Makosa 10 aliyotenda Mungu

Makosa 10 aliyotenda Mungu

Kama unadhani kuna nafasi ya kujua ni vp Mungu yupo basi usingehitimisha kuwa Mungu hayupo,ushahitimisha kuwa hayupo na ukasema kabisa kuwa watu wametunga na hakuna kinachoongezeka wala kupungua kwa kumjua au kutokumjua.

Ndiyo maana mie nataka nijue zaidi kutoka kwenye hilo hitimisho lako,nimeuliza kwanini watu wanaamini Mungu hadi sasa hali ya kuwa hakuna athari zozote ya kujua au kutokujua kwenye hili jambo?

Nakuuliza wewe sababu najua ushachunguza kote huko na ukahitimisha kuwa hayuko.

Mimi ndio nijifunze kutoka kwako huwa wanasema hakuwa mwenye kuuliza anajua zaidi kuliko anayeulizwa?

Hata darasani mwalimu anawauliza wanafunzi haimaanishi hajui bali anataka kujua wana uelewa upi?

Wewe kama mwalimu inaonekana unajua mungu yupo nipe njia na mm nimjue umetumia nini? kumfahamu
 
Maneno yako si yapingi upo katika haki wengi hawajui unayoyajua wewe nimependa uchambuzi wako

Jiulize duniani kuna mataifa mangapi mfano wachina wakiomba mungu kwa njia wanayoijua wao wanafanikiwa huku waislam wana mungu wao wakimuomba anawapa na wakristo wana mungu wao wakimuomba anawapa achilia mbali wahindu wabudha wagiriki wiccan masonic wachawi druidism duality atheism judaism na waafrika kabla ya uislam na ukristo

Kwa nini kila mtu akiomba anafanikiwa kwa njia anayoijua mwenyewe?
Tatizo sio unachokiomba ila kinachokupa hayo unayoyaomba,mfano wa kuomba watu waliyokufa na ukapata unachokiomba je,ndio utasema huyo mtu aliyekufa na tukamzika ndio kajibu maombi?
 
Mimi ndio nijifunze kutoka huwa wanasema hakuwa mwenye kuuliza anajua zaidi kuliko anayeulizwa?

Hata darasani mwalimu anawauliza wanafunzi haimaanishi hajui bali anataka kujua wana uelewa upi?

Wewe kama mwalimu inaonekana unajua mungu yupo nipe njia na mm nimjue umetumia nini? kumfahamu
Hapa tunajadiliana hatufanyi mtihani,wewe ushapinga kiujumla hili suala la kuwepo Mungu kwamba hayupo,kwa hivyo mimi hapa naamini jambo la kutungwa tu. Hivyo ndio ulivyomalizana nami.

Sasa mie ndio nayetaka kujua zaidi kutoka kwako,kwanini watu bado wanaendelea kuamini uwepo wa Mungu?
 
Mara oooh Mungu ni Alfa na Omega(mwanzo na mwisho) maana yake anajua hata ya kesho yetu.
Kama anajua hata mambo yajayo alishindwa nini kuwaokoa watu wake visiwa vya Ukerewe wasizame kwani hajui kwamba kuna watu nyuma yao walikuwa wanawategemea?
Kwa hiyo yeye anafurahi sana kuona wajane na watoto mayatima walioachwa na wapendwa wao wakiteseka?
Maana imeandikwa kwamba yeye ni mwenye nguvu na uwezo.
Lakini pia imeandikwa kwamba yeye ni mwenye upendo na huruma.
 
Kitu gani unacho kiomba kinakupa? niambie nijue
Sio unachokiomba kinakupa,mtu aliyekufa hawezi kukupa chochote ukimuomba.

Mie nimepinga suala hilo kwa sababu hauwezi kuomba sanamu na wakati umelichonga mwenye na ulitunza mwenyewe,halafu wewe useme ukiomba linajibu maombi.

Wewe unayesema kuwa hivyo vitu vinavyoombwa vinajibu maombi ndio utueleze vinapata wapi uwezo huo?
 
