Kiby
JF-Expert Member
- Nov 16, 2009
- 6,933
- 4,704
Katika uumbaji hakuna makosa labda iwe tu kwa ukaidi kuwe na mabadiliko ya matumizi ya asili. Kama ilivyo sheria na kanunu kwamba ukiiharibu asili utavuna uharibifu.
Mfano aliyetengeneza gari kila kifaa pale kina umuhimu wa kuwepo pale kilipo ili kusudi la matumizi liwe sahihi. Mfano tairi zitakanyaga kila aina ya uchafu, eksosi itakuwa na moto kiasi cha kutoshikika kwa mkono wa binadamu, ndani kuna kinyoyozi cha baridi kali nk.
Kila kitu kipo mahala pake kutimiza kusudi la mtengenezaji. Vivyo hivyo na uumbaji wa ulimwengu. Shetani na malaika watakatifu, wema na waovu, usiku na mchana, jehana na paradiso, maji na moto nk.
Bila hivi kuwepo na viwepo mahala pake lengo la Mungu lisingetimia. Ila sasa linalenga shabaha na ndio maana hata wewe mtoa mada upo mahala pako sahihi. Haiwezekani kuwe na mshindi bila cha kushindaniwa. Hakuna negative bila positive nk.
Siku shetani akikubali kwamba yeye ni shetani na kwamba jehanamu ya moto ndipo mahali pake alipoumbiwa na asidai vinginevyo taabu kwa viumbe wengine zimekoma. Na hili nalo litakuwa ni kwa wakati muafaka ulioamriwa na Muumbaji.
Sent using Jamii Forums mobile app