Makosa 10 aliyotenda Mungu

Makosa 10 aliyotenda Mungu

Sijamdhihaki nimesema kweli. Kwani kuna uongo hapo??

Sisi ni wazambi ambao tukimuona Mungu twaweza kufa ko ni vizur sana Mungu kutoonekana kwetu ,pili ikumbkwe Mungu alimuumba lucifa akiwa kamilifu asye na dhambi kwakuwa Mungu amewapa Uhuru viumbe wake ndo chanzo cha uasi
 
Umenielewa kweli? Nimekuuliza kulikuwa na haja gani ya kutunga kwa kuandika maelezo yote yale yaliyo kwenye kitabu cha biblia?

Kwa sababu sioni haja kutunga maelezo yote yale ili tu waseme ni maneno ya Mungu,kwako wewe linaingia akilini jambo hilo? Ndio maana nikakuuliza baada ya kumsoma huyo sijui James,je maelezo yako wewe ni yapi?
Akijibu kiusahihi nitag
 
Shida yako unataka uthibitishiwe kuwa Mungu yupo katika njia unayoitaka wewe (preconceived way). Mtu akikuthibitishia kinyume cha hivyo unavyotaka unashindwa kumuelewa/hutaki kumuelewa.

Na jambo la muhimu ni kwamba thibitisha wewe mwenyewe umetoka wapi? na baada ya hapo ndipo uulize mambo mengine kama yanayohusu uwepo wa Mungu nk.

Au ulitaka umuone Mungu akiwa na ofisi yake amekaa kitini na juu ya meza kuna mafaili mbalimbali, pembeni kukiwa Mihuri, kompyuta,simu ya mezani,jokofu lililojaa vinywaji baridi na meza ndogo juu yake kuna chupa ya chai nk, hapo ndipo ungeamini kuwa YEYE yupo!!!??. A Very, very absurd notion.
Hapa umemaliza Mkuu...

huyu Kiranga (na wenzake) wanashabihiana na watata wa zamani hizo waliokuwa wanawadai na kuwataka mitume kuthibitisha uwepo wa Mungu kwa namna wanavyotaka wao.

Sasa mtu anasema kuwekwe ngazi malaika wawe wanapanda na kushuka ardhini na mbinguni wakionekana na watu nao watumie hiyo ngazi kwenda kumface Mungu; sasa sindo uchizi huu
 
Mkuu hapo mbn umeweka vitisho,,,juzi Hapo raisi wa philipino alisikika akisema "kwa yeyote atakae nithibitishia kua mungu yupo kwa kupiga selfie na mungu niko niko tayali kujiuzuru" but nothing happened to him alaf kwenye hiyo hoja yako ya namba nne huyo aliyetengeneza titanic mungu alichukia kwa maneno ya dhihaka akaamua kuzamisha meli na kuua watu wengine kwa ajili ya dhihaka ya mtengeneza meli yani nisawa namm niwe na ugomvi na ww alafu nije nilete vurugu hadi kwa watoto zako wasio na hatia
Duterte yeye matusi dharau na kebehi zake ni juu ya Wakatoliki na anasema kabisa Wakotoliki wamletee picha ya Mungu wao. Kwahiyo huenda yeye anaamini Mungu yupo lakini kwa namna/mfumo/dini nyingine tofauti na Wakatoliki sio kama nyinyi ambao mnamtukana Mungu in general (MwenyeziMungu )

Kwani mara ngapi tunawasikia Wakrist wakimtukana (Allah) Mungu wa Waislam, na Waislam nao kinyume chake na wengi wengineo kwa mfumo huo.

N. B
Sikusudii kumtetea huyo Mfilipino (mana wote ndio walewale- wote ndo nyinyi) lakini nimetaka tu kuweka sawa hiyo hoja mana naona kama mmeshupaa kwayo.
 
Hutaki kukiri kwamba hiyo hoja yake ya msingi kupinga uwepo wa Mungu ndiyo baseless, kwa sababu kama shida na taabu ni kigezo cha kutokuwepo Mungu, sasa utasema nini juu ya raha na starehe zilizopo??, bila shaka, kulingana na msingi wa hoja yake Mungu atakuwepo kwa sababu ya raha na starehe zilizopo!!, na ndiyo maana nasema yeye amekurupuka tu bila kufanya tathmini ya kina kabla hajatoa hiyo hoja kwa sababu hata mwenye akili ndogo ataona hiyo hoja ikijipinga yenyewe kabla haijapingwa na mtu. (THE SELF CONTRADICTORY ARGUMENT).

Tafuteni hoja zingine na kamwe hamtapata kwa sababu hamjui mpo hapa duniani kwa sababu ipi na nani kawaleta?, na wala hamkuja kwa hiyari yenu halafu leo mnakuwa washindani na wajuvi kana kwamba mmejiumba wenyewe.