Maneno yako si yapingi upo katika haki wengi hawajui unayoyajua wewe nimependa uchambuzi wako

Jiulize duniani kuna mataifa mangapi mfano wachina wakiomba mungu kwa njia wanayoijua wao wanafanikiwa huku waislam wana mungu wao wakimuomba anawapa na wakristo wana mungu wao wakimuomba anawapa achilia mbali wahindu wabudha wagiriki wiccan masonic wachawi druidism duality atheism judaism na waafrika kabla ya uislam na ukristo

Kwa nini kila mtu akiomba anafanikiwa kwa njia anayoijua mwenyewe?
Mkuu watu hawajui kufikiri; ndo shida. Waandishi wa vitabu hivi kama wangeandika kwamba kiumbe aliye na uweza ni Tai; waafrica wangekubali .. lakini wenzetu wasingekubali hadi wakafanye utafiti.
Ninachokiamini ni kwamba uhai ni nishati (energy) na nishati huwa haifi bali inabadilika toka mfumo fulani kurudi mwingine.
 
Hawa watu kutoijua misingi ndio huwa kuna waangusha sana,huishia kuyasema yale ambayo kiuhalisia hawawezi kuyathibitisha hata kwa dakika moja.

Mathalani huwa wanasema Uwepo wa Mola ni matokeo ya fikra za mwaadami,ukiwauliza kivipi ? Bro hapo nanga itapaa hupati jibu.
Ni matokeo ya kifikira za binadamu kwa sababu,

Bila uongo wa Muhammad kuwaaminisha watu kuwa kuna Mungu hata wewe usingekuwa na fikira hizi za uwepo wa Allah.
In short Allah ametengenezwa na kupandikizwa kichwani kwako na binadamu aitwae Muhammad kupitia qur'an,taurati,injili na Zaburi.

Kadhalika na kwa wale wa upande wa pili,bila wanadamu waliojiita manabii kumtengeneza Mungu kifikira na kuwapandikiza watu,tusingekuwa na makanisa leo.

Acheni kuwa watumwa wa kifikira,Mungu hayupo.
 
Tatizo lako kubwa unataka kumjua Mungu kupitia theories za wana sayansi ambao kimsingi na wao pia ni binadamu kama wewe.
Hawa wanaohubiri habari za Mungu siyo wanadamu kama wewe?

Unajua kwamba kwa mujibu wa vitabu vyenu kuna maneno yanasema mambo yote yaijazayo dunia yakiwemo nahayo ya wanasayansi ni mali ya Bwana/Mungu?

Ama unapingana na maandiko yenu kwamba mambo ya wanasayansi si miongoni mwa yanayoitwa mali ya Bwana?

Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
 
Pointi yako ya msingi ni ipi?

Oltung'anyi kaongea point nzuri sana hapo juu.

Pointi kubwa kabisa hapo ni kwamba,

Uwezo wa Mungu unaanzia pale ambapo ukomo wetu wa kibinadamu unaishia.Na kadri uwezo wetu wa kimaarifa unapoongezeka ndivyo uwezo wa Mungu unavyotokomea kama vile wazaramo wanavyotokea toka katikati ya jiji la Dar kuelekea Mpiji,Msanga na Chole kutokana na ujio wa wageni.

Uwepo wa maswali mengi yasiyo na majibu hapa duniani ndiyo yamemtengeneza huyo anayeitwa Mungu.

Bahati mbaya sana kwa waelewa huyo Mungu nae amekuja kuwa tatizo badala ya suluhisho.

Ukiingia kiundani unaukosa hata uwepo wake.
 
Kuna swali moja dogo tu nimeuliza kwa wanaosema Mungu yupo, sijajibiwa.

Nawauliza, nawaambia, mnaweza kuthibitisha Mungu yupo?

Thibitsheni.

Mpaka sasa sijapata uthibitisho.

Wanahubiri. Wanapinga. Wanavuruga mjadala. Wanajifaragua.Wanakataa kujibu swali.

