Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 85,962
- 146,245
Kwa hiyo mkuu unataka kusemaje ... Tumia kiswahil pulizi
Kwa wingi wa rehema nakuandikia maswali ambayo yanaulizwa mara nyingi na majibu yake kutoka kwangu.
1.Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote aliyeumba ulimwengu huu ndiye anaaminiwa na watu wengi kabisa kuwa yupo. Quran, Biblia, dini nyingi, falsafa zinamtaja huyu.
2. Mungu huyu yupo kweli?
Tukiangalia kimatiki, dhana ya Mungu huyu kuwapo ina tatizo la kimantiki, kubwa sana.
3.Tatizo gani la kimantiki?
Tatizo hilo ni kwamba, dhana ya kuwepo Mungu huyu inajipinga yenyewe.
.
4. Dhana hii inajipingaje?
Dhana hii inajipinga kwa sababu tunaambiwa, upande mmoja, Mungu ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, hana sababu ya kimantiki kuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana kuwepo, dhambi inawezekana kuwepo, matetemeko ya ardhi yanawezekana kuwepo, magonjwa yanawezekana kuwepo, kifo kinawezekana kuwepo, tsunami linawezekana kuwepo n.k, halafu upande wa pili tunaambiwa Mungu kauumba ulimwengu uwe unaruhusu mabaya hayo.
Huku ni kujipinga kusiko kwa kiungu. Ni kama mtu anakwambia kwamba katika jometri ya Euclid, duara haliwezi kuwa pembetatu, halafu akakuambia kuna pembetatu iliyo duara.
Ama amaekosea kusema pembetatu haiwezi kuwa duara, ama amekosea kusema kwamba kuna duara iliyo pembetatu.
Hawezi kuwa sawa pote.
5. Vipi kuhusu habari kwamba Mungu hakutaka ulimwengu uwe na mabaya, ila shetani, uasi, dhambi ndizo zilifanya dunia iwe na mabaya?
Hilo litamaanisha Mungu aliumba ulimwengu unaoruhusu uasi, dhambi, ubaya kuwea kuwepo, kwa nini?
6. Vipi kuhusu habari kwamba Mungu aliruhusu ubaya uweze kuwepo ili watu wawe na uchaguzi na uhuru?
Kwanza kabisa kwa nini uhuru na uchaguzi uwe muhimu kuliko kutokuwepo kwa mabaya?
Ukiwa na mtoto mchanga ambaye hana ujuzi sana, utampa maziwa na sumu ili tu awe na uhuru wa kuchagua? Hapana, utampa maziwa na kuficha sumu asiweze kuifikia. Sasa kwa nini Mungu katuachia watoto wake tuifikie sumu? Kwa nini hakuificha?
Pili, si kweli kwamba tuna uhuru wa kuchagua. Hatuchagui wazazi wetu, hatuchagui kabila letu, hatuchagui tutazaliwa wapi, hatuchagui tutazaliwa lini, hatuchagui tutakuwa na genes gani, hatuchagui tutakufa lini, hatuchagui tuzaliwe au tusizaliwe.
Hii habari ya kwamba tuna uhuru wa kuchagua mema na mabaya ni uongo. Kuna mengine yana mizizi katika genes, mengine ni sehemu ya socioeconomic background.
Tatu, kuna mabaya mengi hayahusiani kabisa na habari za uchaguzi wa mazuri na mabaya, mabaya kama majanga ya kiasili hayana uhusiano wowote na uchaguzi wa mazuri na mabaya.
7. Vipi kuhusu maandiko matakatifu yanayosema Mungu yupo?
Maandiko matakatifu ni jitihada za watu tu kujipangia maisha yao kwa namna inayoeleweka kwao, mengi yana mafundisho mazuri, lakini sehemu nyingi tunaona yanajipinga, yanatetea mabaya, yanaonesha kwamba yameandikwa na watu tu, kuhusu Mungu ambaye hayupo
8. Mbona watu wengi wanaamini kuwepo kwa Mungu?
Kwanza kabisa, habari ya kwamba watu wengi wanaamini kuwepo kwa Mungu ina mushkeli. Watu wengi wangeamini kweli kuwepo kwa huyu Mungu, ujambazi, uuaji, wizi, utapeli, dhambi nyingi sana zisingekuwepo. Kuwepo kwa mabaya haya kwa sana duniani kunaonesha watu wanapenda kujinadi kwamba wanaamini kuwepo kwa Mungu, lakini ndani kabisa, ama wanakubali kwamba hawajui vizuri habari hii au wanaikataa kabisa.
Pili, ulimwengu unatoka katika zama za ujinga na kwenda kwenye zama za elimu na maenddeleo ya habari.Kitu kuaminiwa na watu wengi hakuoneshi kitu hicho ni kweli. Kuna wakati watu waliamini jua linazunguka dunia, lakini sasa watu wengi wamejua dunia ndiyo inazunguka jua. Kwa hiyo kitu kuaminiwa na watu wengi hakumaanishi kuwa kitu hicho ni kweli.
9. Kama Mungu hayupo, ulimwengu umeanzaje? Unaweza kujibu swali hili ili kuonesha kwamba Mungu hayupo?
Sijui. Habari iliyo karibu zaidi kutueleza kuhusu mwanzo wa ulimwengu ni kuunganisha Albert Einstein's Relativity na Quantum Theory kupata theory mpya ya Quantum Gravity. Kwa sasa hatujaweza kupata mahesabu ya kuweza kuondoa singularities fulani.
Lakini hata kama naishia kusema tu sijui jibu la swali hili kimsingi, kutokujua huko hakuna maana kwamba sitajua jibu la uongo.
Nikijua kwamba square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko 2, mtu akiniambia square root ya 2 ni 10 (ambayo ni kubwa kuliko 2), nitajua 10 si square root ya 2 hata kama sijui square root ya 2 ni nini.
Kijana wa miaka 20 akiwa hamjui mama yake mzazi, akajua mama yake mzazi ni lazima awe na umri wa zaidi ya miaka 20 (ili aweze kuwa amemzaa) halafu akaoneshwa mtoto kike wa miezi mitatu, akaambiwa huyu ndiye mama yako mzazi, atajua huyu si mama yake mzazi, bila hata kumjua mama yake mzazi ni yupi.
Kukubali Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote ndiye aliyeumba ulimwengu huu wenye kuweza kuwa na mabaya ni sawa na kukubali mtoto wa miezi mitatu ni mama mzazi wa mtu mwenye miaka 20
10. Sasa tufanye nini?
Tujifunze zaidi, tuchunguze zaidi, tutafute ukweli bila kupenda majibu rahisi rahisi. Tukubali majibu ya kweli hata kama hatuyapendi.
Majibu ya uongo ambayo ni wazi kabisa hayana logical consistency, tuyakatae.
*Angalizo, hapa naongelea umuhimu wa ujuzi, kwa misingi ya mantiki na ukweli. Sizungumzii imani per se. Imani ni sehemu muhimu ya utu na watu wanaruhusiwa kuamini wanavyotaka. Katiba ya nchi na mazimio ya kimataifa yanaruhusu uhuru wa kuabudu.