NANI KAMA MUNGU?
Hakuna kama MwenyeziMungu
 
kisicho kuwepo hakithibitiki huwezi kukithibitisha kwa kuwa hakipo wewe unayesema kipo ndio unayetakiwa ukithibitishe kama kipo
Usinikumbushe ya Mark Angel

Kama ni hivyo na wewe huna akili kwa kwa kuwa huwezi kuthibitisha kama ipo pia umeamini hao wanasayansi wakati hukuwahi kuwathibitisha uwepo wao (hao uliosoma proofs zao za kutokuwepo kwa Mungu )
 
Usinikumbushe ya Mark Angel

Kama ni hivyo na wewe huna akili kwa kwa kuwa huwezi kuthibitisha kama ipo pia umeamini hao wanasayansi wakati hukuwahi kuwathibitisha uwepo wao (hao uliosoma proofs zao za kutokuwepo kwa Mungu )

Kosa alilofanya mungu ni kijikanyaga mwenyewe hana msimamo kama yupo mmoja ni jibu yafuatayo:-

Je ni mungu gani huyo je ni allah au yehova au marduku au adonai au zeus au budha?

Kama ni mmoja mbona anatuma watu wenye mafundisho tofauti?

Na yehovah na allah hawafanani na hawatakuja kufanana? Je original mungu mwenyewe kati ya hao wawili ni yupi?

Nani aliumba ulimwengu kati ya hao wawili ?

Mbona ukiomba kwa kila mungu unafanikiwa? mfano mkristo hana haja ya kumjua allah wakati yehova na yesu ndio kila kitu na muislam hana haja ya kumjua yehova wakati allah na muhammad ndio kila kitu kwake

Ukishindwa kujibu hayo maswali unanithibitishia mungu wako hayupo na tena hana msimamo
 
Kosa alilofanya mungu ni kijikanyaga mwenyewe hana msimamo kama yupo mmoja ni jibu yafuatayo:-

Je ni mungu gani huyo je ni allah au yehova au marduku au adonai au zeus au budha?

Kama ni mmoja mbona anatuma watu wenye mafundisho tofauti?

Na yehovah na allah hawafanani na hawatakuja kufanana? Je original mungu mwenyewe kati ya hao wawili ni yupi?

Nani aliumba ulimwengu kati ya hao wawili ?

Mbona ukiomba kwa kila mungu unafanikiwa? mfano mkristo hana haja ya kumjua allah wakati yehova na yesu ndio kila kitu na muislam hana haja ya kumjua yehova wakati allah na muhammad ndio kila kitu kwake

Ukishindwa kujibu hayo maswali unanithibitishia mungu wako hayupo na tena hana msimamo
Kwanza kwanini unazungumzia hao wawili tu(hujawataja na miungu ya wahindi na wachina huko) na wakati umesema hawafanani na hawatofanana? Kipi kinafanya uwazungumzie hao wawili na kutaka kujua yupi wa kweli?
 
Kwanza kwanini unazungumzia hao wawili tu(hujawataja na miungu ya wahindi na wachina huko) na wakati umesema hawafanani na hawatofanana? Kipi kinafanya uwazungumzie hao wawili na kutaka kujua yupi wa kweli?
Wewe unaweza kuthibitisha Mungu gani yupi?
 
Kwanza kwanini unazungumzia hao wawili tu(hujawataja na miungu ya wahindi na wachina huko) na wakati umesema hawafanani na hawatofanana? Kipi kinafanya uwazungumzie hao wawili na kutaka kujua yupi wa kweli?

Hao wawili ndio wana wadominate wengine ingawa upo sahihi kusema sikuwazungumza wengine lkn mbona nimewataja marduku a u zeus namaanisha na miungu mengine
 
Keshajibu hili swali mbona unalirudia kila mara..!?

'Watu hawaamini Mungu kwa sababu ya uthibitisho' ni iImani_ Ova
Hajajibu. Kakataa kutoa uthibitisho.

Nikikwambia nioneshe njia ya kutoka Shule ya Uhuru kwenda Ilala, ukaniambia nisiende Ilala niende Kinondoni, hujanionesha njia ya kutoka Shule ya Uhuru kwenda Ilala.

Usitake kulazimisha mtu aliyeshindwa kunijibu awe kanijibu.

Imani unaruhusiwa kuamini hata mavi yako Mungu.

Ukiamini mavi yako Mungu yanakuwa Mungu?
 