Lakini hawajaweza kuthibitisha Mungu yupo.

Mungu anatakiwa asiwe na contradiction. Huyu Mungu wa Biblia na Quran kwa mfano, mtu akiweza kuniondolea contradictions zote zilizopo katika habari zake, sio tu nitakubali, bali pia nitafurahi sana. Contradictions hizo ni hizi.

Kwa uchache.

1. Kwa nini Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote, upendo wote na utakatifu wote, kaumba ulimwengu ambao maovu yanaweza kutokea, wakati alikuwa ana uwezo wa kuumba ulimwengu ambao maovu hayawezi kutokea? Naomba jibu lisiwe kusema maovu yapo kwa sababu ya shetani. Swali linauliza kabla shetani hajaumbwa Mungu alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao shetani hawezi kuwepo. Jibu la swali lisiseme maovu ni matokeo ya dhambi za watu. Mungu angeweza kuumba ulimwengu ambao dhambi haiwezekani. Jibu lisiseme free will, hatuna hiyo inayoitwa free will katika mengi sana na hata kui define tu watu hawawezi.

2. Inakuwaje Mungu awe ndiyo mtoa rehema ya kumjua, anachagua mwenyewe nani amjue na nani asimjue, halafu mtu akishindwa kumjua Mungu, kwa sababu Mungu hajamchagua huyo mtu kumpa neema yake Mungu ya kumjua, huyo mtu aonekane ana makosa, ahukumiwe kuchomwa moto? Baba anawezaje kumhukumu mtoto ambaye hajui kusoma, kama mtoto hajui kusoma kwa sababu baba ndiye aliyemnyima nafasi ya kwenda shule?

3. Inakuwaje mahakama za watu tu zinakataza mtoto kuhukumiwa kwa makosa ya mzazi, lakini vitabu vya Mungu vinasema Mungu anahukumu watoto na wajukuu vizazi hata vizazi? Kwa kosa la mzazi wa zamani sana? Huyu Mungu mbona haki yake haijafikia hata haki yetu watu tu?

4. Mnasema Mungu anajua yote. Anayajua maisha ya mtu yote mwanzo mpaka mwisho kabla hata mtu hajaishi. Na anachojua huyo Mungu kitatokea, ni lazima kitokee. Anavyojua si kama utabiri wa hali ya hewa kwamba kuna 80% ya mvua. Yeye anajua kitu kamili hakina utata. Sasa kama anajua hivyo, ina maana mtu muuaji, alimjua huyu atakuwa muuaji kabla hata hajazaliwa. Na muuaji huyo hawezi kuepuka kuua hata afanye nini. Kwa sababu kuepuka kuua wakati Mungu kashajua huyu ataua ni kum prove Mungu wrong. Sasa kama huyu mtu anaenda kuwa muuaji, na hana jinsi ya kuepuka hilo, tutasemaje ana uhuru wa kuamua na anaua kwa uamuzu wake na atahukumiwa motoni kwa uuaji?

5. Mbona hivyo vitabu vinavyosemwa ni vya Mungu vina contradictions lukuki?

6. Mbona huyo Mungu mnayemsema yupo hathibitishiki? Anajificha asijulikane vizuri kwa nini? Kwa nini hakufanya ulimwengu uweze kumjua vizuri bila uwezo wowote wa kuwepo ubishi juu ya uwepo wake?

7. Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote anaweza kuumba jiwe zito sana kiasi yeye mwenyewe ashindwe kulibeba? Akiweza kuumba jiwe hilo, atakuwa hawezi yote, maana kuna jiwe atakuwa kashindwa kulibeba. Akishindwa kuumba jiwe hilo, atakuwa hawezi yote maana kuna jiwe atakuwa kashindwa kuliumba.

8. Kwa nini Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, ameruhusu kifo kitenganishe wapendanao, baba na mama, wazazi na mtoto, marafiki etc, wakati alikuwa na uwezo, ujuzi na upendo wote wa kuumba ulimwengu ambao kifo hakiwezekani kuwepo?

