Makosa 10 aliyotenda Mungu

Makosa 10 aliyotenda Mungu

Kwa wingi wa rehema nakuandikia maswali ambayo yanaulizwa mara nyingi na majibu yake kutoka kwangu.

1.Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote aliyeumba ulimwengu huu ndiye anaaminiwa na watu wengi kabisa kuwa yupo. Quran, Biblia, dini nyingi, falsafa zinamtaja huyu.

2. Mungu huyu yupo kweli?

Tukiangalia kimatiki, dhana ya Mungu huyu kuwapo ina tatizo la kimantiki, kubwa sana.

3.Tatizo gani la kimantiki?

Tatizo hilo ni kwamba, dhana ya kuwepo Mungu huyu inajipinga yenyewe.
.
4. Dhana hii inajipingaje?

Dhana hii inajipinga kwa sababu tunaambiwa, upande mmoja, Mungu ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, hana sababu ya kimantiki kuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana kuwepo, dhambi inawezekana kuwepo, matetemeko ya ardhi yanawezekana kuwepo, magonjwa yanawezekana kuwepo, kifo kinawezekana kuwepo, tsunami linawezekana kuwepo n.k, halafu upande wa pili tunaambiwa Mungu kauumba ulimwengu uwe unaruhusu mabaya hayo.

Huku ni kujipinga kusiko kwa kiungu. Ni kama mtu anakwambia kwamba katika jometri ya Euclid, duara haliwezi kuwa pembetatu, halafu akakuambia kuna pembetatu iliyo duara.

Ama amaekosea kusema pembetatu haiwezi kuwa duara, ama amekosea kusema kwamba kuna duara iliyo pembetatu.

Hawezi kuwa sawa pote.

5. Vipi kuhusu habari kwamba Mungu hakutaka ulimwengu uwe na mabaya, ila shetani, uasi, dhambi ndizo zilifanya dunia iwe na mabaya?

Hilo litamaanisha Mungu aliumba ulimwengu unaoruhusu uasi, dhambi, ubaya kuwea kuwepo, kwa nini?

6. Vipi kuhusu habari kwamba Mungu aliruhusu ubaya uweze kuwepo ili watu wawe na uchaguzi na uhuru?

Kwanza kabisa kwa nini uhuru na uchaguzi uwe muhimu kuliko kutokuwepo kwa mabaya?
Ukiwa na mtoto mchanga ambaye hana ujuzi sana, utampa maziwa na sumu ili tu awe na uhuru wa kuchagua? Hapana, utampa maziwa na kuficha sumu asiweze kuifikia. Sasa kwa nini Mungu katuachia watoto wake tuifikie sumu? Kwa nini hakuificha?

Pili, si kweli kwamba tuna uhuru wa kuchagua. Hatuchagui wazazi wetu, hatuchagui kabila letu, hatuchagui tutazaliwa wapi, hatuchagui tutazaliwa lini, hatuchagui tutakuwa na genes gani, hatuchagui tutakufa lini, hatuchagui tuzaliwe au tusizaliwe.

Hii habari ya kwamba tuna uhuru wa kuchagua mema na mabaya ni uongo. Kuna mengine yana mizizi katika genes, mengine ni sehemu ya socioeconomic background.

Tatu, kuna mabaya mengi hayahusiani kabisa na habari za uchaguzi wa mazuri na mabaya, mabaya kama majanga ya kiasili hayana uhusiano wowote na uchaguzi wa mazuri na mabaya.

