.

4.SAFARI YA WANA WA ISRAELI:
Mungu aliwatoa wana wa Israel kutoka Misri kwa madai ya kuwapa nchi ya ahadi, matokeo yake aliwaamuru wafanye uvamizi wa nchi za watu(mf. waamori, wamoabu na wakanani). Kwanini asingebadilisha jangwa na kuwatengenezea waisraeli nchi yao? mbona Gadaffi aliweza? Imagine waje wapuuzi hapa TZ wachukue nyumba na ardhi kwa madai kwamba wameagizwa na Mungu, ungereact vipi? WE HAVE TO BE FAIR!

5.KUTOTIMIZA AHADI YAKE KWA ABRAHAM:
Mungu alimwambia Abraham kuwa atampatia uzao wa wana wengi kama nyota za angani au mchanga wa pwani. Sasa hivi ukichanganya walio wa Abrahamu na wasiyo wa kwake bado watu hawawezi kuwa sawa na nyota au mchanga wa pwani. Ata ukijumlisha na waliokufa back to Adam. Atatimiza lini hi ahadi? je kuna muda wa kutosha? mbona watumishi wake wanasema Yesu yuu karibu kuja ili kutamatisha nyakati?

6.KUWEPO KWA MZIO(ALLERGY):
Kwanini watu wengi ambao ni wema wana allergy na vitu alivyoumba Mungu? mbona maandiko yanasema kila alichoumba Mungu ni chema? Kwanini aumbe mimea na wanyama wenye sumu kwa watu wake awapendao? au hakujua?

7.MAJANGA ASILIA:
Kama Mungu aliumba dunia ili iwe sehemu ya amani kwa watu wake na wamwabudu yeye, kwanini kuna matetemeko ya nchi, vimbunga na mafuriko. Kwanini anawauwa watu kikatili hivi? au haya nayo tumsingizie shetani?

8.KUUMBA VIUMBE HATARISHI:
Kwanini Mungu aumbe bacteria, virusi, fangasi na viumbe wengine wanaosababisha magonjwa na kifo? Kwanini hawa viumbe wasingefia kwenye yale mafuriko ya Nuhu ili watu wema alio wabakiza waishi kwa amani? Je hawa viumbe hatari Mungu alimwamuru Nuhu awaingize wawili wawili kwenye safina?

9.JEHANAMU NA MOTO WAKE:
Kwanini Mungu aumbe jehanamu kuteketeza waovu? Kwani hajui kusamehe? Kwanini huruma yake ina kikomo kwa shetani? Kama wewe ni mzazi, mwanao akikukosea na hajaomba msamaha, itabadilisha uhalisia kuwa yule sii mwanao? SHETANI PAMOJA NA WAOVU NI KAZI YA MIKONO YAKE, PRODUCTS OF HIS OWN MIND BEFORE CREATED THEM. So aache kuweka vinyongo na kutamani kulipiza kisasi juu ya kazi yake.

10.KASORO KWENYE MWILI WA BINADAMU:
Kwanini pawepo na mabadiliko hasi kwenye jeni za binadamu(mutation)? kwani hakujua hicho ni chanzo cha viwete??? Kidole tumbo(appendix) ni cha kazi gani? mbona hajatoa maelezo namna ya kukitumia? Na chuchu za mwanaume ni za kazi gani?

TO THE RIGHT WING OR THE LEFT WING WE ARE NEITHER, NOT EVEN AT THE MIDDLE....R.I.P MOBUTU!

===================
Ni kufuru kubwa kunena kuwa mungu amekosea na hii ni kwa dini zote
 
Kama wewe hujaweza kuthibitisha Mungu wako yupo na anayeamini mavi yake ni Mungu naye hajaweza kuthibitisha mavi yake ni Mungu, wote mmeshindwa kuthibitisha mnachosema ni Mungu ni Mungu kweli.

Sasa katika hilo mna tofauti gani?
Tunatofautiana kwenye maana ya neno Mungu.
 
Hiyo ni imani potofu na uongo.

Unaelewa hilo?
Usichokiamini lazima kiwe uwongo kwako,usichotambua wewe ni kuwa msimamo wako wa kuwa hakuna Mungu hautokani na hizi sababu unazotoa humu na hivyo mtu kusema kuwa kuna Mungu ni imani potofu kwako.
 
"Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako;
kumpenda BWANA, Mungu wako, kuitii sauti yake, na kushikamana naye; kwani hiyo ndiyo uzima wako..."
~ KUMB 30:19-20
 
Usichokiamini lazima kiwe uwongo kwako,usichotambua wewe ni kuwa msimamo wako wa kuwa hakuna Mungu hautokani na hizi sababu unazotoa humu na hivyo mtu kusema kuwa kuna Mungu ni imani potofu kwako.
Unajua kuna tofauti kati ya "uongo" na "uongo kwako"?

Why are you shifting goals?
 
"Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako;
kumpenda BWANA, Mungu wako, kuitii sauti yake, na kushikamana naye; kwani hiyo ndiyo uzima wako..."
~ KUMB 30:19-20
Thibitisha Mungu yupo.
 
Umeandika fuupi halafu haijaonesha upuuzi mtupu upo wapi, kwa nini ni upuuzi mtupu, na kwa nini wewe uliyeandika huu ni upuuzi mtupu usiwe ndiye umeandika upuuzi mtupu.
Hahahaaaaaa
 
10. Chuchu za Mwanaume za kazi gani?
Hili kweli swali fikirishi inabidi sayansi iingilie hapa....
 
Ukisoma wataalam wa kusoma Biblia kama James L Kugel, profesa aliyefundisha mpaka Harvard masomo ya Biblia, anasema Biblia ni kitabu kilichoandikwa na watu tu, kimefutwa futwa mara nyingi na kubadilishwa sana, na ni hadithi za Wayahudi tu, kwa hiyo si kitu cha kusoma kama habari za ukweli.

Ni kama sisi tuanze kuandika habari za kina Shaka Zulu na Mwanamalundi tuwafanye mitume.
Nakubali kwa asilimia zote biblia is just as illusion thing hadi kuraan vyote ni uzushi tup
 
Tatizo nikwamba Uaminifu wetu kuhusu Mambo Ya Mungu, Musingi wake ni kutoka Wazazi Wetu !!..... Haya Makosa ya Biblia, tumeyakuta leo baada ya kukua na kua na Hakili timamu !!.... Tujilaumu sisi ao tulaumu wazazi wetu !,.... Tukibadili Mtazamo wetu kuhusu Mungu, ni Upotoshaji mkubwa sana !!.... na mwisho we Tutapotea njia !!
 
Back
Top Bottom