Kiranga mungu hayupo na huyu wanaemsimulia ni mpuuzi kuliko au mzembe sana na kiumbe cha makusudi sana na kibaya kuliko ka ni kweli kipo
Watu wanajiondoa akili tu,kwa uvivu, kwa ujinga, kwa woga, kwa cognitive dissonance, kwa logical non sequitur, kwa deus ex machina, kwa tradition, kwa vitu viiingi, ili mradi Mungu huyu awepo tu.
Maana maisha yao yote yanazunguka habari za Mungu huyo kuwepo.
Hata wakijua ukwelikwamba hayupo, watabisha.
Leo nilikuwa nasikia habari BBC World Service, kuna Jumuiya ya Wajapani ilihamia South America, Brazil huko ndanindani.
Japan kulikuwa kunajaa watu, watu wakaenda Peru na Brazil.
Basi kuna watu wakasikia Japan imepiga, imeshindwa katika vita vikuu vya pili.
Jumuiya ya Kijapani ikakataa ukweli huo,ikawa inawaita wanachama wake, inawauliza, Japan imeshindwa?
Ukisemaimeshindwa, Jumuiya inakutenga, unatumiwa barua za vitisho, unaonekana huna uzalendo.
Kwa Jumuiya hii, kitu muhimu ilikuwa si ukweli,kamaingekuwa kitu muhimuni ukweli, kujua ukweli ilikuwa kazi rahisi kabisa.
Kwa jumuiya hii, kitu muhimu ilikuwa ni imani kwamba Japan haiwezi kushindwa kitu.
Kwa hivyo, imani ikawa muhimu kuliko ukweli.
Kwao, Japan haiwezi kushindwa.
Sasa na hapa, naona habari hizo hizo. Kuchambua ukweli kuhusu uwepo wa Mungu si kitu muhimu.
Watu wanatakakulazimisha Mungu yupo, kwa imani tu.
Ndio wale wale tu wanaosema "Japan haiwezi kushindwa". Wanasema "Mungu wa milele lazima awepo".
Pathetic!