7. Vipi kuhusu maandiko matakatifu yanayosema Mungu yupo?

Maandiko matakatifu ni jitihada za watu tu kujipangia maisha yao kwa namna inayoeleweka kwao, mengi yana mafundisho mazuri, lakini sehemu nyingi tunaona yanajipinga, yanatetea mabaya, yanaonesha kwamba yameandikwa na watu tu, kuhusu Mungu ambaye hayupo

8. Mbona watu wengi wanaamini kuwepo kwa Mungu?

Kwanza kabisa, habari ya kwamba watu wengi wanaamini kuwepo kwa Mungu ina mushkeli. Watu wengi wangeamini kweli kuwepo kwa huyu Mungu, ujambazi, uuaji, wizi, utapeli, dhambi nyingi sana zisingekuwepo. Kuwepo kwa mabaya haya kwa sana duniani kunaonesha watu wanapenda kujinadi kwamba wanaamini kuwepo kwa Mungu, lakini ndani kabisa, ama wanakubali kwamba hawajui vizuri habari hii au wanaikataa kabisa.

Pili, ulimwengu unatoka katika zama za ujinga na kwenda kwenye zama za elimu na maenddeleo ya habari.Kitu kuaminiwa na watu wengi hakuoneshi kitu hicho ni kweli. Kuna wakati watu waliamini jua linazunguka dunia, lakini sasa watu wengi wamejua dunia ndiyo inazunguka jua. Kwa hiyo kitu kuaminiwa na watu wengi hakumaanishi kuwa kitu hicho ni kweli.

9. Kama Mungu hayupo, ulimwengu umeanzaje? Unaweza kujibu swali hili ili kuonesha kwamba Mungu hayupo?

Sijui. Habari iliyo karibu zaidi kutueleza kuhusu mwanzo wa ulimwengu ni kuunganisha Albert Einstein's Relativity na Quantum Theory kupata theory mpya ya Quantum Gravity. Kwa sasa hatujaweza kupata mahesabu ya kuweza kuondoa singularities fulani.

Lakini hata kama naishia kusema tu sijui jibu la swali hili kimsingi, kutokujua huko hakuna maana kwamba sitajua jibu la uongo.

Nikijua kwamba square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko 2, mtu akiniambia square root ya 2 ni 10 (ambayo ni kubwa kuliko 2), nitajua 10 si square root ya 2 hata kama sijui square root ya 2 ni nini.

Kijana wa miaka 20 akiwa hamjui mama yake mzazi, akajua mama yake mzazi ni lazima awe na umri wa zaidi ya miaka 20 (ili aweze kuwa amemzaa) halafu akaoneshwa mtoto kike wa miezi mitatu, akaambiwa huyu ndiye mama yako mzazi, atajua huyu si mama yake mzazi, bila hata kumjua mama yake mzazi ni yupi.

Kukubali Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote ndiye aliyeumba ulimwengu huu wenye kuweza kuwa na mabaya ni sawa na kukubali mtoto wa miezi mitatu ni mama mzazi wa mtu mwenye miaka 20

10. Sasa tufanye nini?

Tujifunze zaidi, tuchunguze zaidi, tutafute ukweli bila kupenda majibu rahisi rahisi. Tukubali majibu ya kweli hata kama hatuyapendi.

Majibu ya uongo ambayo ni wazi kabisa hayana logical consistency, tuyakatae.

*Angalizo, hapa naongelea umuhimu wa ujuzi, kwa misingi ya mantiki na ukweli. Sizungumzii imani per se. Imani ni sehemu muhimu ya utu na watu wanaruhusiwa kuamini wanavyotaka. Katiba ya nchi na mazimio ya kimataifa yanaruhusu uhuru wa kuabudu.
Asante sana mkuu kwa hii Comment
 
Inawezekana ikawa kweli.

Lakini, hilo nalo linahitaji uchunguzi zaidi.

Ukisoma quantum physics na relativity utaona hata muda si kitu ambacho kipo kama kitu cha msingi kabisa.

Relativity inasema upimaji wa muda unategemea na mtazamaji alipo. Qquantum physics inasema muda upo quantized, unaweza kuukata ukafika kusiko na muda huko chini.

Kwa muale wa mwanga unaoenda kwa spidi ya mwanga, muda umesimama, mambo yote yaliyopita, yaliyopo na yajayo, yanatokea kwa wakati mmoja huo huo. Muale wa mwanga hauna muda unaopita.