Kwa nini watetezi wa Quran waajitapa sana kusema vitu fulani vichache vimethibitishwa kisayansi, kuinadi Quran kama kitabu cha ukweli, wakati vingi sana vina contradictions ama vinapingana na sayansi ama havijathibitishwa kisayansi, hawasemi vinapingana nansayansi au havijathibitishwa kisayansi?

10.Kama kuna Mungu kweli, kwa nini karuhusu confusion ya dini nyingi tofauti kuwa na vitabu vingi tofauti vyote vinasema vya Mungu wa kweli?

Kwa leo tuishie na maswali haya 10.

Wwanaosema Mungu yupo wanaweza kujibu?

Kaka hujawahi niangusha kwenye hii mijadala.

Wakikujibu nitag ili nami nije nione majibu hayo.

Yakiridhisha nitasilimu leoleo ama nitaomba kabisa nikabatizwe kwenye maji mengi, palepale ilipozamia ferry ya MV Nyerere.
 
Sio unachokiomba kinakupa,mtu aliyekufa hawezi kukupa chochote ukimuomba.

Mie nimepinga suala hilo kwa sababu hauwezi kuomba sanamu na wakati umelichonga mwenye na ulitunza mwenyewe,halafu wewe useme ukiomba linajibu maombi.

Wewe unayesema kuwa hivyo vitu vinavyoombwa vinajibu maombi ndio utueleze vinapata wapi uwezo huo?

Hapo nimekuonyeshea mungu hayupo wala huitaji msaada

Wee hata ukiomba miti utapata unachotaka hata uombe jiwe utapata unachotaka

Na hiyo nguvu unayo wewe mwenyewe
 
Unaota kweupe yaan unatumia quran kuelezea muda

Nikuonyeshe hiyo quran yako na wewe mwenyewe wote hamjui muda nini?

Leo siku gani na tarehe ngapi?

Hahaha leo tarehe 16/Muharram/1440 Hijiriyya sawa na tarehe 25/9/2018 Miladiyya.

Una swali lingine ?
 
Unaota kweupe yaan unatumia quran kuelezea muda

Nikuonyeshe hiyo quran yako na wewe mwenyewe wote hamjui muda nini?

Leo siku gani na tarehe ngapi?
Bro ulitaka nitumie nini zaidi ? Kama Qur'an inanipatia majibu ya maswali yangu kwa ukamilifu.

Ulitaka nitumie nini bro ?
 
Dawa ya Ukimwi ni ipi?

Na kwa nini aweke magonjwa ilihali mengine tu tiba zake ni gharama mno kiasi cha watu maskini kujifia kwa kushindwa Ku afford?

Kwa nini hakuumba Ulimwengu usiowezekana kuwa na magonjwa?


Katika hadithi imekuja ya kuwa "Hakuna ugonjwa aliouleta Allah aliyejuu isipokuwa una dawa yake". Au kama alivyosema Rasul amani ya Allah iwe juu yake.

Na katika Qur'an Allah mlezi anasema "Kila nafsi itaonja umauti"

Ulimwengu unao ufikiria ungekuwa dhaifu na ndio maana yeye akaumba uwili. Hivi ongekuwaje leo kungekuwa na huzuni tu peke yake ?

Ingekuwaje leo kungekuwa na usiku tuu ?

Ingekuwaje leo kungekuwa na njaa tu.

Ukifikiria ujinga basi fikiria na elimu.

Ama kuhusu gharama sio tatizo kwake yeye,ndio tupo katika dunia ambayo maskini anaishi,maskini ana raha na kinyume chake na tupo katika dunia ambayo tajiri anaishi,tajiri ana huzuni na kinyume chake.
 
Hata mimi biblia ninayo ila iliyotafsiriwa kiswahili,ndiyo hiyo unakusudia na wewe?

Kwanini mungu wa biblia kakubali maandiko yake yaandikwe kwa lugha nyingine wakati mungu wa quran analazimisha maandiko yake yaandikwe kwa kiarabu peke yake?

Hapo ndipo kwenye tatizo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom