Zurri mungu hana lugha kwanini unakuwa kariri kiarabu ni lugha bora?
Kwan mungi ni mwarabu?
Mbona biblia imeandikwa kwa kiswahili kwanini warabu wanakataa hili kuna nini katika quran?
Kaka mimi singumzii hisia mimi nazungumzia elimu na ukweli na haki.
Mtume alipewa utume kwa lugha ya kiarabu kwa maana alikuwa na waarabu,ili ujumbe ufike kwa wepesi na kubainishwa vilivyo.
Qur'an imekuja na misamiati mingi ambayo waarabu walikuwa hawaijui,Qur'an imekuja kuleta maana mpya kwa maneno ya zamani ya waarabu.
Allah ameweka lugha tofauti toafauti ili watu husika wa wasiliane.
Katika taratibu za Allah ambazo hukuti zikibadilika na ndio ukamilifu wenyewe,akimteua mjumbe basi anampa mafunzo kwa lugha yake ili ujumbe uwafikie hadhira husika.
Kaka elimu ina maajabu yake,leo hii ni muhali wewe kutumia lugha ya kiswahili kuandika Qur'an au Hadithi,kwani huwezi kutosheleza maana iliyokusudiwa.
Kwahiyo wanazuoni wamekubaliana kutokana na hali hii,ili kuipa heshima yake Qur'an na Hadithi zikinukuliwa zinukuliwe kwa lugha yake ya asili na hii inakuepusha wewe kukosea katika kupotosha ujumbe jambo ambalo ni dhambi.
Kuna tofauti kati ya tafsiri na tarjama. Tafsiri ni kutoa maelezo kinaga ubaga juu ya kauli husika au tamko husika,na tarjama ni kutoa neno kwa neno toka lugha moja kwenda nyingine. Hapa kwenye tafsiri tumetume ruhusiwa kwa lugha yoyote uijuayo wewe kadhalika kwenye tarjama.
Umezungumzia au umeleta mfano wa Biblia,kitendo cha kusema "mbona...." hii ni njia moja ya kukata tamaa na kutaka huruma njia hii katika haki na elimu haitakiwi kinachotakiwa ni hoja.
Ukweli ni kwamba ni kila lugha inajitosheleza kwa watu wake,na kila lugha inachukua maneno kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine,hali hii haibadilishi ukweli juu ya ubora wa lugha wa kiarabu. Ubora wa lugha ya kiarabu unakuja katika uwezo wa kubainisha mambo,elimu zake na mengine mengi.
Maajabu ya elimu,tunaambiwa elimu haina mwenyewe bali elimu ina watu wake.
Narudi...........