Muda ni mazingaombwe unayoyaona wewe kwa sababu huwezi kwenda kwa spidi ya mwanga.

Na causality - habari ya kwamba jambo la mwanzo linapelekea kuwepo jambo linalofuatia- si kitu cha lazima kabisa katika level fulani ya ulimwengu.

Kwa hiyo, kwenye macroscopic world huku, mambo yana vyanzo.

Ukirudi chini kwenye Planck scale huko, hata muda haupo. Hivyo mambo hayana chanzo, au, si lazima mambo yawe na chanzo hususan, kwa sababu ili mambo yawe na chanzo, inabidi muda wa kufanya kimoja kitokee kabla ya kingine uwepo.

Kuna mambo mengi sana hatujui, na hatutakiwi kuanza kutoa majibu kabla hatujachunguza na kujua.
Mzee kiranga hii post ni nzito sana
 
Mzee kiranga hii post ni nzito sana
Hiyo kuielewa vizuri mpaka usome Albert Einstein's Relativity halafu ufuatilie malumbano ya Einstein na Niels Bohr.

Halafu umfuatilie Einstein alipoanzia mpaka yalipomshinda. Umsome Bohr naye Copenhagen interpretation. Uwasome Heisenberg, Schrodinger, Dirac, Fermi, Oppenheimer, Wheeler, Everett, Pauli, Feynman, Hawkings, Penrose et cetera. Na malumbano yao wote.

Sasa watu wanabisha wengine hata hayo majina hawayajui.

Licha ya kuwasoma na kujua dunia inaendaje.

Shida sana kubishana kwa fact hapo.
 
Kwa wingi wa rehema nakuandikia maswali ambayo yanaulizwa mara nyingi na majibu yake kutoka kwangu.

1.Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote aliyeumba ulimwengu huu ndiye anaaminiwa na watu wengi kabisa kuwa yupo. Quran, Biblia, dini nyingi, falsafa zinamtaja huyu.

2. Mungu huyu yupo kweli?

Tukiangalia kimatiki, dhana ya Mungu huyu kuwapo ina tatizo la kimantiki, kubwa sana.

3.Tatizo gani la kimantiki?

Tatizo hilo ni kwamba, dhana ya kuwepo Mungu huyu inajipinga yenyewe.
.
4. Dhana hii inajipingaje?

Dhana hii inajipinga kwa sababu tunaambiwa, upande mmoja, Mungu ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, hana sababu ya kimantiki kuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana kuwepo, dhambi inawezekana kuwepo, matetemeko ya ardhi yanawezekana kuwepo, magonjwa yanawezekana kuwepo, kifo kinawezekana kuwepo, tsunami linawezekana kuwepo n.k, halafu upande wa pili tunaambiwa Mungu kauumba ulimwengu uwe unaruhusu mabaya hayo.

Huku ni kujipinga kusiko kwa kiungu. Ni kama mtu anakwambia kwamba katika jometri ya Euclid, duara haliwezi kuwa pembetatu, halafu akakuambia kuna pembetatu iliyo duara.

Ama amaekosea kusema pembetatu haiwezi kuwa duara, ama amekosea kusema kwamba kuna duara iliyo pembetatu.

Hawezi kuwa sawa pote.

5. Vipi kuhusu habari kwamba Mungu hakutaka ulimwengu uwe na mabaya, ila shetani, uasi, dhambi ndizo zilifanya dunia iwe na mabaya?

Hilo litamaanisha Mungu aliumba ulimwengu unaoruhusu uasi, dhambi, ubaya kuwea kuwepo, kwa nini?

6. Vipi kuhusu habari kwamba Mungu aliruhusu ubaya uweze kuwepo ili watu wawe na uchaguzi na uhuru?

Kwanza kabisa kwa nini uhuru na uchaguzi uwe muhimu kuliko kutokuwepo kwa mabaya?
Ukiwa na mtoto mchanga ambaye hana ujuzi sana, utampa maziwa na sumu ili tu awe na uhuru wa kuchagua? Hapana, utampa maziwa na kuficha sumu asiweze kuifikia. Sasa kwa nini Mungu katuachia watoto wake tuifikie sumu? Kwa nini hakuificha?