1.KUMUUMBA SHETANI:
Hili lilikuwa kosa kubwa sana. Makosa yate yamechepuka kutoka hapa. Shetani anawasababishia watu maovu, then Mungu anawahukumu watu dhaifu. Hapa Mungu inambidi amkamate shetani na kumtokomeza ili maovu yaishe, kama wote wanatoshana nguvu basi wasuluhishe ugomvi wao na kupatana ili maisha yawe ya amani.

2.KUISHI MAFICHONI:
Toka enzi na enzi, Mungu amekuwa akiishi mafichoni, kwanini asijitokeze na kujionesha kwa viumbe vyake? Anaishi mafichoni kwani yeye ni Joseph Kony? Hili limepelekea watu wake kudanganywa na manabii wa uongo na kutapeliwa bure. God come from your hidings and reveal yourself to your people.

3.MAFURIKO YA WAKATI WA NUHU:
Mungu alisababisha mafuriko ili kuangamiza watu waovu na kubakiza watu wema, Yes he did, sasa waovu wa leo wametoka wapi? mbona aliuwa watu wengi bila huruma? Kama mafuriko yalikuwa ni suluhisho la maovu, Yesu na mitume walijia nini? It seems he fought effects instead of causes.

4.SAFARI YA WANA WA ISRAELI:
Mungu aliwatoa wana wa Israel kutoka Misri kwa madai ya kuwapa nchi ya ahadi, matokeo yake aliwaamuru wafanye uvamizi wa nchi za watu(mf. waamori, wamoabu na wakanani). Kwanini asingebadilisha jangwa na kuwatengenezea waisraeli nchi yao? mbona Gadaffi aliweza? Imagine waje wapuuzi hapa TZ wachukue nyumba na ardhi kwa madai kwamba wameagizwa na Mungu, ungereact vipi? WE HAVE TO BE FAIR!

5.KUTOTIMIZA AHADI YAKE KWA ABRAHAM:
Mungu alimwambia Abraham kuwa atampatia uzao wa wana wengi kama nyota za angani au mchanga wa pwani. Sasa hivi ukichanganya walio wa Abrahamu na wasiyo wa kwake bado watu hawawezi kuwa sawa na nyota au mchanga wa pwani. Ata ukijumlisha na waliokufa back to Adam. Atatimiza lini hi ahadi? je kuna muda wa kutosha? mbona watumishi wake wanasema Yesu yuu karibu kuja ili kutamatisha nyakati?

6.KUWEPO KWA MZIO(ALLERGY):
Kwanini watu wengi ambao ni wema wana allergy na vitu alivyoumba Mungu? mbona maandiko yanasema kila alichoumba Mungu ni chema? Kwanini aumbe mimea na wanyama wenye sumu kwa watu wake awapendao? au hakujua?

7.MAJANGA ASILIA:
Kama Mungu aliumba dunia ili iwe sehemu ya amani kwa watu wake na wamwabudu yeye, kwanini kuna matetemeko ya nchi, vimbunga na mafuriko. Kwanini anawauwa watu kikatili hivi? au haya nayo tumsingizie shetani?

8.KUUMBA VIUMBE HATARISHI:
Kwanini Mungu aumbe bacteria, virusi, fangasi na viumbe wengine wanaosababisha magonjwa na kifo? Kwanini hawa viumbe wasingefia kwenye yale mafuriko ya Nuhu ili watu wema alio wabakiza waishi kwa amani? Je hawa viumbe hatari Mungu alimwamuru Nuhu awaingize wawili wawili kwenye safina?

9.JEHANAMU NA MOTO WAKE:
Kwanini Mungu aumbe jehanamu kuteketeza waovu? Kwani hajui kusamehe? Kwanini huruma yake ina kikomo kwa shetani? Kama wewe ni mzazi, mwanao akikukosea na hajaomba msamaha, itabadilisha uhalisia kuwa yule sii mwanao? SHETANI PAMOJA NA WAOVU NI KAZI YA MIKONO YAKE, PRODUCTS OF HIS OWN MIND BEFORE CREATED THEM. So aache kuweka vinyongo na kutamani kulipiza kisasi juu ya kazi yake.

10.KASORO KWENYE MWILI WA BINADAMU:
Kwanini pawepo na mabadiliko hasi kwenye jeni za binadamu(mutation)? kwani hakujua hicho ni chanzo cha viwete??? Kidole tumbo(appendix) ni cha kazi gani? mbona hajatoa maelezo namna ya kukitumia? Na chuchu za mwanaume ni za kazi gani?

TO THE RIGHT WING OR THE LEFT WING WE ARE NEITHER, NOT EVEN AT THE MIDDLE....R.I.P MOBUTU!

===================
Hayo yote amekupa nguvu ya kuyashinda, una nguvu kubwa sana kuliko hayo unayaona kama ni makosa.
 
Back
Top Bottom