BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,377
- 8,120
Akizungumza katika hafla ya kukaribishwa jijini Dodoma, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda amesema kutokana na Serikali kutenga Bajeti kwaajili ya miradi ya Maendeleo kwaajili ya Wananchi, Chama kinawataka Mawaziri kuwasilisha Ripoti ya kazi zao katika Sekretarieti yake .
Ameongeza kuwa Waziri yeyote atakayekaa zaidi ya Robo Mwaka (Miezi Minne) bila kufanya kazi, bila kuwa na Ripoti ya utekelezaji wa kazi za Wizara na Ilani ya chama hicho atachukuliwa hatua kwasababu sasa ni wakati wa kuwatumikia Wananchi.