Pili, si kweli kwamba tuna uhuru wa kuchagua. Hatuchagui wazazi wetu, hatuchagui kabila letu, hatuchagui tutazaliwa wapi, hatuchagui tutazaliwa lini, hatuchagui tutakuwa na genes gani, hatuchagui tutakufa lini, hatuchagui tuzaliwe au tusizaliwe.

Hii habari ya kwamba tuna uhuru wa kuchagua mema na mabaya ni uongo. Kuna mengine yana mizizi katika genes, mengine ni sehemu ya socioeconomic background.

Tatu, kuna mabaya mengi hayahusiani kabisa na habari za uchaguzi wa mazuri na mabaya, mabaya kama majanga ya kiasili hayana uhusiano wowote na uchaguzi wa mazuri na mabaya.

7. Vipi kuhusu maandiko matakatifu yanayosema Mungu yupo?

Maandiko matakatifu ni jitihada za watu tu kujipangia maisha yao kwa namna inayoeleweka kwao, mengi yana mafundisho mazuri, lakini sehemu nyingi tunaona yanajipinga, yanatetea mabaya, yanaonesha kwamba yameandikwa na watu tu, kuhusu Mungu ambaye hayupo

8. Mbona watu wengi wanaamini kuwepo kwa Mungu?

Kwanza kabisa, habari ya kwamba watu wengi wanaamini kuwepo kwa Mungu ina mushkeli. Watu wengi wangeamini kweli kuwepo kwa huyu Mungu, ujambazi, uuaji, wizi, utapeli, dhambi nyingi sana zisingekuwepo. Kuwepo kwa mabaya haya kwa sana duniani kunaonesha watu wanapenda kujinadi kwamba wanaamini kuwepo kwa Mungu, lakini ndani kabisa, ama wanakubali kwamba hawajui vizuri habari hii au wanaikataa kabisa.

Pili, ulimwengu unatoka katika zama za ujinga na kwenda kwenye zama za elimu na maenddeleo ya habari.Kitu kuaminiwa na watu wengi hakuoneshi kitu hicho ni kweli. Kuna wakati watu waliamini jua linazunguka dunia, lakini sasa watu wengi wamejua dunia ndiyo inazunguka jua. Kwa hiyo kitu kuaminiwa na watu wengi hakumaanishi kuwa kitu hicho ni kweli.

9. Kama Mungu hayupo, ulimwengu umeanzaje? Unaweza kujibu swali hili ili kuonesha kwamba Mungu hayupo?

Sijui. Habari iliyo karibu zaidi kutueleza kuhusu mwanzo wa ulimwengu ni kuunganisha Albert Einstein's Relativity na Quantum Theory kupata theory mpya ya Quantum Gravity. Kwa sasa hatujaweza kupata mahesabu ya kuweza kuondoa singularities fulani.

Lakini hata kama naishia kusema tu sijui jibu la swali hili kimsingi, kutokujua huko hakuna maana kwamba sitajua jibu la uongo.

Nikijua kwamba square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko 2, mtu akiniambia square root ya 2 ni 10 (ambayo ni kubwa kuliko 2), nitajua 10 si square root ya 2 hata kama sijui square root ya 2 ni nini.

Kijana wa miaka 20 akiwa hamjui mama yake mzazi, akajua mama yake mzazi ni lazima awe na umri wa zaidi ya miaka 20 (ili aweze kuwa amemzaa) halafu akaoneshwa mtoto kike wa miezi mitatu, akaambiwa huyu ndiye mama yako mzazi, atajua huyu si mama yake mzazi, bila hata kumjua mama yake mzazi ni yupi.

