Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 87,466
- 151,516
Wewe huijui mantiki wala shahada.Nimemaliza kazi ya kukuonyesha kwamba huijui mantiki bali unajifaragua na msamiati upatikanao katika mantiki bila kuufanyia upembuzi yakinifu na mazingatio.
Kwa maana bila kuijua mantiki, huwezi kuijua shahada.
Na kwa hivyo, hata katika Waislamu haupo.
Kwa sababu huwezi kuwa Muislamu bila kuijua shahada.
Siyo tu huelewi kwamba Mungu hayupo.
Bali, hata huyo Mungu unayemsema yupo humuelewi wala kumkubali kwamba yupo.
Utamkubali vipi bila mantiki? Na wewe unaita mantiki ujinga?
Uanaita kumkubali Mungu wako mjinga.
Unaita shahada ujinga.