Ndugu, kabla ya uwepo wako, kulikuwa na Mungu? Ulimwengu je?, wanadamu walikuwepo? Unayo kumbukumbu yoyote ya uwepo wa Mungu kabla ya kuwepo kwako?
Umeuliza swali rahisi nina kujibu swali lako hili. Na mimi nikikuuliza swali bro naomba unijibu.
Mim sio binadamu wa kwanza kuumbwa,kwa maana kabla yangu mimi kulikuwepo wazazi wangu.
Mola alikuwepo sababu alikuwa ameshawaumba walionitangulia.
Sina kumbukimbuku sababu sababu sikuwepo na hili halibadilishi ukweli.
Kwani Mola wenyewe anasema "Ilipita kitambo dahari binadamu hakuwa ni kiumbe chenye kujulikana...."
Akasem tena Mola muumba katika sura hiyo hiyo :
"Kisha tukampa uongofu wa njia,akipenda ashukuru na akipenda akufuru"
Hapa nakupa hoja ya kiakili tena ya kihesabu.
Chukulia una seti A yenye elementi a,b,c,d,e. Tunasema seti A imeundwa na elementi hizo nilizo zitaja. Katika seti hii kuna vitu viwili,kuna tokeo la kupatikana seti A iliyoundwa na vijenzi tajwa na kuna kile chanzo kilichopelekea kuwepo kwa seti A.
Kawa maana kupatikana kwa seti A lazima kuwepo na yule mfanyaji ambaye nyuma yake hakuna mwingine.
Hapa kimahesabu tuna sema kuna Universal set,seti ambayo imejumuisha seti nyingine kama vile B,C,D,E,F....
Hii universal set ndio ambaye kutoka kwake amepatikana A,B,C,D,E,F na wengine. Sasa kwenu nyie mnaojiita wafikiriaji wakuu fikra zenu zimeishia hapo.
Mchakato wa ujenzi wa seti A ni ule ule mchakato wa ujenzi wa Universal se (U). Kama una amini A,B,C,D,.... ni matokeo ya U. Basi lazima kutakuwa na yule aliyekuwepo kabla ya U.
Ukikataa kuwepo yule aliye nyuma ya U. Basi inabidi ukubuli kuna seti zaidi ya U na itaendelea.
Na je zaidi ya U kuna nini ?
Mathalani,ikitoka 1 inafata 2 kisha inafata 3. Je nyuma ya moja nini ? Bila shaka ni 0 na hi sifuri ni kitu gani ?
Mfano mwingine ni huu :
1+1+1= 3 je inawezekana 1+1+1=0 ?
Ukinipa jibu nakuja kumalizia kazia yangu.