Kukubali Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote ndiye aliyeumba ulimwengu huu wenye kuweza kuwa na mabaya ni sawa na kukubali mtoto wa miezi mitatu ni mama mzazi wa mtu mwenye miaka 20

10. Sasa tufanye nini?

Tujifunze zaidi, tuchunguze zaidi, tutafute ukweli bila kupenda majibu rahisi rahisi. Tukubali majibu ya kweli hata kama hatuyapendi.

Majibu ya uongo ambayo ni wazi kabisa hayana logical consistency, tuyakatae.

*Angalizo, hapa naongelea umuhimu wa ujuzi, kwa misingi ya mantiki na ukweli. Sizungumzii imani per se. Imani ni sehemu muhimu ya utu na watu wanaruhusiwa kuamini wanavyotaka. Katiba ya nchi na mazimio ya kimataifa yanaruhusu uhuru wa kuabudu.
Hakuna anayesema suala la uwepo wa Mungu sio imani,kwa maana nyengine suala la uwepo wa Mungu ni suala la imani ndiyo iko hivyo.

Sasa wewe kama unapinga kuwepo kwa Mungu, basi ni kwamba unapinga hii imani ya kwamba kuna Mungu na si vinginevyo kwa hivyo utajua mwenyewe unapinga kwa kutumia nini hilo haijarishi ila hili jambo ni la imani.

Najua unaliondoa hili jambo kwenye imani ili mwishoni uweze kusema hakuna anayeweza kuthibitisha kuwa Mungu yupo na kutumia kama silaha yako ya mwisho.
 
Unajuaje kwamba sijaondoa mjadala huu kwenye suala la imani ili kuwapa nafasi ya faragha yao wanaotaka kuamini tu, bila mjadala?
 
Kama mwanadamu kwa kutumia akili ya ubongo wake anashindwa tu kuulewa mwili wake vizuri mpka leo hii karne ya 21, sembuze atawaweza kumuelewa MUNGU ambaye haonekani kwa kutumia ubongo huo huo!?..

Msijichoche bure. Akili ya mwanadamu ipo LIMITED.
 
Asiyetaka mjadala hatojadili na ni haki yake ila suala la uwepo wa Mungu ni imani,kuliondoa hili na kuliweka pengine unavuruga hata mjadala wenyewe.
 
In logic, we call this "a priori" fallacy.

3.1a

The a priori - fallacy occurs when someone decides ahead of time what the conclusion to an argument is, then only considers evidence that supports that conclusion, or twists what evidence there is to support the predetermined conclusion.

In divine science we call the disease you suffer as a " DEITY BLINDNESS "

Like "colour blindness" from which a man eyes can not distinguish colours despite their presence, the deity blindness is the disability one suffers from, in which he/she is unable to realise the presence of God despite the existence of His distinguishing clear signs.

The existing calamities and disasters in the world have mistakenly been taken as a yard stick to deny God existence, if that's the case, then what can you say about the existing blissful luxurious life men lead in the world ??!!

From your argument viz, God does not exist only because we suffer from the calamities and disasters, then its reverse argument proves God existence ,😁😁

You happen to be in this world unwillingly therefore you must abide by the trials and tribulations and you have to exercise your mental power wisely to understand the wisdom behind your making and the environment in which you live, don't be arrogant and proud of yourself as arrogance and pride are diseases which blur one understandings of things let alone the divine science which is by far tough for our minds unless we implore for help from God Himself.

You being one among creatures in this world, the wisdom has it that there should be a creator around the disciplined creatures and universe. The law is, having a Creature there must be a Creator.

I beseech you Confess the existence of God by exercising your intelligence fully while seeking His assistance lest may come a time you will publicly and forcibly confess His existence in this very forum (Jf) in which you deny Him and you will realise His greatness in agony.
 
Kama mwanadamu kwa kutumia akili ya ubongo wake anashindwa tu kuulewa mwili wake vizuri mpka leo hii karne ya 21, sembuze atawaweza kumuelewa MUNGU ambaye haonekani kwa kutumia ubongo huo huo!?..

Msijichoche bure. Akili ya mwanadamu ipo LIMITED.
Katika logic hii tunaita "non sequitur fallacy"
 
In divine science we call the disease you suffer as a " DEITY BLINDNESS "

Like "colour blindness" from which a man eyes can not distinguish colours despite their presence, the deity blindness is the disability one suffers from, in which he/she is unable to realise the presence of God despite the existence of His distinguishing clear signs.

The existing calamities and disasters in the world have mistakenly been taken as a yard stick to deny God existence, if that's the case, then what can you say about the existing blissful luxurious life men lead in the world ??!!

From your argument viz, God does not exist only because we suffer from the calamities and disasters, then its reverse argument proves God existence ,😁😁

You happen to be in this world unwillingly therefore you must abide by the trials and tribulations and you have to exercise your mental power wisely to understand the wisdom behind your making and the environment in which you live, don't be arrogant and proud of yourself as arrogance and pride are diseases which blur one understandings of things let alone the divine science which is by far tough for our minds unless we implore for help from God Himself.

You being one among creatures in this world, the wisdom has it that there should be a creator around the disciplined creatures and universe. The law is, having a Creature there must be a Creator.

I beseech you Confess the existence of God by exercising your intelligence fully while seeking His assistance lest may come a time you will publicly and forcibly confess His existence in this very forum (Jf) in which you deny Him and you will realise His greatness in agony.
Hujaelewa hata argument yangu ikoje, hivyo, huwezi kuijibu.

Nikikupa glasi nusu ina maji, nusu ina mkojo wangu, nikakwambia kunywa, glasi ina maji safi, huwezi kusema ina mkojo, ukisema ina mkojo nitakwambia ina maji safi pia, utakunywa hayo maji yaliyochanganyika na mkojo?

Mungu wako alishindwa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezi kufanyika wala kufikirika?
 
Na mimi hunielewi, kama nikikupa kiloba cha ugali na kiloba cha mavi ya nguruwe utachagua kipi kula?
 
Asiyetaka mjadala hatojadili na ni haki yake ila suala la uwepo wa Mungu ni imani,kuliondoa hili na kuliweka pengine unavuruga hata mjadala wenyewe.
Hujajibu swali nililokuuliza, swali ulilojibu sijakuuliza.

Unajuaje kwamba sijaondoa mjadala huu kwenye suala la imani ili kuwapa nafasi ya faragha yao wanaotaka kuamini tu, bila mjadala?
 
Hujaelewa hata argument yangu ikoje, hivyo, huwezi kuijibu.

Nikikupa glasi nusu ina maji, nusu ina mkojo wangu, nikakwambia kunywa, glasi ina maji safi, huwezi kusema ina mkojo, ukisema ina mkojo nitakwambia ina maji safi pia, utakunywa hayo maji yaliyochanganyika na mkojo?

Mungu wako alishindwa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezi kufanyika wala kufikirika?

Kwanza hoji imekuaje wewe ukaja duniani bila hiyari yako, ukishapata jibu ndipo uje kuuliza kwanini hizo shida na matatizo yanawapata watu?, pia usisahau kujiuliza raha na starehe pia wanazokula "matajiri".😁😁
 
duu ih mada inatisha saiz naanza kuelewa kwann tunakatazwa kumjua God pia kwann zaman vitabu vyeny habar za God vilikuw vinasomw na wachache
 
Hujajibu swali nililokuuliza, swali ulilojibu sijakuuliza.

Unajuaje kwamba sijaondoa mjadala huu kwenye suala la imani ili kuwapa nafasi ya faragha yao wanaotaka kuamini tu, bila mjadala?
Kama unaona sijajibu ulichouliza basi pengine ni kutokana na kukosea kwako kukosea kuuliza,lichunguze vizuri swali lako.
 
Back
Top Bottom